NA DENIS NYALI IRINGA
Kufuatia kuripotiwa kwa wingi wa matukio ya ubakaji mkoani iringa na tanzania kwa ujumla mkuu wa wilaya ya kilolo Mh Asia abdallah ameagiza kuhamishwa mara moja mkuu wa kituo cha mtitu kilichopo wilaya ya kilolo kutokana na uzembe wa kutofikisha taarifa za tukio la ubakaji kwa mkuu wa kituo cha polisi wilaya .
Tukio hilo limetokea baada ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano na nusu kubakwa na watu watatu katika kijiji cha mawambala na kuharibiwa vibaya sehemu ya mwili wake.
Akizungumzia Tukio hilo la kikatili lilotokea katika kijiji cha
mawambala kata ya ukumbi wilaya ya kilolo mkoani iringa afisa mtendaji wa
kijiji hicho NOLASCO KIHWELO amesema taarifa juu ya tukio hilo
zimelipotiwa na mama wa mtoto huyo.
Mtendaji wa kijiji ameongeza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo
yeye pamoja na wazazi hao wakishirikiana kumkamata mtuhumiwa mmoja huku wengine
wawili wakikimbilia kusikojulikana.
Akizungumza kwa uchungu mama wa mtoto huyo amesema alikuwa
akipika jikoni ndipo baba mdogo wa mtoto huyo alipo mwona mtoto huyo akishindwa
kutembea na ndipo mama yake alipofika na kumkuta tayari ameshafanyiwa ukatili
huo.
NAYE mtoto aliyefanyiwa ukatili huyo ambaye hajui
lugha ya Kiswahili akizungumza kwa lugha ya kihehe amesema watuhumiwa
waliotekeleza kitendo hicho walimtisha kuwa asimwambie mtu na endapo akisema
watamkata kwa panga.