BREEEEKING....!! MAJAMBAZI WATATU WAUAWA NA POLISI KWA RISASI WILAYANI KAHAMA....!!
Mmoja wa Majambazi hao walioko katika hospitali ya wilaya ya Kahama |
Jeshi la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limefanikiwa
kuwaua watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi ambao majina yao
hayajafahamika waliokuwa wakipanga kuvamia mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu
uliopo wilayani Kahama usiku wa kuamkia leo.
Miili ya Majamzazi hao watatu waliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Kahama |
Kamanda wa polisi Mkoani humo Evarist Mangala amesema tukio hilo
limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo katika kijiji Namba Tisa, baada
ya kutokea majibizano ya risasi baina ya matuhumiwa hao na Askari wa Doria.
Mangala amesema watuhumiwa hao wanaokisiwa kuwa na umri kati ya miaka
25-30, wamekutwa wakipanga kufanya uhalifu katika mgodi huo, kabla ya
kuanza kurushiana risasi na Askari Polisi
na hatimaye kuzidiwa nguvu na kuuawa.
Amesema awali jeshi la polisi lilipata taarifa kuhusu
uhalifu unaotaka kufanyika katika mgodi huo, na ndipo likafuatilia na kukuta
watuhumiwa hao wakiwa na mabomu matatu ya kurusha kwa mkono wakijiandaa
kufanya uhalifu katika eneo hilo.
Mangala ameongeza kuwa mbali na kukutwa na mabomu hayo ya kivita
pia wamekutwa na bunduki mbili za kivita aina ya SMG zenye namba za usajili
1972PX7482 na UC-17751998 pamoja na risasi 94 ndani ya magazine nne.
Kamanda Mangala amesema miili ya Majambazi hao imehifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
0 comments:
Post a Comment