Dk Emmanuel Nchimbi 
Na Daniel Mjema na Sharon Sauwa Mwananchi

Posted  Decemba21  2013  saa 8:59 AM
Kwa ufupi
  • Serikali kuunda Tume ya Uchunguzi ya Kimahakama kuchunguza  waliohusika na unyama wakati wa operesheni

Dar es Salaam / Dodoma. Ripoti ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na Mazingira iliyowasilishwa jana asubuhi bungeni mjini Dodoma, imewang’oa madarakani mawaziri wanne ambao wizara zao zilishindwa kusimamia vizuri utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Kung’oka kwa mawaziri hao kulitangazwa bungeni jana usiku na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wao baada ya kuwasiliana naye kwa mashauriano akiwa nchini Marekani kwa matibabu.
Mawaziri waliong’olewa kutokana na ripoti ya kamati hiyo iliyoongezewa shinikizo na michango ya wabunge wengi ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa  Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.
Waziri wa  kwanza kutangaza kujiuzulu alikuwa ni Kagasheki huku uamuzi wa mawaziri watatu kujiuzulu ukitangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Kagasheki alitangaza kujivua wadhifa huo sa 2:09 usiku alipokuwa akichangia majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli ambaye ni Mbunge wa Kahama (CCM).
Katika maelezo yake Kagasheki alisema: “…Mimi ni mtu mzima nimesikia hisia nzito sana kwa waliyoyasema wabunge.  Rais Kikwete aliponiteua ilikuwa ni kwa furaha yake na operesheni hii, yaliyotokea yametokea hali ya wanyama huko si nzuri;
Mimi mwenyewe nimewasikia na nachukua fursa hii kuteremka ngazi hii ya uwaziri na nitachukua taratibu za kawaida kuijulisha sehemu inayohusika(Rais).
Baada ya Kagasheki kutangaza hatua hiyo, Spika aliwaita mawaziri Dk Nchimbi na Nahodha kuchangia hoja hiyo, hata hivyo hawakuwepo ndipo alipoitwa Dk Mathayo na kutoa maelezo yake.
Katika maelezo yake Dk Mathayo alisema kuwa ripoti hiyo haikumtendea haki kwani kamati ya Lembeli haikumwita kumhoji na kwamba hata ripoti nzima haikueleza kuhusika na kashfa hiyo. Hata hivyo akihitimisha hoja hiyo Lembeli alisema Dk Mathayo ameshindwa kusimamia mapendekezo tisa, yakiwemo matatizo    ya wafugaji aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete Januari 18, 2006 alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Akitoa maelezo ya kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Niliona nimtafute mkuu wa nchi (Rais Jakaya Kikwete), nilimpa picha yote ya kinachoendelea, alikubali ushauri wa Bunge; ..amekubali kuchukua ya uamuzi wa kutengua uteuzi wao(mawaziri).”
Akihitimisha mjadala huo wa ripoti ya kamati yake, Lembeli alisema: “...Katibu Mkuu na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii nao wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao na unyama uliotokea kwenye mpango wa Operesheni Tokomeza Ujangili. Rushwa iliyopo ndani ya wizara hiyo ni kubwa inakusanywa kwa kutumia simu, hivyo Serikali izichunguze simu zao kuanzia leo.

BREEEEKING....!! MAJAMBAZI WATATU WAUAWA NA POLISI KWA RISASI WILAYANI KAHAMA....!!

Mmoja wa Majambazi hao walioko katika hospitali ya wilaya ya Kahama

Jeshi la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limefanikiwa kuwaua watu  watatu  wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi ambao majina yao hayajafahamika waliokuwa wakipanga kuvamia mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama usiku wa kuamkia leo.
Miili ya Majamzazi hao watatu waliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Kahama
Kamanda wa polisi Mkoani humo Evarist Mangala amesema tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo katika kijiji Namba Tisa, baada ya kutokea majibizano ya risasi baina ya matuhumiwa hao na Askari wa Doria.
Mangala amesema watuhumiwa hao wanaokisiwa kuwa na umri kati ya miaka 25-30, wamekutwa wakipanga kufanya uhalifu katika mgodi huo, kabla ya kuanza  kurushiana risasi na Askari Polisi na hatimaye kuzidiwa nguvu na kuuawa.
Amesema  awali jeshi la polisi lilipata taarifa kuhusu uhalifu unaotaka kufanyika katika mgodi huo, na ndipo likafuatilia na kukuta watuhumiwa hao wakiwa na mabomu matatu ya kurusha kwa mkono  wakijiandaa kufanya uhalifu katika eneo hilo.
Mangala ameongeza kuwa mbali na kukutwa na mabomu hayo ya kivita pia wamekutwa na bunduki mbili za kivita aina ya SMG zenye namba za usajili 1972PX7482 na UC-17751998 pamoja na risasi 94 ndani ya magazine nne.
Kamanda Mangala amesema miili ya Majambazi hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
KIKOSI kizima cha Simba SC kinarejea leo Dar es Salaam kwa ndege kutoka Zanzibar walipokuwa wameweka kambi wiki yote hii kujiandaa na mchezo wa Nani Mtani Jembe kesho dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, Simba watakwenda kambini katika hoteli ya Spice, Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kesho.
Wanarejea leo; Simba SC wanatua kwa ndege leo kutoka kambini Zanzibar

Taarifa zinasema hakuna majeruhi na wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa kesho, unaoandaliwa na wadhamini wa timu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro.  
Simba na Yanga zitamenyana Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, unaoandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Katika mchezo huo, utakaochezeshwa na refa Ramadhan Ibada ‘Kibo’ kutoka Zanzibar, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles kutoka Dodoma, iwapo dakika 90 zitaisha kwa sare, sheria ya mikwaju ya penalti itatumika kuamua mshindi.
Viingilio vya mechi hiyo ni Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu Sh. 7,000, rangi ya chungwa Sh. 10,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000 wakati VIP A Sh. 40,000 na tiketi za mchezo huo utakaoanza Saa 10:00 jioni zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali.
Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Wachezaji wanaoruhusiwa kucheza mechi ya kesho ni wale waliosajiliwa ama kikosi cha kwanza au timu ya vijana pamoja na wapya ambao wameombewa usajili katika dirisha dogo.
Mara ya mwisho zilipokutana timu hizo Mei mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu, Simba SC ilitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kupata sare ya 3-3 Uwanja wa Taifa.
Watu kadhaa wamehofiwa kufariki kufuatia mlipuko uliotokea ndani ya gari moja dogo la abiria katika mtaa wa Pangani mjini Nairobi.
Duru zinaarifu kuwa karibu watu 4 huenda wamefriki katika shambulizi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu 15 waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Hata hivyo polisi hawajatangaza idadi rasmi ya watu waliojeruhiwa wala wale waliofariki.
Mlipuko huo umesemekana kutokea ndani ya matatu iliyokuwa inakwenda katika mtaa wa Eastleigh ambao una idadi kubwa ya wasomali wanaoishi huko.
Athari za mlipuko huo hazikuyasaza magari mengine manne yaliyokuwa karibu na matatu hiyo.
Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliokusanyika katika eneo la shambulizi kujionea yaliyokuwa yanajiri.


                 SAFARI YA MWISHO YA MANDELA  NI LEO

Mwili wa hayati Nelson Mandela umepelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa safari ya mwisho kabla ya kuzikwa siku ya Jumapili kijijini Qunu.
Idadi kubwa ya watu walifurika barabara angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa heshima zao za mwisho.
Mandela aliyefariki tarehe tano Disemba atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili,
Takriban watu 100,000 walitoa heshima zao za mwisho kwa Mandela mjini Pretoria siku ya Ijumaa kabla ya mamia ya wengine kukosa fursa hiyo pale walipokatazwa kumuona Mandela kutokana na ufupi wa mda.

Kijiji cha Qunu

Kijiji cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela.
Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.
Visima vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa. Lakini viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki zake walikesha wakichezea.
Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.
Alipokuwa na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe wao.
Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.
Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika pakubwa, ni kisafi kikubwa na kina dalili za maendeleo, wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu zake kuhusu nyumbani.
Na sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa pamoja na shule, alilemaji, umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo hili kutokana na makavazi aliyojengewa Mandela ambako atazikwa.

JAMBO LA KUFANYA USIKU WA KUAMKIA UHURU

Kuliko kujikunja ndani ya mashuka yako kutokana na mvua, ni vema ukajongea kwenye ukumbi wa huduma ya maombezi na ushauri, BCIC, ambapo kuna mkesha wa kusifu na kuabudu. Ni sehemu pekee ya kuondoa baridi la mwilini huku ukimpa nafasi Mungu kutenda mema anayokuwazia. Sote tukutane huko.

Mandela:Siku ya maombi Afrika Kusini

 
Watu wa umri wote wanamkumbuka Mandela
Wananchi wa Afrika Kusini wanashirki maombi ya kitaifa ya mwendazake Nelson Mandela.
Siku hii ya maombi imesemekana kua siku ya kumkumbuka Mandela na maisha yake.
Rais Jacob Zuma atahudhuria maombi hayo katika kanisa la Methodist mjini Johannesburg, wakishirikiana na viongozi wengine kutoka dini mbali mbali kwa maombi yatakayofanyika siku nzima leo.
Maombi maalum ya kitaifa yatafanyika siku ya Jumanne kabla ya kufanyika mazishi ya kitaifa Jumapili tarehe 15 Disemba.
Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikesha tangu Mandela kufariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Rais Jocob Zuma amewataka wananchi kwenda katika viwanja vya michezo , makanisa, kumbi mbali mbali na sehemu zingine zote za maombi, Leo Jumapili, kumkumbuka Mandela.
"Wakati huu tunapoomboleza kifo cha Mandela, tunapaswa kuwa pia tunaimba kusherehekea maisha yake kwa juhudi za mageuzi alizozifanya na kutuletea maisha mapya, tumuimbie Madiba,’’ alisema Rais Jacob Zuma.
Mrithi wa Mandela alipoondoka mamlakani, Thabo Mbeki, atahudhuria maombi katika kanisa ya Oxford Shul synagogue mjini Johannesburg mchana wa leo.
Viongozi wengine wakuu wa ANC, watahudhuria maombi katika maeneo mengine kote nchini humo,

WAZIRI MKUU AZINDUA JIMBO KUU LA KUSINI, AHIMIZA AMANI

IMG_99641WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania waendelee kuombea amani ya Taifa zima bila kujali tofauti zao za dini na kusisitiza kwamba kila mmoja ana wajibu wa kutunza amani iliyopo.
Ametoa wito huo jana jioni (Jumamosi, Desemba 7, 2013) wakati akizindua Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania (Southern Tanzania Union Mission) la Kanisa la Waadventista Wasabato kwenye sherehe zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waumini zaidi ya 13,000 wa Kanisa hilo walioshiriki uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema: “Mtu asiyejua vurugu hawezi kujua thamani ya amani… lakini lazima tujue madhara ya vurugu huwa ni makubwa kwa watoto, wanawake na wazee.
Aliwasihi viongozi wa kanisa hilo pamoja na waumini kuendelea kuliombea Taifa pamoja na Watanzania wote. “Mimi huwa nafarijika sana ninaposikia sehemu fulani kuna maombi kwa ajili ya Taifa, kwa hiyo ninawaomba Maaskofu na waumini msichoke kuliombea Taifa letu,” alisema.
Mbali na kuliombea Taifa pamoja na kuwaombea waumuni wake, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa kanisa kuendelea kushirikiana na Serikali kutafuta njia ya kuwasaidia waumini wake kukua kiuchumi. “Kanisa lina wajibu wa kuwasaidia wananchi kukua kiuchumi na mimi natambua waumini wa kanisa hili ni wakulima na wafugaji ama vyote viwili.”
Waziri Mkuu alisema moja ya kazi kubwa ya kanisa ni kusaidia waumini wake kukua kiroho na kimwili. Lakini kanisa pia linahitaji kuona maisha ya waumini yanakuwa bora zaidi. ”Tunategemea uchumi wa muumini mmoja mmoja kukua na hivyo uchumi wa kanisa, na uchumi wa Taifa kwa ujumla kukua,” alisongeza.
Alisema anataraji kwamba kupatikana kwa Jimbo Kuu la Kusini kutakuwa ni chachu ya kupata maendeleo zaidi ya kiuchumi katika Jimbo hilo ambalo linafaa sana kwa kilimo. “Pia, tunategemea kasi ya kupata waumini wapya itaongezeka kutokana na kugawanywa kwa Jimbo Kuu moja na kuwa Majimbo Makuu mawili, hivyo kusogeza huduma za kiroho na kiuchumi karibu zaidi na waumini,” alisema.
Waziri Mkuu alisema Jimbo Kuu la Kusini lililozinduliwa jana linajumuisha mikoa ambayo ni maarufu kwa shughuli za kiuchumi. “Imetajwa mikoa takriban 11 ya Tanzania Bara na Mitano ya Visiwani. Ipo mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Katavi, Lindi na Mbeya. Mikoa mingine ni Morogoro, Mtwara, Pwani, Rukwa na Ruvuma. Hakika ni eneo kubwa la kuongoza.”
“Kinachotakiwa ni kwa Kanisa kujipanga vizuri kwa kujiwekea mikakati ya maendeleo. Nawaombeni sana kuanzia sasa, tuwahimize waumini wetu hasa vijana wajikite pia katika kuanzisha miradi ya kilimo na ufugaji, ikiwemo kilimo cha mazao na ufugaji nyuki. Mkitumia fursa hizi zinazowazunguka katika maeneo yetu ya Jimbo hili, mnaweza kabisa kuleta ukombozi wa kiuchumi, hususan kwa vijana wetu,” alisisitiza.
Kanisa hilo lenye waumini wapatao milioni 17.2 duniani, lina makao yake makuu nchini Marekani. Hapa Tanzania lina waumini milioni tano na lilikuwa na jimbo kuu moja ambalo liligawanywa katika majimbo sita na makao yake makuu kwenye mabano kama ifuatavyo:- Kaskazini Mashariki (Same), Kusini mwa Ziwa Victoria (Mwanza), Mara (Musoma), Mashariki (Morogoro), Nyanda za Juu Kusini (Mbeya) na Magharibi (Kigoma).
Mapema, akisoma risala mbele ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini, Mchungaji James Machage alisema kutokana na kupanuka kwa kazi, kanisa hilo limeona vema hapa nchini kuwe na majimbo makuu mawili badala ya moja.
Alisema Jimbo Kuu la Kaskazini ambalo makao yake makuu yatakuwa Arusha litahusisha majimbo ya Mara, Kusini mwa Ziwa Victoria, Magharibi na Kaskazini Mashariki wakati Jimbo Kuu la Kusini litahusisha majimbo ya Mashariki na Nyanda za Juu Kusini na makao yake makuu yatakuwa jijini Dar es Salaam.

BALE APIGA HAT-TRICK REAL IKIUA 4-0 NA KUISOGELEA BARCA MGONGONI KABISA LA LIGA

WINGA Gareth Bale jana amefunga mabao matatu peke yake yaani hat-trick wakati Real Madrid ikiitandika Valladolid 4-0 Uwanja wa Bernabeu, Madrid na kuisogelea Barcelona kileleni mwa La Liga ikibaki inazidiwa pointi tatu.
Mchezaji huyo ghali wa dunia ameendelea kutekeleza vyema majukumu ya Cristiano Ronaldo ambaye ni majeruhi kwa sasa akiwa ametimiza mabao tisa katika mechi 13.Bale aliyefunga mabao hayo katika dakika za 33, 64 na 89 huku lingine liifungwa na Karim Benzema dakika ua 36, anakuwa mchezaji wa pili wa Uingereza kufunga hat-trick katika La Liga akimfuatia Gary Lineker mwaka 1987.
Real Madrid: Lopez, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Alonso, Modric, Di Maria, Isco, Bale na Benzema.
Real Valladolid: Marino, Alcatraz, Rueda, Valiente, Pena, Rubio, Sastre, Rossi, Larsson, Guerray na Bergdich.
La kwanza: Winga wa Real Madrid, Gareth Bale akishangilia bao lake la kwanza Uwanja wa Bernabeu jana
Stuck in: Bale vies for possession with Valladolid's forward Javi Guerra
Bale akimtoka mshambuliaji wa Valladolid, Javi Guerra
Tight at the top: Bale helped Real Madrid narrow the gap at the top of La Liga to three points
Bale ameisaidia Real Madrid kupunguza la pointi La Liga wanazozidiwa na vinara Barcelona hadi kubaki tatu
 
 
 
 
GGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGGG
 

ARSENAL HAIKAMATIKI BWANA WEEEE, YAWAFUMUA CARDIFF 3-0 BARAZANI KWAO...LUKAKU NI HATAREEE

London, England
ARSENAL imezidi kijichimbia kileleni mwa Ligi Kuu ya England, baada ya kuilaza mabao 3-0 Cardiff City, kwenye Uwanja wa Cardiff jioni hii.
Mabao ya Arsenal yamefungwa na Aaron Ramsey dakika ya 29 akimalizia pasi ya Mesut Ozil na 90 pasi ya Theo Walcott na Mathieu Flamini dakika ya 86 pasi ya Ozil tena. 
Ushindi huo, unaifanya Arsenal itemize pointi 31 baada ya kucheza mechi 13, ikiizidi Liverpool iliyo katika nafasi ya pili kwa pointi saba. 
Ramsey hakutaka kushangilia baada ya kuifunga timu yake ya zamani

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu England leo, 
Everton imeichapa 4-0 Stoke City Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, mabao ya Gerard Deulofeu dakika ya 45, pasi ya Gareth Barry, Seamus Coleman dakika ya 49 pasi ya Barry tena, Bryan Oviedo dakika ya 58, pasi ya Gerard Deulofeu na Romelu Lukaku dakika ya 79 pasi ya Oviedo.
Bao pekee la Gary Hooper dakika ya 30 limeipa Norwich ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace Uwanja wa Carrow Road, Norwich, Norfolk.
Lukaku akishangilia bao lake leo

West HamUnited imeifunga 3-0 Fulham Uwanja wa Boleyn Ground, London mabao ya Mohamed Diame dakika ya 47, Carlton Michael Cole Okirie dakika ya 82 na Joe Cole dakika ya 88.
Aston Villa imetoka sare ya bila kufungana na Sunderland Uwanja wa Villa Park na mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England, Newcastle United wataikaribisha West Bromwich saa 5:30 usiku. 



HHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHH

KENYA WAOTEA VIBONDE, WAWACHAPA 3-1 NYAYO

Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
KENYA imeshinda mechi ya kwanza Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuilaza Sudan Kusini mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi jioni hii katika mchezo wa Kundi A.
Ushindi huo unaifanya Harambee Stars ifikishe pointi nne baada ya awali kutoa sare ya bila kufungana na Ethiopia katika mchezo wa ufunguzi.
Joackins Atudo aliifungia Kenya bao la kwanza dakika ya 16 kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Sudan Kusini kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Wachezaji wa Kenya wakimpongeza mfungaji wa bao lao tatu, David Owino leo Nyayo

Sudan Kusini ilisawazisha dakika ya 26 kupitia kwa Nahodha wao, Richard Jistin aliyepiga shuti kali la mpira wa adhabu umbali wa mita 25 ambalo lilimshinda kipa Duncan Ochieng.
Jacob Keli aliifungia Harambee bao la pili dakika ya 29 akiunganisha krosi ya Allan Wanga kutoka upande wa kulia.
Atudo alikosa penalti dakika ya 70, baada ya kipa wa Sudan Kusini, Juma Jinaro kumuangusha Jacob Keli akiwa anakwenda kufunga. 
David Owino aliifungia Harambee bao la tatu dakika ya 78 baada ya kuwatoka mabeki wa Sudan Kusini.   
Matokeo haya yanamaanisha Kenya na Ethiopia sasa zinalingana kwa kila kitu, pointi nne kila mmoja, mabao matatu ya kufunga na bao moja la kufungwa, wakati Zanzibar sasa ni ya tatu kwa pointi zake tatu na Sudan Kusini inashika mkia.

CHAGUO LA GK VIDEO MPYA KUTOKA UINJILISTI SAYUNI



Ni Jumapili nyingine tena kupitia kipengele cha chaguo la GK, hii leo tuno kwaya ya Uinjilisti Sayuni kutoka usharika wa Kilutheri Kindondoni, wakiwa wanajiandaa kuachia toleo la tatu la video wametanguliza wimbo wa kuanzia uitwao "Dua na Maombezi" ambao unahimiza wacha Mungu kumlilia Mungu juu ya Taifa letu la Tanzania ili Mungu atuondolee majanga yote yanayotunyemelea na kuzidisha amani aliyotupa.

GK inakutakia utazamaji na usikilizaji mzuri wa wimbo huu ambao naweza kuwapa hongera kwaya hii kwakuchagua mazingira tofauti katika uchukuaji picha zao tofauti na video za waimbaji wengi wanaorudia maeneo ambayo waimbaji wenzao walisharekodia.


KWAYA YA KWETU PAZURI WAKO NCHINI ZAMBIA

Ambassadors of Christ wakiimba katika tamasha la pasaka jijini Mbeya mapema mwaka huu.

Kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka Kigali nchini Rwanda maarufu kama Kwetu Pazuri wapo nchini Zambia kwa ziara ya siku tano ukiwa ni mwaliko wa kanisa la Wasabato Libala la jijini Lusaka ambapo kwaya hiyo itashiriki katika maonyesho makubwa matatu nchini humo yanayotarajiwa kuanza siku ya jumamosi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo matamasha hayo ambayo yatakuwa na viingilio ili kusaidia ujenzi na huduma ya kanisa la Libala yatafanyika katika ukumbi wa Blessing centre kisha uwanja wa mpira wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola na kumalizia katika ukumbi wa New Government complex siku ya tarehe 2. Kwaya hiyo ambayo ilipata umaarufu sana nchini Tanzania mwaka 2011 kutokana na album yao ya Kwetu pazuri, imekuwa ikipata mialiko katika nchi mbalimbali za Afrika ambako wameonyesha kiu ya kuwaona waimbaji hao.

Ambapo kwa mwaka huu Ambassadors walishiriki tamasha la pasaka nchini Tanzania, tamasha ambalo hata hivyo liliwaweka katika wakati mgumu na makanisa ya kisabato nchini kutokana na kukubali kushiriki tamasha hilo, lakini pia walikuwa nchini Uganda pamoja na Goma nchini Kongo ambako wameshiriki katika matamasha mbalimbali ya kusaidia huduma za makanisa ya Kisabato.

Uwanja wa Levy Mwanawasa ulipo Ndola nchini Zambia,ambapo Ambassadors of Christ wataimba siku ya jumapili.

BINTI ATISHIWA KUCHINJWA NA KUSILIMISHWA KWA NGUVU NIGERIA

Hajja ©Reuters/Joe Brock
"Nilipolia walinipiga, na nilijaribu kuongea pia walinipiga. Waliniambi aninlazima nisilimu kuwa Muislamu ili wasiniue". Hajja anasimulia, binti mwenye umri wa miaka 19, ambaye amepona kwenye mikono ya kundi la kigaidi lenye uhusiano na al-Qaeda, Boko Haram nchini Nigeria.
Milima ya Gwoza ndiko ambako kijiji cha binti Hajja kinapatikana, ambapo kuna siku alikuwa kwenye shughuli za kawaida alipotekwa na kundi hilo, na kulazimishwa kuzunguka nalo kwa miezi mitatu huku akiwapikia na kuwafulia nguo zao.
Katika ushuhuda ambao ameueleza kwa shirika la habari la Reuters, Hajjaa anasema kuwa. licha ya kwamba hakubakwa, ila alikuwa akiteswa vibaya sana na kulazimishwa kuachana na Ukristo, ili apate kuishi, jambo ambalo alikuwa akipingana nao kwa nguvu, hatua ambayo ilimfanya mmojawapo wa watekaji kumbembeleza ili asiuawe kwa kuchinjwa, ambapo siku moja kabla tu hajauwawa ilimbidi akubaliane nao na kuapishwa - na kisha kulazimishwa kusoma Quran.
Kati ya mayeso ambayo ameyapata, Hajja anaeleza kuwa alikuwa ni mtu wa kufua na kupika, na kama hakuwa akifanya hizo shughuli basi alilazimishwa kubeba silaha zao, na kisha siku moja hatosahau ni pale ambapo walimfanya chambo/mateka mbele ya wanajeshi wa serikali ili wasidhurike wala kukamatwa.

CHRISTINA SHUSHO ALIVYOWEKA MAMBO SAWA CCC JUMAPILI

Siku ya jumapili tarehe 24 November, 2013 katika Ukumbi wa Kanisa la CCC Upanga Mwanamuziki wa injili aliyejijengea jina katika ukanda wa Afrika Mashariki na Mwanamuziki anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi kuliko wanamuziki wengine wa injili inchini Tanzania Christina Shusho amefanya Live Recording ya aina yake katika Ukumbi huo.

Live Recording hiyo ilianza majira ya saa 12 ilikuwa nikiwango cha kimataifa na Iliandaliwa kwa ustadi Mkubwa kulinganisha na matamasha mengine ya Injili hapa Tanzania. Christina Shusho katika Nyimbo zake hizo pia alifanya Collabe na wanamuziki wengine wa injili hapa Tanzania kama Upendo Kilahiro pamoja na Joshua Mlelwa. Mgeni rasmi katika Tamasha hili alikuwa Mhe. Bernad Membe waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Waziri hiyo akizungumza katika tamasha hilo alisema ipo haja ya vijana wa kitanzania kumcha Mungu ili kuweza kuja kuwa viongozi wa nyanja mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa hapa Tanzania.

Christina Shusho akiwa sawa stejini.
Christina na Upendo Kilahiro wakiimba pamoja Thamani ya wokovu wangu.
Waitikiaji wa Christina Shusho wakienda sawa.
Mgeni wa heshima mheshimiwa Benard Membe akizungumza na waumini waliofika tamashani.
Christina Shusho akienda sawa na kundi la The Voice.
MC no 2 watukio, unclejimmy temu akienda sawa.
Mpiga Saxaphone nambari One Nchini Uganda Isaiah akihudumu.
Shetani aliipata, maana thamani ya wokovu ilikuwa level nyingine.

Vijana wakisebeneka wakati wa tamasha.
Samuel Yona, aliyeandaa na kuongoza muziki wa mwanamama Christina Shusho.
Upendo Kilahiro na Christina Shusho.
Kamati iliyoandaa tamasha hilo.

ANGALIA PICHA ZA SHANGILIENI KWAYA WAKIWA AFRIKA YA KUSINI KIHUDUMA

Kwaya ya Tumaini Shangilieni toka St.James Kaloleni Arusha inatarajiwa kuwasili siku ya leo ikitokea nchini Afrika ya kusini ambako ilikwenda katika kanisa la Anglican kitongoji cha Tembisa jijini Johannesburg kihuduma. Kwaya hiyo ambayo iliondoka na ndege ya Fastjet siku ya ijumaa, imefanikiwa kufikia lengo lililowapeleka nchini Afrika ya kusini kumuhubiri Kristo.

Wakati huohuo taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba kwaya hii inatarajiwa kuwepo usharika wa Kijitonyama Lutheran jijini Dar es salaam siku ya tarehe 8 mwezi ujao katika kuwasindikiza kwaya ya uinjilisti Kijitonyama ambayo itakuwa ikisherehekea miaka 25 ya kwaya yao tangu ilipoanzishwa.


Taarifa kamili na picha nyingine zitawajia kupitia hapa hapa GK. Kwa leo pata japo kwa kifupi
Mawinguni mwe!
Muonekano wa jiji la Johannesburg kutokea juu karibu na uwanja wa ndege wa OR Tambo.
Mwenyekiti wa Tumaini Dkt. Emanuel Mtangoo na wanakwaya wengine wakizungumza na mwenyeji wao mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa OR Tambo.
Safari ya kuelekea kanisani.
Usharikani Tembisa.
Waimbaji wa Tumaini wakiwa kanisani siku ya jumapili.

YAYA TOURE AITISHIA AMANI CHELSEA, AWAAMBIA REKODI YAO IKO HATARINI

KIUNGO Yaya Toure anaamini Manchester City inaweza kuvunja rekodi ya mabao ya msimu katika Ligi Kuu England msimu huu.
Kiungo huyo wa nguvu amempa jeuri kocha Manuel Pellegrini juu ya uwezo wa kushambulia unaoleta matumaini ya taji kwa kusema rekodi ya Chelsea iko hatarini.
Kocha Carlo Ancelotti akiwa na kikosi mariadi msimu huu 2009-10 aliiwezesha Chelsea kufunga mabao 103 na kutwaa taji misimu minne iliyopita.
Jitu la nguvu: Yaya Toure (kushoto, akipambana na Paulinho wa Spurs, amesema City inaweza kuvunja rekodi ya mabao
Six of the best: Sergio Aguero netted twice in City's rout of Tottenham on Sunday
Mabao sita: Sergio Aguero alifunga mabao mawili City ikiifumua Tottenham Jumapili
Put your hands up: Chelsea netted an incredible 103 goals on their way to winning the Premier League in 2010
Inua mikono juu: Chelsea ilifunga mabao 103 wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 2010

Na baada ya timu ya Pellegrini kufikisha mabao 34 wakiifunga sita Spurs Jumapili, Toure amesema lengo ni kuvunja rekodi hiyo.
Alipoulizwa kwamba inaezekana kuipiku rekodi ya Chelsea, alijibu: "Natumaini hivyo — tuna washambuliaji. Watu wawili mbele (Alvaro Negredo na Sergio Aguero) hawa watu huwezi kuamini. Wanajiamini sana.
"Lakini si kwa sababu ya wachezaji hao wawili tu. Ni timu nzima. Tunashambulia sana na washambuliaji wote wanafurahia hii. Hata (Edin) Dzeko na (Stevan) Jovetic.
"Timu inaelekeza nguvu zake katika kushambulia. Ni babu kubwa. Na unaposhinda kama tulivyofanya kwa Tottenham ni nzuri. Ni washindani wa kweli katika mbio za taji la Ligi Kuu mwaka huu,".
Out of action: But even Edin Dzeko is enjoying life at goalscoring City at the moment, claims Toure
Nje ya Uwanja: Lakini hata Edin Dzeko anafurahia maisha namna ambavyo City inafunga mabao, amesema Toure

MAVETERANI KENYA NA BARA KUKUMBUSHIA CHALLENGE YA ENZI HIZO, HUO MUZIKI WA HARAMBEE USIUPIMIE, KUNA MAHMOUD ABBAS, PETER DAWO, J J MASIGA, JUA CALI NA KADENGE, STARS…

Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
WACHEZAJI wa zamani wa Kenya ‘Wazee wa Kazi’ wametaja kiksi cha nguvu ambacho kinamenyana na wakongwe wenzao wa Bara kutia nakshi michuano ya mwaka huu ya Challenge.
Kikosi hicho chini ya kocha George Sunguti kina wachezaji 30 ambao waliwika Harambee Stars enzi zao.
Wazee wa Kazi; Wachezaji wa zamani wa Harambee Stars

Kikosi hicho ni; Mohammed Abbas (kipa), John Busolo (kipa), Josphat Murila (beki), George Sunguti (mshambuliaji), Austin Oduor (mshambuliaji), Elly Adero, Sammy Pamzo Omollo (mabeki), Allan Thigo (kiungo), Joe Kadenge (mshambuliaji), Tobias Jua Kali Ochola (beki), Ben Oloo, George Onyango, Wycliffe Anyangu (mabeki), Paul Ochieng’ (beki), Peter Dawo (mshambuliaji), Ben Musuku, Aggrey Lukoye, J.J Masiga (washambuliaji), Paul Onyiera (kiungo), Mike Amwayi, Douglas Matual, Joe Birgen, James Siang’a (makipa), Abdul Baraza, Ricky Solomon, John Bobby Ogola, James Nandwa (washambuliaji), Ambrose Golden Boy Ayoyi, John Nyawaya na David Ochieng’.
Tanzania Bara bado haijataja kikosi chake kitakachokuja Nairobi na hadi jana hakukuwa na taarifa za hata kuanza mazoezi.

BARA KUJIFUA STIMA PAMOJA NA SUDAN, ETHIOPIA LEO

Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
TIMU zinazoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge ambayo mwaka inafanyika hapa Nairobi, Kenya ikidhaminiwa na Serikali, zitafanya mazoezi katika viwanja vijnne tofauti leo.    
Viwanja hivyo ni Stima Club, Chuo Kikuu cha Strathmore, Uwanja wa City Stadium Ktuo cha Kimataifa cha Michezo cha Moi (MISC), Kasarani.
Uchovu umeisha; Kocha wa Bara, Kim Poulsen leo atakiongoza kikosi chake mazoezini kwa mara ya kwanza Nairobi, baada ya kuwasili jana. Chini, kikosi cha Stars kikiwasili Nairobi jana usiku.

MISC, Kasarani umetengwa maalum kwa ajili ya wenyeji, Kenya, Harambee Stars, wakati Tanzania Bara, Sudan na Ethiopia watafanya pamoja kwenye Uwanja wa Stima.
Rwanda, Sudan Kusini na Burundi watatumia viwanja viwili vya Strathmore, huku Somalia, Zanzibar na Eritrea wakitumia mwingine na mabingwa watezi Uganda na Zambia watatumia Uwanja wa City.

900 waliuawa katika vita dhidi ya M23

Jeshi la congo linasema kuwa mapigano na waasi wa M23 yamesababisha vifo vya zaidi ya wapiganaji 900 tangu mwezi Mei.
Wanajeshi wa DRC
Msemaji wa jeshi Genarali Jean-lucien Bahuma alisema kuwa takriban wanajeshi 200 na zaidi ya wapiganaji 700 waliuawa katika mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Wanajeshi watatu wa amani wa UN pia waliuawa kwenye makabiliano hayo.
Pia wapiganaji 72 wa Rwanda na wapiganaji 28 wa Uganda waliuawa.
Mwanzoni mwa mwezi huu, waasi wa M23 walitolewa na jeshi la serikali iliyoungwa mkono na kikosi cha wanajeshi wapatao 5000 wa Umoja wa Mataifa lakini serikali ya Congo na waasi walikosa kuelewana kuhusu mpango wa baadae wa amani.
Waasi wa M23 walisitisha vita na kujisalimisha baada ya jeshi la DRC kwa ushirikiano na wanajeshi wa UN kupigwa vita vikali na kuwaondosha katika maeneo waliyokuwa wameyateka.
Maelfu ya wakaazi wa Mashariki mwa DRC walilazimia kukimbilia nchi jirani ya Uganda kutafuta hifadhi wakati kundi hilo lilipokuwa linaendesha uasi wao na hata kuuteka mji wa Goma kwa muda.
Kudni la M23 lilifanya vitendo vya kikatili dhidi ya watu wa Mashariki mwa DRC ikiwemo ubakaji na kuwatumia watoto kama wapiganaji.

BALOTELLI AZUA LINGINE ITALI BAADA YA KUTWEET "THIS IS THE END"

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amewachangasha tena mashabiki wake leo baada ya kutweet 'this is the end' (huu ni mwisho) saa kadhaa baada ya kukosa penalti AC Milan ikilazimishwa sare ya 1-1 na Genoa.
Mshambuliaji huyo hatari, alitweet ujumbe huo Kiingerezamajira ya saa 11 Alfajiri kwa sa za kwao katika akaunti yake ya @finallymario.
Pamoja na hayo, saa sita baadaye akatuma ujumbe mwingine wa tweet Kitaliano, uliosomeka: ‘Forza Milan comunque e sempre.’ ambao Kiingereza ni 'Go on Milan, no matter how and forever'.
Mwisho wa barabara? Mario Balotelli alikosa penalti timu yake AC Milan inayosuasua ikilazimishwa sare ya 1-1 na Genoa
What does he mean? Balotelli tweets after AC Milan's draw with Genoa
Anamaanisha nini? Balotelli ametweet baada ya sare ya AC Milan na Genoa
Turn around? Balotelli later tweeted his support for Milan a few hours later
Spot of bother: Balotelli misses a penalty against Genoa
Balotelli akipiga penalti aliyokosa
No joy: Balotelli has missed two penalties this season
Hakuna furaha: Balotelli amekosa penalti mbili msimu huu
Down and out: Mario Balotelli looks dejected as AC Milan fail to win again
Down and out: Mario Balotelli looks dejected as AC Milan fail to win again

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog