UJERUMANI BINGWA KWA MARA YA 4 KOMBE LA DUNIA, YAMFUNGA MESSI BILA HURUMA
Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia baada ya kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya nne nchini Brazil usiku huu.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Low akinyanyua juu Kombe la Dunia.
Mario Gotze akiifungia Ujerumani bao pekee na la ushindi dhidi ya Argentina usiku huu.
Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia na Gotze.
Aliyekuwa
mchezaji wa Barcelona, Carles Puyol (kushoto) na modo wa Brazili,
Giselle baada ya kuleta Kombe la Dunia uwanjani kabla ya mechi ya
fainali kati ya Argentina na Ujerumani kuanza.
Meesi na Neuer wakiwa na tuzo zao.
**********
TIMU ya Ujerumani imetwaa Kombe la Dunia 2014 kwa ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Argentina katika muda wa nyongeza baada ya suluhu kwenye muda
wa kawaida wa dakika 90.
Bao hilo lililoipa ushindi Ujerumani limefungwa na Mario Gotze
dakika ya 113 ya mchezo na kuifanya timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia mara
ya nne baada ya mwaka 1954, 1974 na 1990.
Katika michuano hiyo, kipa wa Ujerumani, Manuel Neuer ametwaa tuzo ya
kipa bora, Lionel Messi wa Argentina akitwaa tuzo ya mchezaji bora huku
mshambuliaji wa Colombia, James Rodriguez akiwa ndiye mfungaji bora
baada ya kutia kambani mabao sita.
0 comments:
Post a Comment