Home » »

KIKOSI kizima cha Simba SC kinarejea leo Dar es Salaam kwa ndege kutoka Zanzibar walipokuwa wameweka kambi wiki yote hii kujiandaa na mchezo wa Nani Mtani Jembe kesho dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, Simba watakwenda kambini katika hoteli ya Spice, Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kesho.
Wanarejea leo; Simba SC wanatua kwa ndege leo kutoka kambini Zanzibar

Taarifa zinasema hakuna majeruhi na wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa kesho, unaoandaliwa na wadhamini wa timu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro.  
Simba na Yanga zitamenyana Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, unaoandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Katika mchezo huo, utakaochezeshwa na refa Ramadhan Ibada ‘Kibo’ kutoka Zanzibar, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles kutoka Dodoma, iwapo dakika 90 zitaisha kwa sare, sheria ya mikwaju ya penalti itatumika kuamua mshindi.
Viingilio vya mechi hiyo ni Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu Sh. 7,000, rangi ya chungwa Sh. 10,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000 wakati VIP A Sh. 40,000 na tiketi za mchezo huo utakaoanza Saa 10:00 jioni zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali.
Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Wachezaji wanaoruhusiwa kucheza mechi ya kesho ni wale waliosajiliwa ama kikosi cha kwanza au timu ya vijana pamoja na wapya ambao wameombewa usajili katika dirisha dogo.
Mara ya mwisho zilipokutana timu hizo Mei mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu, Simba SC ilitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kupata sare ya 3-3 Uwanja wa Taifa.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog