hata kama;;;
MAPENZI YA KWELI |
Mapenzi ya kweli
Kwenye nyumba tunazoishi mara nyingi
tumekua tukifuga na kuishi na Paka au Mbwa kitu ambacho ni kawaida na ni nadra
sana kukutana na mtu anaeishi na au kufuga viumbe ambavyo ni hatari kwa maisha
ya binadamu mfano Nyoka.
Sasa hii inaweza
kutushangaza kwa sababu kuna Simba ajulikanaye kama mkuu wa msitu alihamishia
makazi yake kwenye nyumba ya Melanie Griffith mwigizaji ambaye kwa sasa ana
umri wa miaka 57.
Unaambiwa Simba
huyu alihamia kwenye nyumba hiyo toka Melanie akiwa na umri wa miaka 14 huko
Sherman Oaks,California Marekani ambapo mama yake Melanie ni mwigizaji Tippi
Hedren na baba yake wa kambo kwa muda huo Noel Marshall.
Kingine cha
kufahamu ni kwamba hii familia ilikuwa inamlea Simba huyu nyumbani ambae
alipewa jina la Neil kama wanyama wengine, mfano Mbwa au Paka.
Picha za Melanie na mama yake wakiwa
wanacheza na simba huyo ziliwekwa kwenye jarida la ‘Life Magazine‘ mwaka 1971 ambapo zilikua
zinaonesha mtoto huyo kuwa na ukaribu mkubwa na Simba na hata kulala na
kuogelea nae.
Mama Melanie
aliyeigiza kwenye filamu ya ‘The
Birds’ miaka 8 baada ya kupigwa kwa picha hizo
alionekana pia kupenda kucheza na mnyama huyo pori.
Simba huyu alikuja kuishi na familia hiyo
wakati mama Melanie na baba wakiwa wanatengeneza filamu Afrika ambapo kwenye
matembezi yao waliona kuna nyumba yenye Simba ambao hawana makazi mazuri ndipo
walipoamua kumchukua Simba huyo kutengeneza filamu inayohusiana na Simba.
Kweli baadae
walitengeza filamu iliyoitwa ‘Roar’ ambapo ilitolewa kwenye miaka ya 80 ambapo
kwenye mahojiano yaliyofanywa mwezi April mwaka 1982 na The Guardian, U.K
ilitangazwa filamu hiyo ya Roar.
Griffith
alielezea jinsi alivyopata alama za usoni na kusema Simba huyo hakumaanisha
kumuumiza, aliendelea kusema ‘Baada ya kukaa miaka 7 na Simba unasahau kama
Simba ni mnyama na pia ni hatari kuwa nao karibu, katika utengenezaji wa filamu
hamna mnyama alieumia sema watengenezaji wengi wameumia na wapo hospitali’
Mama wa Griffith ambaye
sasa ana miaka 85 alipendezwa sana na uhusiano wa Griffith na wanyama mpaka
akaamua afungue kituo cha kulea wanyama ambao wamekosa malezi kiitwacho
‘Shambala Preserve’ kwenye mjia wa Acton California Marekani mwaka 1972.
|
0 comments:
Post a Comment