DK SLAA KUZINDUA KESHO KAMPENI ZA CHADEMA UCHAGUZI MDOGO KALENGA, CCM KUANZA JUMAPILI

[Image]
Dk Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa kesho Jumamosi atazindua kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wilayani Iringa katika kijiji cha Kalenga.
Kwa upande wao Chama cha Mapinduzi (CCM) kitanzaa kampeni zake keshokutwa Jumapili katika kijiji cha Mseke wakati kikiendelea na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni hizo.
Uchaguzi huo unakishirikisha chama kingine cha Chausta kilichomsimamisha Richard Minja kupeperusa bendera yake.
CCM kwa upande wao imemsimamisha, Godfrey Mgimwa, huku Chadema ikiwa imemsimamisha Grace Tendega.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka, jimbo la Kalenga lina jumla wapiga kura 85,051.
Akizungumza Katibu wa Chadema Iringa Vijijini, Felix Nyondo alisema Dk Slaa atawasilia mjini Iringa kwa gari mapema kesho katika mapokezi yatakayohusisha msafara mkubwa wa magari na pikipiki katika eneo la Ndiuka mjini hapa.
Mbali na Dk Slaa, Nyondo alisema wengine watakaokuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni hizo ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Leman na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Alisema baada ya uzinduzi huo, Chadema itaendelea na kampeni za kila siku na kwa mujibu wa ratiba yao, kila siku watakuwa wakifanya mikutano 39.
Nyondo alisema katika kampeni hizo Chadema itatumia helkopta (chopa) tatu, magari 56 na pikipiki 80.
Alisema vyombo hivyo vya usafiri vitagawanywa katika kata zote 13 za jimbo hilo ili kufanikisha shughuli nzima ya kampeni zao.
Kaimu Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassana Mtenga alisema CCM kwa upande wake inaendelea na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni zake.

STENDI MPYA IGUMBILO HATIHATI KUJENGWA IGUMBILO, WAZIRI APIGA STOP HARAKATI ZA UJENZI WAKE

[Image]
Dk Mahenge akiwa na viongozi wa mkoa na Manispaa ya Iringa katika eneo linalolalamikiwa na wadau wa maji, lisijengwe stendi hiyo

[Image]
Wakiangali Mto Ruaha Mdogo

[Image]
Pana ka umbali

[Image]
Eeneo lenyewe ndio hilo

[Image]
Mto Ruaha Mdogo

Habari kamili kuhusiana na taarifa hii itakujia kesho; Utasoma kauli ya waziri, mkuu wa mkoa, katibu tawala wa mkoa, mstahiki meya, naibu meya, mkurugenzi wa NEMC na Bonde la Rufiji.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE UFAULU UMEPANDA HADI KUFIKIA ASILIMIA 58.25



Jumla ya watahiniwa laki 235,227 wa kidatu cha nne sawa na asilimia 58.25 ya waliofanya mtihani wa taifa kuhitimu kidatu hicho  kwa mwaka 2013 wamefaulu.

Ambapo Wasichana waliofaulu ni laki 106,792 na wavulana waliofaulu ni laki 128,435. 

Wanafunzi 74,324 sawa na asilimia 21.09 wamefaulu katika madaraja ya I -III.


Jumla ya wanafunzi waliopata daraja la 4 (division 4) ni laki 126,828, wasichana wakiwa 62,841 na wavulana 63,987.
 Shule 10 zilizoongoza ni St.Francis Girls, Marian Boys, Feza Girls, Precious Blood, Canossa, Marian Girls, Abbey
Shule kumi zilizoongoza: Anwarite Girls, Rosmini, na DonBosco Seminary
Zilizofanya vibaya: Singisa, Hurui, Barabarani, Nandanga, Vihokoli, Chongoleani, Likawage, Gwandi, Rungwa, Uchindile

DOKII,NYAMIDELA,MASCO NA EZENICE KUPAMBA KAMPENI ZA UCHAGUZI KALENGA


[Image]
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

Aliyekuwa msanii maarufu wa maigizo ya kibongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ambaye kwa sasa anajishughulisha na sanaa ya muziki hasa katika mambo ya siasa ameahidi kuwepo mkoani Iringa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge

Dokii aliyasema hayo juzi wakati aliposhiriki uzinduzi wa Mwaka wa Kilimo wa Afrika katika kijiji cha Kaning’ombe  kilichopo jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini

msaani huyo alisema atashiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni humo  huku akiahidi katika  kampeni hizo kusimama kwenye majukwa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumpigia kampeni mgombea wake, Godfrey Mgimwa.

Kwa upande wake msanii anayeshughulika na kazi za chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Iringa Damasi Masonda (Nyamidela) ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Godfrey Mgimwa washa moto kalenga alisema kuwa yeye kama msanii anayekitumikia chama hicho atahakikisha anafanya kampeni ya kumnadi Mgimwa katika jimbo lote la kalenga.

 Nyamidela ambaye alishawahi kuzunguka katika kampeni za urais mwaka 2010  amesema kuwa moto alioufanya katika kampeni hiyo na kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mkoa wa Iringa ndio atakao washa katika jimbo la kalenga. 

Nyamidela ambaye ametamba na vibao kama face book, mautamu, kiambule, ccm jiwe kuu, nimepata mzuka wa kura vijana zai pamoja na wimbo nyamidela ambao ndio umebeba jina la msanii huyo.

aidha katika kampeni  hizo wasanii wengine mkoani humo wanaotarajia kumnadi mgombea Mgimwa ni msanii anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mgata (Masco)  ambaye anatamba kwa kibao cha maisha magumu kijana pambana pamoja na  ezekiel Nice (Ezenice) anayeondoka kwa nyimbo za mchiriku huku akitamba kwa wimbo wa CCM chama bora.


uchaguzi huo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu  umetokana  na  aliyekuwa mbunge wake Dk William Mgimwa kufariki dunia Januari 1, mwaka huu,

Katika uchaguzi huo mgombea wa ccm Godfrey Mgimwa atapambana na wagombea wa vyama viwili vya siasa ambavyo ni Chadema kilichomsimamisha mgombea Grace Tendega na Chausta kilichomsimamisha Richard Minja.

JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA LAWASHIKILIA WATU SABA.

[Image]

JESHI la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu saba kwa makosa tofauti tofauti likiwemo la mkazi wa Makongati Tarafa ya Mololo aitwaye Mario Kibodya (30) kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili jina limehifadhiwa (8) na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
 
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake Kaimu kamanda wa polisi Mrakibu mwandamizi Peter Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 20 februari majira ya saa 9 kamili mchana.
 
Wakati huohuo mkulima aliyefahamika kwa jina la Junus Mkovano (35) mkazi wa Mgama tarafa ya Kiponzero anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumbaka mkulima mwenzake aitwaye Lucy Bahary (41).
 
Kaimu Kakamba alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 20 februari majira ya saa 1 kamili asubuhi ambapo mtuhumiwa huyo alimvamia mwanamke huyo akiwa shambani na kumfanyia kitendo hicho na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
 
Mbali na matukio hayo mawili ya ubakaji Kaimu Kakamba alisema watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi  mkoani Iringa kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bhangi misokoto 123.
 
Kamanda Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja watuhumiwa hao ni Joseph Lihundi, Justine Mwelungo, Benedict Nzuki, Baraka Malinga pamoja na Nathani Simon ambao walikamatwa na askari wakiwa doria maeneo ya Makorongoni.

CHADEMA YAHITIMISHA KURA ZA MAONI UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA, MWANASHERIA MWENDA AIBUKA KIDEDEA

[Image]
Sinkala Mwenda akiwa amenyanyuliwa juu baada ya ushindi wa kura za maoni juzi
MGOMBEA Sinkala Mwenda ameibuka kidedea wa kura za maoni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika mchakato wa kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kalenga.
Kura hizo za maoni zilizofanyika juzi katika ukumbi wa St Dominic, mjini hapa zilishirikisha wagombea 13.
Jimbo la Kalenga liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Dk William Mgimwa kufariki dunia Januari 1, mwaka huu.
Mwenda mwanasheia aliyemaliza shahada yake ya sheria katika chuo cha Ruaha Iringa, aliibuka kidedea baada ya kupata kura 132 dhidi ya kura 122 alizopata mshindani wake wa mkuu Grace Tendega.
Kabla ya kura hizo kuanza kupigwa wajumbe wengi walisikika wakimpigia chapuo, Tendega wakidai ana historia nzuri ya kisiasa katika jimbo hilo kwa kuzingatia kwamba katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 aligombea ubunge katika hilo kupitia chama cha Jahazi Asilia na kutoa upinzani mkubwa kwa Dk Mgimwa.
Mwingine aliyekuwa akipewa nafasi ni Zuberi Mwachula ambaye hata hivyo kutokuwepo kwake katika kura hizo za maoni kulisababisha wajumbe wamuadhibu kwa kutompa kura hata moja.
Pamoja na kurudisha fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho, Mwachula aliyekuwa Meneja wa Shirika la Kimataifa la Concern mkoa wa Iringa alishindwa kuhudhuria katika mchakato huo kwa kile kilichoelezwa kwamba yuko nje ya nchi kikazi.
Naye kijana machachari ambaye ni wakala na muuza magazeti maarufu mjini Iringa, Aidan Pungili pamoja na kumudu jukwaa kutokana na uwezo wake wa kujieleza vizuri aliambulia kura 2.
Uchaguzi  huo uliomalizika majira ya saa 4 usiku jana ulisimamiwa na Mjumbe  wa Kamati  Kuu ya Chadema Taifa Chiku  Abwao  na Mkurugunzi wa Oparesheni na Mafunzo ya chama hicho Benson  Kigaila.
Wagombea  wengine ambao  wameonyesha  kufanya vema kiasi  baada ya  kujiunga na Chadema  wakitokea  CCM ni pamoja na Dr Evaristo Mtitu  aliyepata  kura 32 na Ancent Sambala kura 22.
Wengine walioshiriki kura hizo na kura zao kwenye mabano ni  Akbar Sanga (21), Rehema Makoga (4), Henry Kavina (9), Mussa Mdede (48), Mchungaji Samweli  Nyakunga (2) na Mwalimu Vitus Lawa akipata kura (14).
Katika nasaha zake kwa wagombea na wajumbe, Kigaila alisema ushindi wa kura za maoni sio kigezo pekee kinachotumiwa na Chadema kupata mgombea.
“Tunataka hili lieleweke, huu ni mwanzo wa mchakato. Ni lazima tupate mgombea kwa kuzingatia mazingira ya Kalenga, awe anakubali ndani ya chama na kwa wapiga kura wajimbo hilo kwasababu tunataka kushinda,” alisema.
Alisema baada ya kura hizo za maoni Kamati Kuu ya Chadema Taifa itakutana kesho Ijumaa, Februari 14 na kufanya maamuzi ya mwisho kwa kuzingatia mambo mengi zikiwemo taarifa za kiintelejensia za ndani ya chama.
“Tuna heshimu sana kura za maoni, lakini sio kigezo pekee. Watanzania wana imani sana na Chadema, kitakachotufanya tushinde ni aina ya mgombea tunayempeleka kwa watu, vinginevyo tunaweza kufanya kampeni kubwa na tukashindwa,” alisema.

Taarifa za awali kutoka ndani ya chama hicho zimedai kwamba katika kampeni zao watatumia helkopta mbili na magari nane ya chama  ili kuyafikia makundi ya wapiga kura kwa kasi zaidi.

KESI YA DAUDI MWANGOSI YAANZA KUSIKILIZWA, MWANAHABARI AKAMATWA NA KUBAMBIKIZIWA KESI

[Image]
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, Frank Leonard ( wa nne kushoto mwenye begi ndogo begani) akiwa nje ya mahakama kuu kanda ya Iringa na wanahabari wengine mara baada ya kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya Daudi Mwangnosi kusikilizwa

KESI ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Mkoani Iringa, Daudi Mwangosi imeanza kusikilizwa hii leo baada ya kilichoelezwa na upande wa mashtaka kwamba uchunguzi wake umakamilika.

Kama ilivyo ada, makechero wa Polisi wengi wao wakiwa wamavaa kiraia walikuwepo mahakamani hapa huku wakijaribu kuwazuia wanahabari kutekeleza wajibu wao.

Katika mazingira ya kutatanisha, mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo, Frank Leonard ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa alikamatwa na askari wanne waliokuwa wamevaa kiraia kwa kile kilichoelezwa kwamba alikuwa akipiga picha mahakamani wakati kesi ikiendelea.

Baada ya kukamatwa Leonard, alifikishwa kituo cha Polisi cha Kati mjini Iringa na kuachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi.


Akizungumza na wanahabari baada ya kuachiwa huru, Leonard alisema "wapo baadhi ya askari kwa makusudi wanataka kubomoa mahusiano baina ya wanahabari na jeshi la Polisi ambayo yanaendelea kujengwa na kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi."


Alisema kitendo cha kubambikiziwa tuhuma ndani ya muhimili wa dola unaojitegemea (mahakama) ni kitendo cha uzalilishaji kinachotaka kuaminisha umma kwamba wanahabari ni watu wasiotaka kufuata taratibu za kimahakama.


Alisema akiwa ndani ya chumba cha mahakama hiyo alikamatwa na askari hao bila idhini ya Jaji wa Mahakama Kuu wakati akizima simu yake ya mkononi iliyokuwa katika mtetemo.



"Nilikuwa nazima simu yangu hao askari hao kwasababu wanazojua wao wenyewe waligeuza suala hilo ili lionekane katika sura wanayoitaka na hatimaye wanifungulie mashtaka," alisema.


Alimshukuru Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Iringa, Ngoi kwa kumtendea haki na baada ya kupata ushahidi kufutilia mbali kesi hiyo.

Akizungumza na wanahabari, Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Dunstan Nduguru aliwashangaa Polisi kwa kuingia shughuli za mahakama.

"Hata kama mwandishi huyo angekuwa anapiga picha, haikuwa kazi yao kumkamata mpaka wapewe agizo na Jaji Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo," alisema.

Pamoja na askari hao kuwazuia wanahabari kuchukua picha mara baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani, Nduguru alisema utaratibu wa mahakama unawaruhusu wanahabari kuchukua picha kabla shughuli kabla shughuli za mahakama hazijaanza na baada ya shughuli hizo kwisha.

"Kuwazuia wanahabari kufanya kazi zao kwa utaratibu huo sio sahihi; siku nyingine mkiona kuna dalili ya kupata bugudha kama hiyo naomba mnijulishe ili niondoe mzozo huo," alisema. 

Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Mary Shangali, Wakili wa upande wa mashtka, Adolph Maganga alisema Adolph Maganda alisema kwa kukusudia mtuhumiwa Pacificius Cleophace Simoni anatuhumiwa kumuua Mwangosi kinyume na kifungu cha sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Alisema katika tukio hilo lililotokea Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa, mshtakiwa alifyatua bunduki yake na kusababisha kifo cha marehemu, papo hapo.

Alisema siku ya tukio marehemu alikuwa Nyororo kwa ajili ya kuripoti na kutoa taarifa kwa umma juu ya mkutano uliokuwa ufanywe na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alisema mshtakiwa akiwa mmoja wa wafanyakazi wa Polisi, waliwasihi Chadema wasifanye mkutano huo kabla wafuasi wake hawajaanza kurusha mawe kwa Polisi na baadhi yao kupata majeraha.

Kutokana na mzozo huo, wakili huyo wa serikali alisema polisi walipiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi hao kabla mshtakiwa huyo hajamfyatulia bomu marehemu.

Wakili huyo aliwasilisha ramani ya eneo la tukio, ripoti ya mtaalamu wa milipuko na ripoti ya daktari aliyechunguza mwili wa marehemu Mwangosi na gazeti la Mwananchi la Septemba 3, 2012 lililochapisha  picha ya tukio hilo katika ukurasa wa mbele kama vielelezo vinavyohusiana na kesi hiyo.

Wakili wa upande wa utetezi Lwezaula Kaijage alitaja mambo wanayokubaliana katika kesi hiyo kuwa ni jina na anuani ya mshtakiwa na kwamba marehemu Mwangosi alikufa kifo ambacho si cha kawaida.

Na kwamba mshtakiwa Simoni alikamatwa na amefikishwa mahakamani akihusishwa na mauaji hayo.

Wakili Kaijage alisema vielelezo vingine vilivyoletwa na upande wa mashtaka hawakubaliani navyo kwakuwa vinahitaji ushahidi kutoka kwa wahusika.

Jaji Shangali aliahirisha kesi hiyo mpaka kikao kingine cha mahakama kuu kitakapoitwa ili ianze kusikilizwa.

BREAKING NEWSSssssss CCM WASHINDA KWA KISHINDO KATA ZOTE TATU MKOA WA IRINGA , NJOMBE CHADEMA WAIGALAGAZA CCM .........................................................

CHAMA  cha  mapinduzi (CCM)  mkoa  wa  Iringa  kimefanikiwa  kutetea kata  zake  zote tatu ambazo  leo   wananchi  wameshiriki  kupiga kura  kuwachagua madiwani  kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki  dunia  huku chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kikishindwa  vibaya katika  uchaguzi huo.

Mbunge  wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambae  alikuwepo  eneo la Nduli  akifuatilia  matokeo  ya uchaguzi huo pamoja na  wafuasi wa Chadema  alilazimika  kuondoka katika eneo hilo  baada ya  kubaini kuwa hali ya ushindi kwa Chadema ni ndoto.
Huku   wafuasia  wa  CCM  wakionekana  kumpongeza  aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na  kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa  Hassan Mtenga kuwa  kazi  yake imeonyesha inaonyesha  wazi  safari yake ya  kulitwaa jimbo la Iringa mjini .

Katika  Matokeo hayo ambayo hadi sasa  majira ya saa 12.50  bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 810 huku  Chadema  wakifuatia kwa kura 491

Mbali ya  matokeo  hayo ya kata ya  Nduli pia  CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za  wilaya ya  Kilolo.

Wakati katika kata ya  Njombe mjini mgombea  wa  Chadema amepata  kukibwaga vibaya  chama  cha Mapinduzi (CCM) ambapo  matokeo yanaonyesha  mgombea wa CCM amepata  kuongoza kituo kimoja pekee   kwa tofauti ya  kura  2  huku  vituo vyote  Chadema ikiibuka kidedea.

NYOTA YA JACKSON KISWAGA YANG'ARA KALENGA ,WANA KALENGA WAWAOMBA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU KUTOWACHAGULIA WINGINE ZAIDI YA KISWAGA

Wazee wa kabila la Kihehe, kata ya Kalenga mkoani Iringa wakimpa heshima ya kichifu  alipokuwa Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga ambae  leo anapigiwa  kura  za maoni  za  kusimamakugombea  ubunge  kupitia  CCM jimbo la Kalenga
Bw Kiswaga  akiwashukuru  wana kalenga kwa maombi  na imani  yao kwake .

Wakati  leo  wajumbe wa Halmashauri  kuu ya CCM jimbo la kalenga  wanakutaka  katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa  kumteua  mgombea  ubunge  kupitia  CCM katika  jimbo la Kalenga  wana Kalenga  wasema isingekuwa demokrasia  kwa  kila mmoja kugombea basi  wangempitisha moja kwa moja  Jackson Kiswaga  kuwa mbunge  wao

Kwani   walisema jitihada zake  za kimaendeleo  katika  jimbo la Kalenga na mkoa  wa Iringa ni kubwa na hakuna mgombea  hata mmoja kati ya  tisa  waliojitokeza ambae anaweza kumfikia  Kiswaga katika  kujitolea  kwa shughuli za kimaendeleo jimbo la Kalenga na  mkoa wa Iringa .

Alisema Samson Kalinga  kuwa  hata  wakati  wa uhai  wake  mbunge wa  jimbo  hilo Dr  Wiliam Mgimwa alipata  kumpongeza  kwa  kuonyesha ukeleketwa wa kweli wa maendeleo ya wana Kalenga kwa  kuchangia shughuli mbali mbali  za kimaendeleo .

Hata  hivyo  alisema imani ya  wana kalenga  ni kuona  wana CCM hao  leo  wanamchangua mtu  mwenye  malengo ya kweli  ya  kuwakomboa wana Kalenga  kama  ilivyo kwa Kiswaga na  si vinginevyo .

Kiswaga  amepata  kujitolea  kuchangia  sekta  ya elimu kwa kujenga madarasa katika  shule ya  sekondari Lipuli, kununua  vitanda  vya  kujifungulia  wakina mamaa Hospital ya Ipamba , kuchangia  madawati na umeme shule ya msingi Tanangozi ,kuchangia madawati shule ya msingi Lulanda na maeneo mengine  mengi.

Wengine  wanaowania  katika mchakato  huo ni pamoja na Evaristo Mtitu , Godfrey Mgimwa ,Hafsa Mtasiwa, Gabriel Kalinga, Peter Mtisi, Edward Mtakimo, Bryson Kibasa na Thomas Mwakoka.
 
Huku  anayepewa nafasi  kubwa ya  kuibuka na ushindi  huo  hadi  sasa ni Kiswaga  na  kwa mbali  huenda  akiafuatiwa na kalinga na Mtasiwa pamoja na Mtitu huku  mtoto  wa Mgimwa Bw Godfrey  akipewa nafasi ndogo ya  ushindi katika  mchakato huo

CCM NJOMBE NA IRINGA WALAANIA VURUGU ZA CHADEMA WATAKA WANANCHI WACHAGUE CCM, FILIKUNJOMBE AWAFUNDA NJOMBE , JESHI LA POISI LAONYA WATAKAOFANYA VURUGU KESHO KUKIONA


Kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akiwa katika mkutano wa kampeni kata ya Nduli Iringa 
 .....................................................................................................
WAKATI  wananchi  wa kata ya  Nduli jimbo la Iringa mjini na  wale  wa kata ya Njombe mjini  jimbo la Njombe  kusini  kesho wanashiriki katika zoezi la upigaji  kura katika  uchaguzi mdogo  wa udiwani ,chama  cha mapinduzi (CCM ) mkoa  wa  Iringa na Njombe  kimelaani  vurugu  zinavyofanywa na viongozi na  wafuasi  wa Chadema katika chaguzi hizo na  kuwaomba  wananchi kujitokeza  kwa wingi karika uchaguzi  huo bila vitisho na kuchagua wagombea  wa CCM.
Huku  jeshi la  polisi Imkoa  wa Njombe likidai limejipanga kwa ulinzi polisi mkoa  wa Iringa limedai   kuwa  kuna  kikundi  kinasakwa kwa  kutaka  kufanya  vurugu katika uchaguzi huo na kuwaondoa  hofu  wananchi kufika  kupiga kura  bila kuogopa .
Kaimu  katibu  wa CCM mkoa  wa Iringa Hassan Mtenga  alitoa  kauli hiyo leo  wakati akizungumza na mtandao huu  wa www.matukiodaima.com..

Alisema  kuwa  lengo la chama  chochote cha siasa ni  kuona  wananchi  wake  wanaendelea  na shughuli  zao katika hali ya amani na utulivu   na  kuwa chama  chochote cha siasa  kinachojihusisha na vitendo vya  kinyama dhidi ya wananchi  wake ni wazi hakipo kwa  ajili ya kulinda amani ya wananchi.

Hivyo  alisema vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Chadema na mbunge  wa  jimbo  hilo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  juzi ni  wazi kuwa Chadema hakipendi kuna wananchi  wakifanya shughuli  zao kwa amani  na kutokana na unyama  huo  unaofanywa na Chadema ni vema  wana Nduli kuendelea kuchagua  CCM ili amani  iliyopo izidi kulindwa .

Mtenga  alisema mbali ya CCM kuruhusu  vyama  vingi vya  siasa  mwaka 1994 ila bado baadhi ya  vyama  vya siasa  vimekuwa ni mwanzo  wa  kuvuruga amani ya watanzania na  kuwa ni vyama vya  kusababisha  vurugu  hata mauwaji kwa  watanzania .

Alisema  kuwa haiwezekani  kwa  chama makini chenye kupenda  amani  kuona kinashabikia vurugu  na hata  wabunge  wake  na  viongozi  wake kila kukicha  wakikamatwa kwa  vurugu katika mikutano.

Mtenga  alisema  jimbo la Iringa mjini limeendelea kuzolota katika maendeleo  kutokana na vurugu  za kisiasa za mara kwa mara  zinazojitokeza na  kuwa hata  maendeleo  yanayoonekana kama huduma ya maji  safi kwa wananchi wa Nduli ni  jitihada za mbunge wa  wa CCM aliyekuwepo kabla ya Msigwa pamoja na mbunge viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati ambae  kila  wakati bungeni amekuwa akipigania .

"Tunapenda  kuwahakikishia  wana Nduli  kuwa  iwapo  mtatuwekea mrithi  wa diwani  marehemu Iddi Chonanga  kutoka  CCM pale  alipoishia  diwani  wenu katika maendeleo pataendelezwa  zaidi  kwani  mwenye  kukabidhiwa  mikoba ya diwani  aliyekufa ni lazima awe  kutoka  CCM na si vinginevyo"

Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akizungumza katika mkutano huku mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe akimsikiliza
............................................................................................................................
Kwa  upande  wake  Chama  cha  Mapinduzi mkoa  wa Njombe kimeeleza  kusikitishwa na vurugu  mbali mbali  zinazojitokeza katika kampeni  za udiwani kata ya  Njombe mjini baada ya  wafuasi na viongozi wa Chadema  kuwapiga wananchi .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa  jimbo la Njombe Kaskazin  alisema kuwa siasa  inayofanywa na  wana Chadema kwa Njombe mjini ni siasa ya kinyama na kuwa ilipendeza kwa vyama vya  siasa  kushindana kwa sera na hoja badala ya  kushindana kwa vurugu .

HIvyo  alisema  kuwa ili  CCM kuendelea  kutimiza ahadi zake na kuongoza kata  hiyo ni  wajibu wa  wananchi wa Njombe kuchagua mgombea wa CCM badala ya  kuwasikiliza wafuasi hao wa Chadema kutoka nje ya Njombe ambao wapo kwa ajili ya kutaka kuvuruga uchaguzi  huo.

Huku mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwataka  wana Njombe mjini  kutokubali  kata   hiyo ya Njombe mjini  kuchukuliwa na vyama vya upinzani na  kuwataka  kuchagua chama  cha mapinduzi.

Filikunjombe  alitoa kauli hiyo  wakati wa kumnadi mgombea  udiwani wa CCM katika kata  hiyo ya Njombe mjini na  kuwa Wilaya ya  Ludewa na Njombe ni wilaya  majirani na  kuwa  masilimali za  Ludewa ambazo ni makaa ya mawe na Liganga si tu ukombozi kwa  wana Ludewa ni ukombozi wa mkoa wa Njombe na Taifa  hivyo kuwataka  vijana  kuendelea  kuwa na imani na serikali ya chama cha mapinduzi chini ya Rais Dr Jakaya  Kikwete ambae katika utawala  wake watanzania  wanashuhudia miradi hiyo mkikubwa  inaanza.

Alisema  kuwa uchumi  wa Njombe na Ludewa  baada ya kuanza kwa miradi  hiyo utakuwa  zaidi kutokana na vijana  wengi kupata ajira katika  miradi hiyo.
                                        LISU AKIWA NA MKEWE
Mungu amembariki kwa watoto mapacha watatu Wawili wakiwa Wa Kiume na Mmoja wa Kike, Mama na Watoto Wanaendelea vema.

BAADA YA MWIMBAJI MATHA MWAIPAJA KUPATA MTOTO WA KIUME SASA NI ZAMU YA MWIMBAJIA ANAYESIFIKA SANA KWA KUIMBA LIVE JOHN LISU AMBAYE WIKI HILI MUNGU AMEMJALIA KUPATA MAPACHA WA TATU NA MKEWE NELLY KAISI LISU

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog