HEBU LEO TAFAKARI TOFAUTI YA KIONGOZI NA MTAWALA
Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM) |
KIONGOZI
1. Ni mtu wa Watu
• Kiongozi kipaumbele chake ni watu
• Anakuna kichwa afanye nini ili watu wake waweze kuishi kwa amani na furaha.
• Kupenda kuwasikiliza watu wanasema nini, wanalia juu ya nini, wanacheka juu ya nini nk.
2. Hugusa Moyo wa Mtu
• Mkono wa kiongozi hugusa moyo wa wafuasi.
• Ushawishi wake kiongozi huwa sio wa akilini au kichwani bali hupenya hadi ndani ya moyo wa mtu.
• Anauhakika wa kuwa na watu nyuma yake kumfuata popote atakapo kwenda
3. Huuliza Kuna nini Moyoni
• Hutaka kujua nini kimeujaza moyo wako
• Mbona huna furaha moyoni kumetokea nini? Nifanye nini kukusaidia furaha ya moyo wako iweze kurudi.
• Mbona unafuraha sana leo nini kimetokea mpaka umekuwa mwenye furaha hivyo moyoni? Unahitaji kuendeleza hiyo furaha yako.
4. Hufundisha Watu
Kiongozi hufundisha wato na sio kufundisha somo
Kiongozi hutamani hata Yule mbumbumbu asiyeelewa darasani au kanisani ameelewa na kupokea kitu.
Huchukua juhudi za makusudi kufuatilia zaidi.
Kipimo chake cha uwelewa wa wanafunzi ni Yule mtu wa mwisho kuelewa darasani.
5. Ana upeo wa Kuona Mbali
• Huangalia faida itakayopatikana kule mbele sio lazima sasa.
• Anawekeza sasa kwaajili ya sasa na badae
• Anawekeza vikubwa anavuna vikubwa pia.
• Anafanya leo kwajili ya kesho
6. Ni Mbunifu na Muanzishaji (Originate)
• Anamawazo mapya
• Anabuni na kuwapa wengine
• Anaweza kubuni na kupitisha barabara katikati yam situ mnene mahali usingefikiri kamwe barabara ingepita
• Ni mvumilivu kusubiria matunda kwa wakati wake.
7. Hujiuliza Nini na Kwanini (What and Why)
• Ninafanya nini na kwanini ninafanya hiki.
• Huwa na sababu ya kutosha kumuwezesha kufanya anachokifanya kwa nguvu zaidi.
MTAWALA
1. Ni Mtu wa Vitu
• Kitu cha muhimi kwake ni vitu sio watu.
• Kama ni mmiliki wa basi, likipinduka chakwanza kuuliza gari imesalimika haijaumia?
• Akiambiwa mzee gari imepona ila watu wote wamevunjika vunjika na kufa atasema afadhali.
• Akiambiwa gari imesagiga sagika hakuna hata cha kuokota ila watu wote wamesalimika ataangua kilio kweli maana gari imekwisha.
2. Hugusa Vitu vya mtu
• Tofauti na kiongozi mtawala hagusi moyo anagusa vitu
• Mitambo au vitu nivyamuhimu sana kuliko watu.
• Chombo kikiungua ni hasara kubwa sana lakini mtu akivunjika mguu ni kawaida ajali kazini.
3. Huuliza Kunanini mfukoni
• Tofauti na kiongozi ambaye huuliza kunanini moyoni, interest ya mtawala nikujua kuna nini mfukoni.
• Hugusa pochi na sio moyo
• Hugusa kichwani na sio Moyoni
4. Hufundisha Somo
• Hufundisha somo watu na sio kufundhisha watu somo
• Hufundiaha kumaliza mtaala na sio kufundisha kuwaelimisha.
• Hufundisha kwa kuwapa wanafunzi taarifa, na sio badiliko la maisha.
• Teaching for information not transformation.
5. Ana upeo wa Kuona ya Sasa
• Hushughulika sana na ya sasa.
• Macho yake ni dhaifu hayana nguvu ya kuona ya mbele.
• Anataka kupanda leo na kuvuna leo.
• Hana mpango wa kuwekeza kwaajili ya baadae.
6. Huiga na kukarabati Kilichokuwepo (Immitate)
• Hana uwezo wa kubuni vitu vipya.
• Yeye huendeleza walivyobuni wengine
• Kama ni barabara hana uwezo wa kubuni barabara mpya ataziba tu viraka vya barabara aliyokabidhiwa.
• Kama ni kanisa akipewa hata kama likijaa hawezi kuja na mpango mpya wa kujenga linguine la kisasa bali atakuwa anabadilisha tu milango na kupiga rangi upya nk.
7. Hujiuliza Kivipi na Lini (How and When)
• Nitafanyaje hiki nilichopewa kiendelee kuonekana kizuri?
• Lini nitaweza kutekeleza hii kabla sijanyan’ganywa madaraka haya?
NB: VIONGOZI WENGI TUNAO WAITA “VIONGOZI” KIUKWELI SIO VIONGOZI NI WATAWALA