Operesheni
ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri
wawili ambao pia walikuwa manaibu mawaziri katika Serikali ya Awamu
ya Nne.
Taarifa
kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli
alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele
ya mawaziri wenzao kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri
kilichofanyika hivi karibuni.
"Ni
mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa
moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....
"Mawaziri
wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili
tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo,
aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.
“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.
Mawaziri
hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania
Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara
ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati
akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.
Chanzo
hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao
alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake
ya kuwaletea wananchi maendeleo.
“Magufuli
alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana.
Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho
Rais
Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na
kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya
hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.
Utendaji
wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika
kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya
kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisadi.
0 comments:
Post a Comment