Mtoto ashukiwa kuwaambukiza wengi Mali
Shirika la afya duniani WHO linasema kwa msichana wa umri wa miaka
miwili ambaye alithibitishwa kuwa mgonjwa wa kwanza wa ebola nchini Mali
alisafiri kilomita kadha kwa basi nchini humo huku akionyesha dalili za
kuugua ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 40 ambao walikaribiana naye
wametengwa. Huenda msichana huyo alisafirishwa kwenda nchini Mali na
nyanyake baada ya mazishi ya mamake nchini Guinea moja ya nchi ambazo
zimeathirka pakubwa na ugonjwa wa ebola.Utawala nchini Mali sasa umethibitisha kuwa msichana huyo ameaga dunia kwenye hospitali moja mjini Mayes alikokuwa akipewa matibabu.
Mwandishi wa BBC anayehusika na masuala ya afya anasema kuwa huenda ikawa changamoto kubwa kuwapata watu wengine ambao walikaribiana na msichana huyo.
0 comments:
Post a Comment