NYOTA WA MUZIKI WA INJILI UGANDA AFA AKIOGELEA TANZANIA
Marehemu Mark Elvis enzi za uhai wake. |
Marehemu ni mmoja kati ya watoto yatima waliolelewa na kanisa maarufu la
Watoto nchini Uganda baada ya wazazi wake kufariki akiwa na miaka sita
tu, ambapo alichukuliwa na kanisa la Watoto ambao walimpeleka shule na
kuhitimu elimu ya juu ya sekondari na ndoto yake toka wakati huo ilikuwa
kuingia kwenye muziki, ndoto ambayo ilitimia kama alivyotaka na
kujikuta akipata umaarufu baada ya nyimbo zake kushika nafasi za juu
katika radio mbalimbali nchini Uganda.
Kaka wa marehemu aitwaye Ivan ambaye alikuwa ni mmoja kati ya watoto wa
kwanza wakati huduma ya Watoto inaanza mwaka 1994 naye alifariki dunia
miaka michache iliyopita. Kutoka na hayo yote Elvis aliamua kumwachia
Mungu maisha yake na kila kitu alichonacho hasa katika kumwimbia yeye
kutokana na tumaini na upendo alioupata kutoka kwa Yesu, kuliko
kufikiria machungu anayopitia.
Katika moja ya mashairi ya nyimbo zake Elvis aliimba"If I were to change
anything about my life, I wouldn't change a thing. It's what I
experienced in the past that moulded me into who I am today," he always
remarked in interviews. "It's been God's grace, love and care that has
carried me through."
Mpaka umauti unamkuta kijana huyo ana album tatu ya kwanza inayoitwa
"Your love"aliitoa mwaka 2009, Church boy(2011) na hivi karibuni
aliachia single zake katika album mpya ijayo moja ya nyimbo hizo ni
Topowa game unaopendwa kwenye vituo vya radio na televisheni nchini
kwake.Kati ya mafanikio aliyopata katika muziki wa injili tangu aingie rasmi mwaka 2006 ni pamoja na tuzo za Uganda Olive Awards, pamoja na kutajwa kwenye tuzo za Grooves za Kenya kama mwimbaji bora kutoka Uganda. Lakini pia ameimba kama mwimbaji mtangulizi katika matamasha ya waimbaji wakubwa wa gospel duniani waliofika Kampala Uganda kama Kirk Franklin, Papa San,Sean Slaughter na Cece Winans.
0 comments:
Post a Comment