Home » »

JOYOUS CELEBRATION YAVUNJA REKODI AFRIKA YA KUSINI


Kundi la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini limevunja rekodi ya kuwa kwaya ya kwanza nchini Afrika ya kusini kushika nafasi ya kwanza kwenye mtandao wa kuuza muziki wa iTune kupitia album yake mpya ya 18 iitwayo 'One Purpose' ambayo imetoka rasmi jana kupitia mtandao huo.

Album hiyo ya Joyous ilianza kupigiwa debe kwenye mtandao wao wa Facebook mapema wiki mbili zilizopita kwa watu kulipia kabla ya siku yenyewe rasmi kutoka, ambapo iTune kwakushirikiana na kundi hilo waliweka shindano kwa mashabiki wa kundi hilo kueleza kwanini wanahamu na album mpya ya kundi hilo, ambapo mshindi anajinyakulia kadi ya manunuzi ya iTune ambayo inamwezesha mshindi kununua nyimbo mbalimbali katika mtandao huo kwakiasi cha kadi yake.

Album mpya ya Joyous itakuwa na nyimbo 39 kwa maana ya CD tatu za kusikiliza huku pia ikitegemewa kwamba kutakuwa na DVD mbili kama ilivyokuwa kwa toleo lao la 15 ambalo lilikuwa na sehemu ya kwanza na ya pili. Joyous ni kundi ambalo tayari limejijenga nchini Afrika ya kusini na kupendwa nje ya mipaka ya nchi hiyo tangu kundi hilo kupitia mwimbaji wake kutoka Nigeria mwenye uraia wa Afrika ya kusini pia mchungaji Agu Uchechukwu ama Uche double double kuimba wimbo wa 'My God is good' ambao ulifungua mipaka ya kundi hilo kufahamika zaidi duniani, kazi ambayo pia inaendelezwa na Mzimbabwe Mkhululi Bhebhe ambaye nyimbo zake na Uche zimetokea kupendwa na kutizamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kuliko waimbaji wengine wa kundi hilo.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog