MWANAJESHI MMOJA AFA MWINGINE AJERUHIWA KTK AJALI YA MAPOROMOKO YA MAWE MLIMA KILIMANJARO
Jana majira ya saa kumi alfajiri
kumetokea ajali ya maporomoko ya mawe katika eneo la juu la Mlima
Kilimanjaro la Hans Meyer na kusababisha kifo kwa mwanafunzi Malata
Thomas kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli .
Aidha, mwanafunzi mwingine Matenga S.J alivunjika mguu wake na anaendelea na matibabu katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.
Wanajeshi hawa walikuwa pamoja na wenzao 265 walikuwa katika mafunzo yao ya kawaida ya ukakamavu katika Mlima Kilimanjaro.
AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJINYONGA NA KHANGA
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Olen Gadau (26) mkazi wa kijiji cha Igoma
mkoani Iringa alikutwa ndani ya jiko akiwa amefariki dunia mara baada ya
kujinyonga kwa kutumia kipande cha khanga.
0 comments:
Post a Comment