Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la DOTTO MWAIPOPO mkazi wa Kafundo – Ipinda wilayani Kyela Mbeya ameuawa kwa kuchomwa kisu ubavu wa kulia na BONIPHACE KISWAGA Mfanyabiashara na Mkazi Chaugingi Mkoani Njombe kwa madai ya kufanya utapeli.
Taarifa ya Polisi Mkoa wa Mbeya imesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11.01.2017 majira ya saa 4 usiku katika Kitongoji cha Ipinda – Chini, Kijiji na Kata ya Ipinda, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.
Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu kuwatapeli watuhumiwa pesa ambazo kiasi halisi bado hakijafahamika kwa madai kuwa yeye ni mganga wa kienyeji na atawasaidia kuwa matajiri.
Aidha katika tukio hilo mtuhumiwa huyo BONIPHACE KISWAGA alijeruhiwa kwa kupigwa na wananchi na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa matibabu. Watuhumiwa wengine wawili ambao walikuwa pamoja na mtuhumiwa aliyekamatwa walikimbia na msako mkali unaendelea.
0 comments:
Post a Comment