BEI YA KIINGILIO KWENYE UZINDUZI WA JOHN LISU HADHARANI.
Waandaaji wa uzinduzi wa albamu ya “Uko Hapa” ya mwimbaji
nguli wa muziki wa Injili Tanzania, John Lisu unaotarajia kufanyika
Oktoba 5, mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam, kampuni ya
Msama Promotions wametangaza viingilio rasmi.
Msama Promotions wametangaza viingilio rasmi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama viingilio hivyo ni shilingi 5000
kwa viti vya kawaida na watoto na shilingi 10,000 kwa viti maalum.
Msama ametoa wito kwa waamini
mbalimbali nchini kujitokeza katika uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake
katika tasnia ya muziki wa Injili nchini.
0 comments:
Post a Comment