WAPENDA MIUJIZA, HIKI NDICHO KINACHOWAPATA
Mtume Lesego Daniel. |
GK imeamua kuandika tena hii leo kuhusiana na huduma hii, mara baada ya
kuona video fupi iliyorekodiwa na mchungaji Thami Dlalisa wakati
akiangalia kipindi kwenye runinga kilichokuwa kikionyesha huduma ya
mtumishi Lesego akiwa amemrukia kwa juu kwa kumkanyaga kwa nguvu
mwanadada aliyekuwa amelala chini kwa ajili ya maombi kitendo ambacho
pia kilisikika sauti ya waumini wake ikionyesha mstuko namna dada huyo
atakavyohimili uzito wa mchungaji huyo.
Katika maelezo yake mchungaji Dlalisa ambaye alirekodi video fupi ambayo
ipo chini, amewataka marafiki zake wa facebook kuangalia video
aliyorekodi yenye dakika 12 na kuwataka maoni yao wanafikiriaje
watakachokiona, mchungaji anamrukia muumini wake wakati wengine
wamesimama kama mazombi huku wengine wamekaa kama wanatazama igizo.
Ambapo watu walioweka maoni yao walionekana kuponda sana huduma hiyo
huku wengine pia wakisema hata waumini nao pia wanachangia kwa kupenda
kufuata miujiza.
0 comments:
Post a Comment