Rais Magufuli leo January 13 2017 akiwa Shinyanga ametoa onyo kwa magazeti mawili ya Tanzania ambayo anasema yamekua yakiandika habari za uchochezi na kupotosha Wananchi.
Bila kuyataja magazeti yenyewe, JPM amenukuliwa akisema ‘Serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya mambo ya uchochezi, hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la kuweka maneno ya uchochezi, chini ya utawala wangu hilo halitokuwepo‘
‘Kuna Magazeti mawili tu kila ukisoma wao ni kuchochea tu, ikizungumzwa habari hii wao wanageuza…… nasema na nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia na wasikie, wasiposikia wasisikie……. Magazeti mengine na vyombo vyote vingine vinatoa uchambuzi mzuri sana‘
Rais Magufuli amesema uwepo wa amani kwenye taifa la Tanzania ndio unaowezesha wawekezaji mbalimbali kuja wakiwemo wa kiwanda cha Fresho cha kutengeneza mifuko ya kubebea bidhaa za chakula Tanzania na kiwanda cha jambo cha kuzalisha vinywaji baridi Shinyanga kujengwa hivyo bila amani hakuna Mwekezaji ataweka pesa zake Tanzania.
0 comments:
Post a Comment