ASKOFU DR SOLLO AMSHAURI RAIS KIKWETE KULIVUNJA BUNGE LA KATIBA, AWASHANGAA UKAWA KWA VURUGU
![]() |
Rais Dr Jakaya Kikwete |
![]() |
Viuongozi wa UKAWA |
Askofu Dr Boaz Sollo akiwa katika moja kati ya mikutano yake ya kuliombea Taifa amani
UMOJA wa katiba ya wananchi (UKAWA) wazidi kukaliwa kooni baada yaaskofu wa kanisa la Overcomers Power Centre Iringa Dr Boaz Sollo kupinga vikali uamuzi wa UKAWA kutoka bungeni na kwenda kwa wananchi kabla ya kuifanya kazi waliyotumwa bungeni kama wajumbe wa bunge la katiba na hivyo kumshauri Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete kulivunja bunge hilo ili kuepusha amani kuvurugwa nchini.
Huku akisema kuwa akiwa kama mtumishi wa Mungu anaamini kabisa kuwa serikali mbili ni jibu la watanzania katika endeleza umoja ,amani na mshikamano ulioachwa na waasisi wa Taifa hili hayati Baba wa TaifaMwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Rais waKwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kuvurungwa na wanasiasa wachache wasiopenda amani ya nchi hii .
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es salaam ambako amealikwa kwa huduma za kanisa , askofu Dr Solloa alisema kuwa tayari kanisa lake limeanza kufunga na kuomba kwa ajili ya amani nchini na kuliombea bunge hilo la katiba ili mwenyezi Mungu kuliunganisha bunge hilo na kuepusha mgawanyiko ulioanza kujitokeza na kundi hilo la wana Siasa wanaojiita wana UKAWA .
" Watamzania tulipongeza uteuzi wa Rais wetu mpendwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuteua miongoni mwa watanzania wachache kati ya wengi kwa ajili ya kwenda kushiriki bunge hilo kuandaa katiba ya nchi huku tukiamini kuwa walioteuliwa wangetufikisha pazuri zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo wajumbe hao wameanza kuhatarisha amani na utulivu nchini "
Kitendo cha wajumbe wa bunge hilo kutoka nje ya ukumbi na kutaka kuanza kuzunguka mikoani ni sawa na kuwasaliti wananchi ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu wajumbe hao kuwaletea katiba mpya ila sasa wameanza kutishia amani ya nchi kwa kutafuta huruma ya wananchi katika kuungwa mkono wao na vyama vyao.
" Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais Dr Kikwete ni kulivunja kabisa bunge hilo ili kunusuru amani ya nchi hii ambavyo dalili ya kuvurugwa imeanza kujitokeza kupitia UKAWA ....tulitegemea wajumbe hao wangebaki ndani ya bunge na kutuandalia katiba bila kuunda umoja wa kuanzisha vurugu nchini kwani wote bila kujali vyama vyao na taasisi zao walizotoka walipaswa kuwa kitu kimoja katika bunge hilo kwa kuwasilisha hoja za kuwa na katiba bora si vinginevyo "
Alisema kuwa ni vema kuendelea na katiba iliyopo kuliko kusubiri katiba ya wajumbe hao ambayo mwelekeo wake si mzuri bali upo kwa ajili ya matakwa ya wachache kisiasa .
Askofu huyo alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wanachanganywa na wana siasa hao ila ukweli wazanzibar na watanzania wanapenda kuona amani iliyopo inaendelea kuwepo na suala la maendeleo linaendelea na sio utitiri wa serikali hali maisha yao kiuchumi ni duni .
Hata hivyo alisema kutokana na mwenendo wa bunge hilo kwa sasa kanisa lake limetangaza mfungo wa maombi maalum kwa ajili ya Tanzania ili kuepuka chuki kupandikizwa na wachache kwa lengo la kuvuruga amani yetu .
source. francis godwini.
0 comments:
Post a Comment