SIASA Onyo alilolitoa Rais Magufuli kwa Magazeti mawili ya Tanzania


Rais Magufuli leo January 13 2017 akiwa Shinyanga ametoa onyo kwa magazeti mawili ya Tanzania ambayo anasema yamekua yakiandika habari za uchochezi na kupotosha Wananchi.
Bila kuyataja magazeti yenyewe, JPM amenukuliwa akisema ‘Serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya mambo ya uchochezi, hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la kuweka maneno ya uchochezi, chini ya utawala wangu hilo halitokuwepo
Kuna Magazeti mawili tu kila ukisoma wao ni kuchochea tu, ikizungumzwa habari hii wao wanageuza…… nasema na nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia na wasikie, wasiposikia wasisikie……. Magazeti mengine na vyombo vyote vingine vinatoa uchambuzi mzuri sana
Rais Magufuli amesema uwepo wa amani kwenye taifa la Tanzania ndio unaowezesha wawekezaji mbalimbali kuja wakiwemo wa kiwanda cha Fresho cha kutengeneza mifuko ya kubebea bidhaa za chakula Tanzania na kiwanda cha jambo cha kuzalisha vinywaji baridi Shinyanga kujengwa hivyo bila amani hakuna Mwekezaji ataweka pesa zake Tanzania.

Mzee Majuto : Ntaendelea Kuigiza Hadi Siku Yangu ya Kifo Changu

Mkongwe wa Filamu za Kibongo nchini, aliyejipatia umaarufu kwa kuigiza vichekesho, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’, aliyeanza kuagiza mwaka 1958 akiwa na miaka 10, ambaye mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji na kumrudia Mungu, amesema ataendelea kuigiza hadi anakufa kwa sababu uigizaji upo kwenye damu na hii inadhihirishwa wazi kwani ni miaka 58 sasa ya uigizaji wake na fani hii ameianza akiwa darasa la pili.

Majuto alizungumza hayo Dar es salaam Jana.Alisema hawezi kukubali kuona fani inachezewa na watoto, hivyo ataendelea kuigiza hadi siku atakayokufa kwa sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na kuigiza.

”Kuigiza kwangu ni kama maradhi vile, hivyo sidhani kama naweza kuacha, siwezi kukaa pembeni  sanaa ikawa inachezewa na watoto sitaki kabisa,  nitaendelea kuigiza hadi nakufa,” alisema Majuto.

Mzee Majuto aliongeza ataendelea kuigiza  ili kuhakikisha anapata chipukizi ambaye anaweza kufanya kile alichokuwa anakifanya yeye hapo baadae.

Alisema bado hajapata mtu wa kurithi mambo yake katika tasnia hiyo, hivyo hawezi akakurupuka kuachana na kazi hiyo bila ya faida ambayo kwa upande wake ni kupata mrithi.

Mganga Auawa Kwa Kuchomwa Visu........Kisa ni Kuwatapeli Watu Kwamba Atawapa Utajiri

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la DOTTO MWAIPOPO mkazi wa Kafundo – Ipinda wilayani Kyela Mbeya ameuawa kwa kuchomwa kisu ubavu wa kulia na BONIPHACE KISWAGA Mfanyabiashara na Mkazi Chaugingi Mkoani Njombe kwa madai ya kufanya utapeli.

Taarifa ya Polisi Mkoa wa Mbeya imesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11.01.2017 majira ya saa 4 usiku katika Kitongoji cha Ipinda – Chini, Kijiji na Kata ya Ipinda, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu kuwatapeli watuhumiwa pesa ambazo kiasi halisi bado hakijafahamika kwa madai kuwa yeye ni mganga wa kienyeji na atawasaidia kuwa matajiri.

Aidha katika tukio hilo mtuhumiwa huyo BONIPHACE KISWAGA alijeruhiwa kwa kupigwa na wananchi na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa matibabu. Watuhumiwa wengine wawili ambao walikuwa pamoja na mtuhumiwa aliyekamatwa walikimbia na msako mkali unaendelea.

NEC: Mbunge Peter Lijualikali kuendelea kuwa mbunge licha ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela

Mjadala umeshika kasi mitaani, mitandaoni na kila mahali baada ya Mahakama ya wilaya ya Kilombero kumhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila faini Mbunge Wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Mbunge huyo, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi 1, 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.

Imeelezwa  kuwa kwa pamoja walifanya fujo kinyume na kifungu namba 89 kifungu kidogo cha kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, ambapo washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya kesi kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka ukathibitisha bila kuacha shaka.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan ameibuka na kukata kiu ya wananchi ya kutaka kujua endapo  baada ya hukumu hiyo Mhe. Lijualikali ataendelea kuwa mbunge.

Akihojiwa na TBC One wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili jana usiku,  Bw. Kailima aliweka bayana kwamba mbunge huyo ataendelea na wadhifa wake kwa kuwa sheria inasema ili kupoteza kiti ni lazima uwe umepewa adhabu ya kifungo cha ZAIDI ya miezi sita jela.

"Ibara ya 67(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza mambo yanayotoa sifa ya kuwa Mbunge kutoka  madarakani ni kifungo cha zaidi ya miezi sita jela. Huyu bwana kafungwa miezi sita kwa hiyo bado hajapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge akiwa gerezani na baada ya kumaliza kifungo chake", alisema Bw. Kailima.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya January 12

VIDEO: Madai yaliyoibuka ndani ya CUF kuhusu wizi wa fedha

Wakati mgogoro ndani ya chama cha wananchi CUF ukiwa haujamalizika na suala hilo kuwa bado lipo mahakamani, leo January 10 2017 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, Julius Mtatiro amekutana na waandishi wa habari na kutoa kueleza kuwa chama hicho kimeibiwa fedha za ruzuku kiasi cha Tsh Milioni 369.37.
Mtatiro ameeleza kuwa fedha hizo zilitoroshwa kutoka hazina ya serikali kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania January 05 2017 na kuingizwa kwenye akaunti yenye jina la The Civic United Front ambapo anasema akaunti hiyo haikuwahi kuiidhinishwa na Bodi ya wadhamini ya CUF ili ipokee ruzuku kutoka Serikali Kuu. Unaweza kubonyeza play hapa chini.

Eric Omondi ni mchekeshaji kutoka Kenya ambaye anakupa uhakika wa kucheka ukimsikia au kumtazama Msanii huyu kairudia movie ya ‘The gods must be crazy’ na ameeiita ‘The Gods are not crazy we are’.Eric Omondi The GoDs are not CRAZY We Are!!

Magazeti ya Tanzania January 09, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo


img_20170109_050446
img_20170109_050503
img_20170109_050519
img_20170109_050534
img_20170109_050549
img_20170109_050626
img_20170109_050643
img_20170109_050700
img_20170109_050714
img_20170109_050729
img_20170109_050743
img_20170109_050756
img_20170109_050812
img_20170109_050827
img_20170109_050842
img_20170109_050857
img_20170109_050914
img_20170109_050928
img_20170109_050943
img_20170109_051000
img_20170109_051013


img_20170109_050253
img_20170109_050317
img_20170109_051026

Pwani: Bunduki Ya Kivita SMG Iliyokuwa Imeibiwa na Mfanyakazi wa Hifadhi ya Saadani Yakutwa Kichakani

Silaha ya kivita aina ya SMG na risasi 30 mali ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani vimekutwa vimefichwa kwenye kichaka jirani na Mto Kitame katika Kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 
Silaha hiyo inadaiwa iliibiwa kwenye Geti la Gama saa tisa usiku Desemba 24, mwaka jana wakati askari wa hifadhi hiyo, Jackson Shirima (23) akiwa kazini. 
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Bonaventura Mushongi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya askari huyo kutoka zamu ya lindo la geti hilo na kujipumzisha kwenye moja ya mahema akiwa na silaha hiyo. 
“Huyu askari alikuwa zamu na kama ilivyo ada huwa wanapokezana zamu ya ulinzi hivyo alitoka na silaha yake akaenda kujipumzisha kwenye hema maana hifadhini hutumia mahema na alipitiwa na usingizi na ndipo ilipoibiwa na mtuhumiwa aliyewahi kuwa mtumishi wa hifadhi hiyo,” alisema. 
Mushongi alibainisha kuwa baada ya wizi huo, askari kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) walianza msako na kupitia taarifa ya msamaria mwema walimkamata mtuhumiwa huyo, mkazi wa Tegeta Kibaoni ambaye alikwenda kuonyesha alipokuwa ameificha kichakani ikiwa na risasi 30. 
Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk James Wakibara alisema wameshtushwa na tukio hilo kwani halijawahi kutokea na kwamba, zaidi ni baada ya kukuta mtuhumiwa huyo aliwahi kuwa mtumishi wao na aliacha kazi miezi kadhaa iliyopita yeye mwenyewe. 
Dk Wakibara alilishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano lilioutoa toka siku ilipoibiwa silaha hiyo hadi ilipopatikana.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog