TAARIFA KAMILI YA AJALI YA BASI KUGONGANA NA LORI NA KUUA WATU 17 DODOMA LEO NA KUJERUHI 56
MAREHEMU NA MAJERUHI WAKIWA KATIKA ENEO LA AJALI BAADA YA AJALI KUTOKEA
Watu
17 wamekufa papo hapo na wengine 56 kujeruhiwa vibaya baada ya basi
walilokuwa wakisafiria kutoka Mpwapwa kwenda Jijini Dar-es-Salaam
kugongana uso kwa uso na Lori wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo asubuhi.
Ajali hiyo ambayo imeua madereva wote wawili, imetokea majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la Pandambili wilayani Kongwa mita chache kutoka mahali ambako ilitokea ajali iliyosababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime Marehemu Chacha Wangwe.
Basi lililopata ajali ni aina ya Scania mali ya Kampuni ya Morobest lenye namba za usajili T258 AVH ambalo liligongana na Lori lenye namba T390 CKT lililokuwa likivuta tela T820 CKU ambalo lilikuwa na shehena ya mabomba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo kamili chake ni uzembe uliofanywa na dereva wa Lori ambaye kwa sasa ni marehemu.

Marehemu Waliotambuliwa ni pamoja na dereva wa loriGabriel Lemanya Mkazi wa Ndebwe wilayani Chamwino,dereva wa basi Said Lusogo, kondakta wa basi Omari Mkubwana Mikdadi Zuberi ambaye alikuwa ni utingo wa Lori.
Wengine ni Justin Makasi, Gabriel Chiwipe, Marick Masawe, Melina Maliseli, Wilson Sudai wote wakazi wa Mpwapwa na watu wawili waliotambulika kwa jina moja moja ambao ni Christina mkazi wa Mpwapwa na Nasibu mkazi wa Kongwa.
Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kongwa na wengine katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma, huku majeruhi nao wakilazwa katika hospitali hizo kwa matibabu
0 comments:
Post a Comment