Upepo mkali uliombatana na mvua kiasi umeezua paa za nyumba nne na kuwaacha wakazi zaidi 15 wakiwa hawajui jambo la kufanya mara baada ya kukumbwa na kadhia hiyo.
Familia
hizo ambazo zipo Mtaa wa Nduli, Kata ya Nduli, Manispaa ya Iringa zimekumbwa na
kadhia hiyo hii leo majira ya saa kumi na moja kasoro jioni ambapo hata hivyo
hakuna mtu alipepatwa na dhoruba ya kupata majeraha ama kifo baada ya janga
hilo.
Akizungumzia
tukio hilo mara baada ya kufika na kujionea hali halisi, Mkuu wa Wilaya ya
Iringa, Ndg Richard Kasesela ameuambia mtandao wa Wazo Huru kuwa, alipata
taarifa hizo majira ya jioni ambapo aliamua kufika ili kujua ni kwa kiasi gani
wakazi hao wamekumbwa na tatizo hilo.
Kasesela
amesema ni tukio ambalo limemsikitisha kwa kiasi kikubwa kwani Mkoa huo bado
upo katika maskitiko makubwa mara baada ya wakazi takribani 391 kutoka karibu
kaya 99 kukumbwa na mafuriko katika Kijiji cha Kisinga, tarafa ya Pawaga yaliyosababisha
serikali kutumia Helkopta kuwaokoa.
Kasesela
amesema kuwa kesho asubuhi atatuma wataalamu kwa ajili ya kufanya tathimi ya
kile kilichotokea ili kuona ni kwa namna gani serikali inaweza kusaidia wakazi
hao ambao kwa sasa wamepatiwa hifadhi na majirani.
Kasesela
amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani humo zimekuwa na changamoto
kubwa kwa wakazi wa maeneo mbalimbali kutokana nakukosa makazi kwa sababu ya adha
kubwa ambazo wamekuwa wakizipata, ambapo amesema serikali itajitahidi kukabiliana
na kadhia yoyote itakayojitokeza ili kuwasaidia wananchi wanaokumbwa na
matatizo yoyote.
Hata
hivyo mkoa wa Iringa umeingia kwenye kadhia hii wakati zimepita siku chache tu
mara baada ya vibanda 51 vya wakulima wa mpunga kusombwa na
maji katika vitongoji vya Mboliboli na Kimande.
0 comments:
Post a Comment