ISRAEL HOUGHTON KUIMBA NCHINI UGANDA MWEZI UJAO, HAKUNA KIINGILIO
![]() |
Watoto Children Choir namba 66 wakiimba kanisani kwao kabla ya kuelekea nchini Australia kwa ziara wiki mbili zilizopita. |
humo.
Israel na kundi lake la New breed wanatarajiwa kuimba siku ya alhamis tarehe 5 katika kanisa la Watoto west tukio ambalo halitakuwa na kiingilio lililopewa jina la 'Watoto Big Party'. Hii itakuwa si mara ya kwanza kwa mwimbaji huyo kuimba jukwaa moja na Watoto children choir ambao amekuwa akikutana nao sehemu mbalimbali. Mwimbaji huyo atakuwa nchini Uganda wiki moja baada ya kumaliza tamasha lake kubwa la uimbaji litakalofanyika jijini London nchini Uingereza tarehe 27 mwezi wa tano akiwa na kundi lake kamili.
Haya kwa wale wapenzi wa mwanamuziki huyo, ni kujipanga nauli ya kwenda na kurudi na sehemu ya kufikia bila kusahau chakula, onyesho halitakuwa na kiingilio.
0 comments:
Post a Comment