Wateja wa Airtel kununua Tiketi za Ndege za Precicsion Air kupitia huduma ya Airtel Money
Wateja wa Airtel kununua Tiketi za Ndege za Precicsion Air kupitia huduma ya Airtel Money
· Wateja wa Airtel wawezeshwa kulipia tiketi zao za ndege kwa njia rahisi na haraka zaidi
Dar es Salaam Jumatano , Mai 7, 2014, kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imeanzisha ushirikiano na Precision Airtel
utakaowawezesha wateja wake nchi nzima kununua tiketi za ndege kupitia
huduma ya Airtel Money
Ushirikiano
huu utawapatia wateja wa Precision Air urahisi katika kupanga safari
zao na kuwawezesha kununua ticket zao wakati wowote bila usumbufu
kupitia huduma ya Airtel Money.
Akionge wakati wa uzinduzi Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema “ushirikiano
huu utawapatia wateja wetu wa Airtel njia mbadala, rahisi naya uhakika
ya kulipia safari zao za ndani na za nje huku ikiwapatia watanzania na
wateja wetu uzoefu tofauti wa kufanya malipo ya tiketi zao za ndege
kupitia simu zao za kiganjani.
Kwa kupitia huduma hii mpya sasa
wateja wetu wataweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege mahali popote
kwa usalama na haraka zaidi kupitia huduma ya Airtel Money. ”
“Tutaendelea
kuthibitisha dhamira yetu ya kutoa bidhaa na huduma za kibunifu huku
tukiwahakikishia wateja wetu huduma bora kupitia huduma ya Airtel Money
na nyinginezo wakati wote”. Aliongeza Matinde
Akiongelea
kuhusu ushirikiano huo Afisa Masoko wa Precision Air Bwana Hillary
Mremi alisema “
ushirikiano huu umekuwa kwa wakati muafaka wakati
Precision Air imejipanga kuboresha huduma zetu na kuwapatia wateja
wetu uzoefu tofauti katika huduma za ndege huku tukihakikisha wateja
wanafurahia huduma zetu zinazoenda zaidi ya matarajio yao.
Wateja
wetu sasa wanaweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege kwa kupitia
huduma ya Airtel Money . kupitia simu zao za mkononi wateja wetu
wanaweza kupiga call center au kutembelea tovuti yetu kufanya booking ya
safari zao na kulipia kupitia Airtel Money na kisha kupokea tiketi yako
kupitia simu yako ya mkononi” aliongeza Mremi
Akiongea
kuhusu namna ya kupata huduma hiyo Meneja uendeshaji wa Airtel Money
Asupya Naligingwa alisema” huduma hii ni rahisi kutumia , mteja
anachotakiwa kufanya ni kupiga simu na kufanya booking ya safari au
kufanya booking kupitia tovuti ya Precision Air ambapo mteja atapewa
namba ambayo itatumika kama reference wakati wa malipo.
Kununua tiketi kupitia Airtel Money wateja wanatakiwa kufanya yafuatayo
Piga *150*60#
|
Chagua namba 5 (Lipia Bili)
|
Chagua namba 8 (NYINGINEZO)
|
Andika jina la biashara
|
PW
|
Ingiza Kiasi cha pesa
|
Kumbukumbu rejea
|
(namba ya booking)
|
Ingiza neno la siri kulipa PW, Tsh xxxxx, kumbukumbu rejea namba xxxxxx
|
Baada ya kufanya hayo utapokea ujumbe wenye uthibitisho wa malipo na tiketi yake ya ndege “aliongeza Nalingingwa
Huduma
ya Airtel Money ni huduma inayowawezesha wateja wa Airtel Nchi nzima
kufanya malipo na miamala ya pesa kupitia pesa simu ya mkononi . kwa
kupitia huduma ya Airtel money wateja wanaweza kulipia ankra kama vile
DAWASCO, LUKU, USA visa, DSTV, kulipia mikopo , kununua muda wa
maongezi, kununua vifurushi vya yatosha na kutuma na kupokea pesa kutoka
kwa marafiki na familia na huduma nyingine nyingi.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment