|
Meneja wa Barclays tawi la Iringa Shamsa Abdul-Latif wakati wa mafunzo hayo |
|
Akifafanua namna wanafunzi wanavyoweza kujiwekea akiba kwa kuzingatia mahitaji yao ya msingi |
|
Wakati mada zikiwasilishwa |
|
Maafisa wa benki hiyo katika picha |
|
Mshauri wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Julius Ngwilla |
|
Afisa Mikopo, Charles Mwakameta alipokuwa akifafanua njia mbalimbali za kutunza fedha |
|
Wakati wa Majadiliano ya vikundi |
|
Katika majadiliano ya vikundi |
Katika
majadiliano yao, wanafunzi hao walitaja vipaumbele vya familia zao kwamba ni
malazi, chakula, maji, shule na mavazi hata hivyo wakasema pamoja na umuhimu
wake, matumizi ya pombe na vitu vingine vya anasa yanadhohofisha upatikanaji wa
huduma hizo kwasababu ya kukosa akbia.
Meneja
wa tawi hilo, Shamsa Abdul Latiff alisema katika mafunzo hayo yanayotarajiwa
kuwanufaisha wanafunzi wa shule nyingine za mkoani hapa kwamba, kila mtu
anaweza kufikia ndoto ya mahitaji yake kama atakuwa na nidhamu ya matumizi ya
fedha.
Aliyataja
mahitaji hayo kuwa ni pamoja na kumudu gharama za elimu, ujenzi, ununuzi wa
vyombo mbalimbali vya usafiri, vyakula na huduma nyingine muhimu kwa matumizi
ya binadamu.
“Wanafunzi
mnaweza kujiwekea akiba kutokana na kidogo mnachopewa na wazazi wenu kwa ajili
ya matumizi yenu ya kila siku muwapo shuleni, lakini pia mnaweza kusaidia
kuwashauri wazazi na walezi wenu kujiepusha na matumizi yasio ya lazima ili
mpate akiba,” alisema.
Meneja
huyo alitoa mfano akisema katika kila Sh1,000 anayopewa mwanafunzi kwa ajili ya
matumizi yake shuleni anaweza kujiwekea akiba ya hadi nusu ya kiasi hicho
ambacho kwa mwaka kinaweza kuwa kikubwa.
“Ukimudu
kuweka akiba, kwa mfano ya Sh 500 kila siku, mwisho wa mwezi utakuwa na Sh 15,000
na mwisho wa mwaka utakuwa na zaidi ya Sh 180,000 na kwa miaka sita ya elimu ya
sekondari utakuwa na zaidi ya Sh Milioni moja unayoweza kuitumia kwa mambo
mengine ya kimaendeleo,” alisema.
Latiff
alisema zipo njia ya nyingi za kuhifadhi akiba ya fedha na akaitaja iliyo ya
uhakika na usalama zaidi kuwa ni kwa kupitia benki.
Awali
Afisa Mikopo na Ufunguzi wa Akaunti wa benki hiyo, Charles Mwakameta alizitaja
njia nyingine za kutunza fedha kuwa ni pamoja na kuficha sehemu mbalimbali
majumbani kama kwenye mito na vitandani.
Zingine
ni pamoja na kuhifadhi kwa kununua bidhaa mbalimbali kama vyakula kwa lengo la
kuziuza pale unapohitaji fedha, kwa marafiki, kwenye makampuni ya simu, vikundi
vya upatu na vyama vya kuweka na kukopa.
0 comments:
Post a Comment