BREAKING NEWS:MUME AUA MTOTO NA KUMCHOMA CHOMA MKE KWA KISU IRINGA
Bi Janeth akiongea na mwandishi wa habari |
Mwanaume mmoja mkazi wa ilolo mpya
pawaga aliyetambulika kwa jina la Isaya Samamba,amejikuta hatiani baada
ya kumuua kwa kumchomachoma mtoto wake Vanesa wa miezi kumi kwa kisu na
kumjeruhi mama wa mtoto huyo anayetambulika kwa jina la Janeth
malenda,akiongea na mtandao huu Bi.Janeth amesema kuwa siku hiyo alikuwa
ameenda katika mkutano wa Injili na aliporudi nyumbani giza lilikuwa
tayari limeingia,walipokuwa chumbani yeye,mtoto pamoja na mumewe
alishangaa kuona ghafla mumewe akimchoma kwa kisu ndipo alipoamua
kukimbia nnje na kupiga kelele ili wasamalia wema waje wamsaidie baada
ya watu kufika walikuta mtuhumiwa amekimbia huku wakishuhudia mwili wa
mtoto ukiwa umejaa damu na utumbo ukiwa nnje.
Watu waliofika walichukua hatua na
kutoa taarifa polisi na ndipo polisi walianza jitihada za kumsaka
mtuhumiwa na alikamatwa usiku wa manane katika nyumba aliyofanyia mauaji
akitaka kuchukua baadhi ya vitu ili atoroke na kufikishwa katika kituo
kikuu cha polisi Iringa.
Mtandao huu unampa pole Bi.Janeth ambaye kwa sasa amelazwa hospitali ya mkoa iringa kwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment