Mgeni rasmi Geogina kiduge wakati akikaribishwa meza kuu. |
Mratibu wa mradi edson mwaibanje akitoa maelezo juu ya mradi huo |
SOMA ZAIDI.
Jumla ya wanawake 85 kutoka katika kata za mji wa mafinga wilaya ya mufindi mkoani iringa wamenufaika na elimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza na DENIS NYALI BLOG mratibu wa mradi wa mabadiliko ya tabia nchi na athari zake ambao unafadhiriwa na WOMEN FUNDS,EDSON MWAIBANJE amesema wameamua kutoa elimu hiyo kwa wanawake kwa kuwa wana nafasi kubwa kuliko wanaume na ndio wamekuwa waathirika wa kwanza wa mabadilko ya tabia nchi.
Aidha mratibu huyo amesema kutokana na jamii ya kimataifa kuelimisha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kupitia elimu ambayo wanawake hao wameipata itawasaidia kuelimisha wana jamii katika kata zao na kutafuta njia mbadala itakayo tumika kukabiliana na hali hiyo.
Nao baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wameshukuru kwa elimu hiyo waliyopewa na kuahidi kuifanyia kazi huku wakielezea kuwa kwa sasa ratiba ya kilimo imekuwa haitabiliki kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
0 comments:
Post a Comment