CHRISTINA SHUSHO ATUMIA MILLIONI 4 KUTENGENEZA VIDEO MOJA, IANGALIE HAPA NA MSIKILIZE AKIELEZA SABABU ZA KUTUMIA GHARAMA HIYO

.
Blogger Ambwene Michael na Christina Shusho.
Kilio changu kila siku waimbaji wa muziki wa injili wabadili uelekeo wao hasa katika kutengeneza video zenye ubora mzuri.Leo nikipiga story na Christina Shusho kupitia Chomoza ya Clouds Tv amefunguka na kueleza wazi gharama ya utengenezaji wa video yake
"Nataka nimjue" ametumia milioni 4 hadi kukamilika.Video hii imetengenezwa na kampuni kubwa nchini Kenya (Link Video Global) chini ya director wa mkubwa J Blessing.Msikilize Christina Shusho akizungumza na mimi na tazama video hiyo.Muziki wa injili nao unahitaji ubora kuanzia utunzi,production ya audio na video kwasababu ndiyo itakayokutangaza kimataifa
Msikilize Christina Shusho akieleza kwa nini ameamua kutumia milioni 4 kutengeneza video moja hapo chini.

MASANJA MKANDAMIZAJI YUKO MAREKANI KUHUBIRI

Masanja alipokuwa jijini New York alipokwenda kwa mara ya kwanza.
Mungu ameendelea kufungua milango kwa mchekeshaji wa kundi la Original Comedy ambaye pia anafanya kazi za kumuhubiri Mungu kijana Emmanuel Mgaya au mwite kwa jina lake la kazi Masanja Mkandamizaji ambaye kwasasa yupo nchini Marekani kwa huduma ya kimungu ambako amealikwa kwa kazi hiyo ikiwa pamoja na kuzungumza na vijana katika miji mitatu ya California, Minnesota pamoja na Dallas.

Masanja amemshukuru Mungu kwa nafasi anayoipata hasa ikizingatiwa kwamba hii ni
mara yake ya pili ambapo amekiri kuwa Yesu ndiye anafanya yote haya katika maisha yake kwakuwa hajawahi kufikiria kwamba siku moja atakanyaga Marekani maana tangu ameanza kazi ya uchekeshaji hajawahi kufika huko ila alipompokea Yesu anaona milango ikifunguka zaidi na zaidi. Masanja akiwa huko akimaliza kilichompeleka amepanga kurekodi baadhi ya vipande vya vipindi vya Original Comedy ambavyo itakuwa kuwafundisha watanzania na vijana nini watu wa Marekani wanafanya.

Aidha katika mahojiano na Silas Mbise kupitia kipindi cha
Gospel Celebration cha WAPO Radio Fm mda mchache uliopita mwigizaji huyo atakuwa nchini Marekani kwakipindi cha mwezi mmoja amemtaka mtangazaji huyo kuoa maana kuchelewa kwake kunafanya wengine kuchelewa mwe mwe mwe Silas si akajikausha ha ha ha, kijana akaishia kukata simu na kusema wakati wa Bwana ukifika atafanya hivyo. Ila kweli anatuchelewesha kha!

VIONGOZI WA KIDINI KENYA KUONGOZA MAOMBI YA KITAIFA JUMANNE

Rais Uhuru Kenyatta na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la mpwa wao marehemu Mbugua Mwangi na mchumba wake Rosemary Wahito ambao waliuawa katika tukio hilo la kigaidi. Picha na Daily Nation Kenya.
Viongozi wa kidini nchini Kenya wanatarajia kufanya maombi kwa taifa lao siku ya jumanne ijayo katika viwanja vya KICC kuanzia majira ya saa nne asubuhi. Akitoa tangazo hilo katibu mkuu wa taasisi ya jumuiya ya Kikristo nchini humo National Christian Council of Kenya (NCCK) bwana Peter Laranja amewataka watu kutoka madhehebu yote pamoja na viongozi wa dini zote kukutana hapo kwa ajili ya kuiombea Kenya.

Laranja amewataka wakenya kuonyesha umoja na nguvu kwa pamoja licha ya hayo ambayo yametokea katika jengo la biashara la Wastegate ambalo watu zaidi ya 60 wameripotiwa kufariki dunia wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya baada ya watu zaidi ya 10 ambao inaaminika ni wanachama wa kundi la kigaidi la Al Shabaab kuvamia jengo hilo mchana wa jumamosi iliyopita.


Aidha pia viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo aliyekuwa waizir mkuu wa kwanza wa nchi hiyo cheo ambacho hakipo tena kwa wakati huu mheshimiwa Raila Odinga amekaririwa akisema kuwa  magaidi wasiwagawe wakenya bali waendelee kuonyesha umoja wao na kumalizia kwakusema kwamba fikra na maombi yake yafike kwa f
amilia zote zilizopoteza ndugu zao katika tukio hilo.

KONGAMANO LA UVUVIO AFRIKA 2013

Tarehe 31 inajongea, na ndio mwisho wa kulipia gharama za kadhaa za kukuwezesha ushiriki nchini Afrika Kusini, ambapo kwa mwaka huu uvuvio huu wa siku sita utafanyika huko ukishirikisha viongozi mbalimbali kutoka makanisa mbalimbali barani Afrika. GK imekufikishia taarifa, kazi ni kwako.

MAKALA: CECILE KYENGE, TOKA CHINI KWENDA JUU, KUTOKATA TAMAA KWAMTOA

Dakta Cecile Kyenge katika mojawapo ya mikutano. ©Reuters
Nilipokuwa mtoto, na nikakosea kisha mama aniseme, nilitamani anipige tu mambo yaishe – unajua ni namna gani maneno yanachoma. Ndio maana hata kuna utani kwamba mzaramo anaweza kukusema hadi ukafa. Haya yote ndio yananirejesha kwa Cecile Kyenge, mwanamama wa kwanza kuwa waziri mweusi nchini Italia.

Kila nikimtazama mama huyu mzawa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Napata ahueni – ahueni kwamba hata kama watu wakikupiga kwa maneno, bado unaweza kutekeleza yale uliyonuia kufanya bila chembe ya wasiwasi.

Wanaomsema wanatokea kila upande – kuanzia viongozi wenzake, hadi wananchi ambao anawatumikia. Ugumu anaokutana nao, unaweza pia kulinganishwa na ugumu anaoupata mchezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Mario Ballotelli – ambapo amewahi kuzungumzai historia yake ya kukachwa na wazazi wake akiwa mdogo, na kuasiliwa na familia mojawapo ya wataliano kabla hajawa raia na hatimaye kulitumikia taifa lake jipya kupitia timu ya taifa, akisakamwa na maneno lukuki kuanzia ndani hadi nje ya uwanja.

Balotelli bado ni kijana, na kwa utukutu wake, ameshatoa majibu mengi ikiwamo ya mkato na hata kuwa mkali zaidi pale anapochukizwa na hata bosi wake.

Ninachokiona ndani ya huyu mama ndicho kinanivuta hasa kuandika hivi, na tayari ninajifunza kitu kwake. Ni mvumilivu, asiyetetereka (japo inavunja moyo sana) wala kushambulia wale ambao wanamtuhumu kwa mambo mengi kwenye nafasi yake ya uwaziri anayeshughulikia uhamiaji.
Dakta Kyenge ofisini. ©Gregorio Borgia/AP
Matukio;
Makamu wa Rais wa senate nchini humo ameshawahi kunukuliwa kisema kuwa anapenda wanyama, na kila akimuangalia Cecile haoni tofauti na nyani aina ya Orangutan. Kauli hiyo ya kiongozi wa juu ilijibiwa kwa ufupi na Bi Kyenge ya kwamba, kama kiongozi huyo ameshindwa kuitumikia nafasi yake, ni vyema basi akaachia kiti.

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI STELA JOEL SIKU YA JUMAMOSI ALIFUNGA HARUSI NA YERIMO

PICHA ZIMEPIGWA NA RUMAFRICA +255 715851523

Mungu ni mwema na ni Mungu wa vitendo. Baada ya maombezi makali ya kila mtu kumtafuta yule ampendae, Mungu aliweza kujibu kilio cha Stella Joel na mpenzi wake Yerimo kwa kufanikisha ndoa yao iliyofungwa katika kanisa la Pentecostal Holiness Mission Light House Christian Center Ubungo na tafrija kufanyika katika ukumbi wa Mawasiliano Ubungo jijini Dar esa Salaam siku ya jumamosi

UNAWEZA KUWASILIANA NA STELLA JOEL KWA SIMU HII  +255 756 846166
AU +255715 049143


Stella Joel kutoka Bukoba (Mhaya)

Yerimo kutoka Iringa (Mhehe)

Bloga wenu Rulea Sanga aliyehusika ipasavyo kukuletea habari hizi na kupiga picha

MATUKIO KATIKA PICHA
SEHEMU YA KWANZA

WAKIANDAA SURA ZAO NA MAVAZI YAO



STELLA JOEL AKIELEKEA KANISANI AKITOKEA SALOON

Mwimbaji wa nyimbo za injili Madam Rutiu ndiye aliyekuwa dereva wa Bwana na Bibi Harusi
MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI NA MWANACHA WA CHAMUITA STELA JOEL LEO ANATARAJIA KUACHA UBACHALA BAADA YA MUNGU KUMPA CHAGUO LAKE .




Mwimbaji wstela joel kwenye picha ya kava la albamu yake aliyowashirikisha waimbaji mbalimbali akiwemo rose mhando

BAHATI BUKUKU AZINDUA KWA KISHINDO, MILIONI 20 ZATOLEWA NA LOWASSA


"Mtu yeyote anayeiombea amani anaipenda nchi hii. Leo natoa changamoto waimbaji wa nyimbo za injili wahubiri sana amani."

Ni kauli ya Waziri Mkuu aliyepita, ambaye pia ni mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa DVD ya album ya Dunia Haina Huruma, ya kwake Bahati Bukuku, ambayo imehudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba Jumapili hii.
Gospel Kitaa ilikuwepo kna kushuhudia ambapo, pamoja na kuwataka waimbaji wa nyimbo za injili wahubiri amani, Mh. Lowassa pamoja na marafiki zake walichangia kiasi cha shilingi Milioni 20.

Waimbaji kadhaa walimsindikiza Bahati kwenye uzinduzi huo ambao haukuwa na kiingilio, ambapo injili ilihubiriwa kwa njia ya uimbaji na watu kukata kiu na njaa ya kiroho waliyokuwa nayo, mkongwe Jennifer Mgendi,  Bonny Mwaitege, Neema Gasper, Rebecca Magaba (Ebenezer), Emmanuel Mgogo (Msikilize Mungu),  Majestic Singers wa EAGT Singers, Sarah Mvungi, ni sehemu tu ya waimbaji waliokuwepo.

Bahati Bukuku pia alitumia fursa hiyo kufungua Bukuku Entertainment ambayo iko Kariakoo mtaa wa Mhonda jijini Dar es Salaam, ambapo ni kampuni ya usambazaji itakayoshughulika na waimbaji chipukizi tu, na si waliokwisha toka tayari na kujulikana kwenye jamii.
Jennifer Mgendi akihudumu

MC wa shughuli, Silas Mbise akishuhudia mgeni rasmi anavyopungiwa
Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akiwaaga wananchi

MAKUMI ELFU WAJITOKEZA KUIOMBEA SYRIA AMANI

Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye maombi ya kufunga ya masaa manne kwa ajili ya taifa la Syria. ©AP
Makumi elfu ya watu walijitokeza siku ya Jumamosi katika kuitikia wito wa Papa Francis, ili kuombea amani taifa la Syria, ambalo limekuwA katika vita ya wenyewe kwa wenyewe, ambapo na kwa sasa Marekani wanataka kushambulia taifa hilo kutokana na kusadikika kutumia silaha za sumu huko Damascus mnamo Agosti 21.

Papa Francis alitumia wasaha huo kuomba kimya kimya, ambapo wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro walibeba bendera za Syria pamoja na vipeperushi vilivyosomeka, "Achaneni na Syria", mengine yakisomeka, "Msiishambulie Syria".

Maombi haya yaliyotangazwa na Papa tarehe mosi Septemba, yaliitikiwa na maaskofu maeneo mbalimbali kuanzia Italy, Cuba, na sehemu nyinginezo, ambapo pia huko Damascus, mufti mkuu alimshukuru Papa kwa jitihada zake na kuwaalika waislamu kufunga na kuomba kwa pamoja na wenzao walioko Roma.
Papa Francis akiendelea kusali kwenye mfungo huo wa wa kuiombea Syria. ©AP
"Wahindu, Wabuddha, na hata wasio na dini wote walijitokeza kufunga kwa ajili ya suala hilo. haya ni mafanikio makubwa sana". Anasema mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Anata.

DEREVA BODABODA IRINGA ATEKWA NA KUUAWA NA WATU WASIOJULIKANA

           
  IRINGA
Zikiwa  zimepita  siku  chache  toka  mmoja kati ya madereva boda boda mjini Iringa kutekwa kisha  kujeruhiwa vibaya kablaya kuporwa  pikipiki  yake ,unyama huo dhidi ya madereva  boda boda  umeendelea kutikisa mji wa Iringa baada Kijana mmoja mkazi wa kihodombi kutekwa kisha kuuwawa kinyama.


Tukio hilo la kinyama  limetokea  usiku  wa  leo baada ya kijana  huyo aliyetambulika kwa  jina la Edger Lalika kukutwa ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani .

Mashuhuda  wa  tukio hilo    wamesema  kuwa tukio la kuuwawa  kwa  dereva  boda  boda  huyo liletokea eneo la  Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa.

Hata  hivyo kijana  huyo anayekadiliwa  kuwa na umri wa miaka 25,ameuwa akiwa anafanya shughuli zake za bodaboda baada  ya  kukodiwa na mteja  wake huyo ambae aliamua  kuitoa roho yake kabla ya kumpokonya boda boda.

Kutokana na tukio  hilo  baadhi ya madereva bodaboda wamelaani vikali kitendo hicho na kuwataka madereva bodaboda wengine kuungana na kushirikiana na jeshi la polisi kufichua vitendo hivyo  vya utekaji na mauwaji  dhidi ya madereva  boda boda.
 

akithibitisha kutokea kwa tukio hilo  kamanda wa jeshi la polisi mkoani iringa bw ramadhan mungi amelaani vikali kutokea kwa mauaji hayo na kuiomba jamii kutoa ushirikiano wa kutosha ili kumbaini mhusika
 
    

DUNIA HAINA HURUMA YA BAHATI BUKUKU VIDEO KUZINDULIWA JPILI DAR KUSAMBAZWA KUANZIA JTATU NCHINI KOTE USIKOSE KUPATA NAKALA YAKO SASA

Mwimbaji wa nyimbo za injili Bahati bukuku akiwa katika huduma ya kumwimbia mungu m
m

HATIMAYE MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA KENYA EMMY KOSGEI AFUNGA NDOA NA MCHUNGAJI WA NIGERIA, ANGALIA PICHA ZOTE

Emmy na mumewe mwenye tai ya zambarau mchungaji Anselm Madubuko mara baada ya ndoa yao.
Hatimaye ile ndoa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wakazi wa nchini na Kenya na Nigeria pamoja na wapenzi wa mwanamuziki nyota wa gospel nchini Kenya imefanyika jana jijini Nairobi kwaku shuhudia mwanadada Emmy Kosgei akisema ndiyo kwa mchungaji Anselm Madubuko wa Nigeria katika viwanja vya bustani ya windsor Garden.

Awali kabla ya ndoa hiyo kumekuwepo maneno mengi kwanini mwimbaji huyo ameamua kuolewa na mchungaji huyo na wengine wakitoa na majibu kabisa kwamba amefuata pesa za mchungaji huyo bali wanapendana na kuwataka watu hao kuacha kufuatilia mambo yake na mahusiano na mumewe huyo, ambapo hakuacha kuweka bayana kwamba amekuwa akipendwa na kupewa matunzo kama malikia na mumewe huyo ambaye naye kwa upande wake amekaririwa akisema kwamba anampenda mwimbaji huyo pia uamuzi wa kumuoa alipewa ruhusa na mwanae mwenye miaka 25 aliyempata na mkewe Connie aliyefariki dunia mwaka jana, "hata kama ningesubiri kwa miaka zaidi bado haitasaidia kumsahau mke wangu, hata miaka 20 haitoshi bado, nimeamua kusahau na kusonga mbele ndio maana nimeamua kuoa sasa kipindi kifupi toka mke wangu afariki dunia" amesema mchungaji Anselm

Aidha mchungaji huyo ameongeza kuwa " nilioana na mke wangu na kuishi naye kwa miaka mingi lakini ghafla ameniacha pekee, mambo mengi yamepita, nimechagua kusikiliza akili na Mungu wangu ananiambia nini, amenichagulia Emmy inatosha kwasasa naangalia mbele zaidi kuongeza familia yangu kwakuwa na watoto na mke wangu mpya" alisema mchungaji Anselm akizungumza na jarida la Encomium.

Harusi ya kitamaduni ilifanyika siku ya alhamisi iliyopita wilayani Koibatek kijijini kwakina Emmy maeneo ya Kelelwa karibu na barabara kubwa ya Ravine, ambapo harusi kubwa inatarajiwa kufanyika huko Nigeria mapema wiki ijayo. Mungu abariki ndoa yao.






HATIMAYE KWAYA YA TANGAZENI KUTOKA DODOMA WAZINDUA ALBAMU YAO
mgeni rasmi akisema neno kabla ya kuzindua albamu

MASANJA MKANDAMIZAJI PAMOJA  SOLOMONI MKUBWA PICHANI AMBAO WALIWAVUTIA MAELFU YA WATU KUFIKA UWANJANI HAPO

WANAKWAYA PAMOJA NA WAGENI WAALIKWA WALIOFIKA KUWATIA MOYO KWA KUWACHANGIA

MGENI RASMI AKIONESHA CD AMBAYO ILIZINDULIWA JANA

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog