IRNGA LEO PATAWAKA MOTOOOOOOOOOOOOOO

                             AJALI YAUWA WAWILI NZEGA TABORA

 Ajali iliyohusisha magari mawili imesababisha waliokuwa kwenye gari dogo kupoteza maisha maeneo ya Nzega, inaasemekana chanzo cha ajali ni speed ya gari dogo na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha eneo hilo.

             NEEMA TENA KWA WAKAZI WA NYANDA ZA JUU                                                     KUSINI.


Mara kwa mara kwenye jiji la Dar es Salaam, yamekuwa yakiandaliwa matamasha mbalimbali ikiwemo la Krismasi na Pasaka chini ya kampuni ya Msama Promotions. Lakini kwa wakati huu kilio cha wananchi kimesikika, hasa baada ya kampuni hii kuamua kupeleka tamasha la Krismasi kwa mwaka 2014 kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma. Haya yote ni kuanzia tarehe 25 ndani ya jiji la Mbeya, na kisha kuelekea Iringa tarehe 26 kabla ya kumalizia na Songea iliyopo mkoa wa Ruvuma tarehe 28 Disemba 2014.


Kwaya Maalum kuzindua Mbeya
Kwaya maalum jijini Mbeya wiki iliyopita iliingia kambini kwa siku moja kujiandaa na uzinduzi wa albamu yao ya Mubhopeghe Pa Finganilo (Kimbilieni kwenye ahadi) yenye nyimbo nane.

Kwa mujibu wa Mchungaji wa Kanisa wa EAGT, Zacharia Mwakasaka kambi hiyo inashirikisha waimbaji ambao ni Maaskofu, Wachungaji na viongozi mbalimbali wa dini waliomo kwenye Kwaya hiyo.

Mwakasaka alisema uzinduzi huo unashirikisha waimbaji, maaskofu na wachungaji waliopita kwenye mikono ya mzee Amulike Mwakiteka (84).

Mwakasaka alisema kupitia uzinduzi huo waumini mbalimbali watajionea viongozi hao ambao wanaongoza makanisa mbalimbali hapa nchini.

Mwakasaka alizitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni pamoja na Mubhopeghe Pa Finganilo, Lazaro, Ilisubha ‘Jua Linachomoza’, Yesu alipokwenda, Jesu Bho Ikufyuka ‘Yesu alipopaa’, Matendo, Gwe Kyala Mwikemo ‘Mungu Mtakatifu’ na Nasobhile ‘Nilikuwa nimepotea Msituni’

Mwakalebela mgeni Rasmi Iringa
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela Desemba 26 anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Krismasi mkoani Iringa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Mwakalebela anatarajia pia kuwaongoza waumini mbalimbali mkoani humo kwa lengo la kumtukuza Mungu kupitia waimbaji mbalimbali hapa nchini.

Msama alisema Mwakalebela atafanikisha lengo la kusaidia wenye uhitaji maalum kama Yatima, Wajane na walemavu ambao wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali.

Msama alisema Mwakalebela ni mdau ambaye anatakiwa aendane na kauli mbiu ya Tanzania ni yetu, Tuilinde na Kuipenda ambayo inachochea wadau ambao wanatakiwa kusaidia wadau hao.

Tamasha hilo linatarajia kuanza Desemba 25, kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kabla ya kuhamia Iringa na kumalizia Desemba 28 Wilayani Songea kwenye uwanja wa Majimaji.
-

MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA TUNAJIVUNIA AMANI NA UMOJA






 HI NI HATARI KWA KIPINDI HIKI CHA MVUA MTOTO AOPOLEWA KWENYE DIMBWI LA MAJI MACHAFU.




Na Mathias Canal, Mufindi

Mtoto mwenye umri ya miaka 5 afariki dunia kwenye dimbwi la maji machafu karibu na mtaa wa stendi ya mabasi Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Mtoto huyo alipotea nyumbani takribani siku 3 zimepita ambapo mama mzazi alitoa taarifa jeshi la polisi liweze kumsaidia lakini juhudi hizo haikuzaa matunda ambapo hii leo amekutwa kwenye dimbwi la maji 

HII NI HATARI HATA KAMA NI UMASIKINI????????? DUH!!!!BINTI ALIYEONGOZA MATOKEO YA DARASA LA SABA AOZESHWA KWA MAHARI YA KILO 2 ZA SUKARI.

Pamoja na Serikali kuendelea kupiga vita wazazi kuwaoza mabinti zao wakiwa bado wadogo lakini bado kuna baadhi ya makabila hapa nchini wameendeleza utamaduni huo kwa kuwaoza mabinti zao sababu kubwa ikitajwa kuwa ni tamaa za kutaka kujilimbikizia mali. 
Lakini kwa msichana huyu wazazi wake wameonekana kutoijali hata ile mali waliyopewa kwani wameweza kumwozesha binti yao wa kike kwa mahari ya kilo mbili za sukari toka kwa mfugaji wa kabila la kimasai. 
Gazeti la NIPASHE limeripoti kuwa mmoja wa wanafunzi walioongoza darasa wa Taifa wa Darasa la saba mwaka huu mwenye umri wa miaka 16 anadaiwa kuozwa kwa mwanaume mwenye miaka 50 baada ya wazazi wake kupewa sukari kilo mbili kama mahari.Kutokana na hali hiyo mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu ukeketeji Mkoani Kilimanjaro NAFGEM umefanya jitihada za kumuokoa pamoja na wanafunzi wengine15 waliotaka kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa ngariba.


Msichana huyo wa miaka 16 wa kabila la kimasai ambaye jina lake limehifadhiwa baada ya kufaulu mtihani huo kwa asilimia kubwa huku akitajwa kuwa miongoni mwa wasichana waliofanya vizuri aliozeshwa kwa mwanaume mmoja ambaye ni mfugaji wa kabila hilo. 

Meneja Mpango wa mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu ukeketaji Mkoani Kilimanjaro Honoratha Nasua alitoa taarifa za kuolewa kwa binti huyo walizipatahuku wanafunzi wengine 15 wakisubiri tarehe ya kufanyiwa ukeketaji ili waozeshwe baada ya tendo hilo. 

Alisema suala la mwanafunzi huyo aliyeozeshwa limefikishwa katika dawati la jinsia la Polisi Wilayani Siha kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria. 

Alisema wazazi wa mwanafunzi huyo wamechangia kudidimiza maendeleo ya mtoto wao kwa kukubali aolewe na kubuni mbinu mpya ya kukeketa watoto wachanga ili kukwepa mkono wa dola na vyombo vya wanaharakati. 

Mtandao huo wa kupinga ukeketaji unaendelea na shughuli zake katika Wilaya hiyo ikishirikiana na Shirika la kimataifa la Elimu kwa ufadhili wa Shirika la misaada la kimataifa la Marekani USAID kupitia mpango wa pamoja wa TUWALEE!

HII SI YAKUKOSA SASA KWA WAKAZI WA MANISPAA YA IRINGA



HATIMAYE KWAYA YA ARISE YA PSA KUTOKA SHULE YA WASICHANA YA IRINGA  INATARAJIA KUZINDUA ALBAM YAO INAYO KWENDA KWA JINA LA HESHIMA NA UTUKUFU....GOSPEL ZA IRINGA ITAKULETEA MOJA KWA MOJA MATUKIO YA UZINDUZI HUO

MWIMBAJI ROSE MHANDO ASIMULIA ALIVYOTEKWA NA KULAZIMISHWA PENZI KWA BASTOLA


Nyota wa Nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando.
Stori: Erick Evarist na Imelda Mtema NYOTA wa Nyimbo za Injili Bongo,Rose Mhando (pichani)amefungukia eneo fupi la maisha yake magumu ambapo alisema amewahi kutekwa kwa bastola na mwanaume mmoja, akampeleka msituni ambako alimlazimisha kuwa naye kimapenzi lakini akadunda
 Rose alieleza kwa machungu kwamba, tukio hilo lilimkuta hivi karibuni mjini Dodoma ambako ndiko kwenye makazi yake ya kudumu.Ilikuwa ni katika mahojiano ya kukiri kwake (my confession) ambapo Rose aliweka bayana kuhusu mazingira ya tukio hilo la kushangaza.
MSIK
IE MWENYEWE
“Dunia ina mambo mengi sana ndugu zanguni, wengine wema, wengine waovu. Mimi nakumbuka siku moja kuna mwanaume ambaye nilikuwa na ukaribu naye.“Huyu bwana, ana jina kubwa sana Dodoma. Alinichukua kwenye gari kwa ajili ya kunisaidia mambo fulani maana alikuwa ananisaidia katika kazi zangu.
Bunduki, Mabomu pamoja na Magazine.
“Nilishangaa kumuona anapeleka gari nje ya mji,  nikamuuliza tunakwenda wapi, akasema tulia utajua.
“Sikuwa nimemuwazia ubaya, hivyo nilitulia lakini matokeo yake akanipeleka hadi porini ambako alikutana na watu wengine, naamini walikuwa wasaidizi wake.
“Naamini ulikuwa mpango kabambe. Wale watu wakaniweka chini ya ulinzi na kunifunga kamba kisha wakanioneshea mtutu wa bastola,” alisema Rose huku akisisitiza ni tukio ambalo hawezi kulisahau.
AAMBIWA KISA
Rose aliendelea kudai kuwa, mpaka hapo hakuwa amejua kisa lakini akiwa amekutana macho na mdomo wa bastola. Ndipo akaambiwa kuwa, anatakiwa kuwa chini ya himaya ya kimapenzi ya mwanaume huyo la sivyo siku zake zilikuwa zinahesabika.“Niliona ni jambo la ajabu, kwani mwanaume kumtaka mwanamke ni mpaka silaha na kutishia kuua?” alihoji staa huyo mkubwa wa gospo.
AKUBALI YAISHE
Rose aliendelea: “Kwa pale nilikubali kwamba niko tayari kuwa mtu wake lakini nikamwambia tukirudi mjini tukae tuongee kwa kirefu, akakubali.“Tulifika mjini nikiwa najisikia kuumwa sana maana wale wasaizidi wake walikuwa wakinisulubu kwa kunipigapiga pia ile kamba niliyofungwa ilichangia kunipa maumivu makali.”
Mfano wa Bastola iliyotumika.
AKACHA KUKUTANA
Rose alisema walipofika mjini walipanga kukutana baadaye ili wayaongee lakini yeye akakacha kutokea kwenye kikao, hivyo akaenda polisi (hakutaja kituo) ambako alifungua jalada la uchunguzi.“Nimekuwa nikisita kumwanika kwa jina huyo mwanaume kwani yupo na ni adui yangu mkubwa. Naishi kwa tahadhari kubwa sana, naamini siku nikimtaja ataniua.
“Mbaya zaidi najua mambo yake mengi, mabaya kwa mazuri lakini mabaya ni mengi sana kwani hata wakati ananisaidia kuhusu kazi zangu alinitenda maovu mengi, nimemwachia Mungu.”
KWA NINI AMEAMUA KUSEMA?
“Nimeamua kusema ili moyo wangu uwe mweupe, nimekuwa nikiwaza siku hadi siku kuhusu lile tukio, ni kumbukumbu mbaya sana kwangu, lakini kwa kukiri kwangu huku sasa nitakuwa na amani.”
Amani: “Polisi walichukua uamuzi gani?”
Rose: “Walisema wanafanya uchunguzi wa kina lakini sijawahi kuambiwa walifikia wapi!”
Amani: “Baada ya kuingia mitini jamaa hajawahi kukutumia meseji ya kukutishia maisha?”
Rose: “Hapana, alijua nimekwenda polisi.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime.
Amani: “Unadhani ni kwa nini alikuteka hadi msituni, kwa nini asikwambie tu kawaida mjini?”

Rose: “Alishawahi kuanza hizo dalili za kunitaka nikamwonesha sitaki, nilimwambia nataka kazi kwake na si mapenzi. Mimi najua fedha ndiyo jeuri yake.”              
Amani: “Ana familia?”
Rose: “Ana mke na watoto.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipotafutwa hakuweza kupatikana kuzungumzia ishu hiyo.

AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA KUKATWA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA




NA DENIS NYALI

IRINGA

Mtu mmoja amelipotiwa kufaliki dunia mkoani iringa huku wengine wakishikiliwa najeshi la polisi kwakukutwa na nyara za serikili

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo  kamanda wa polisi mkoani iringa ACP ramadhani mungi amesema kuwa tukio la kwanza limetokea katika kijiji cha lyamuko kilichipo kata ya boma la ng’ombe wilaya ya kilolo mkoani iringa.

 ambapo amemtaja mtu mmoja anaye fahamika kwa jina la pakton mgwilanga (80) mkulima mkazi wa kijiji cha lyamuko ameuwawa kwakukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji lake la uso na kukatwa kiganja cha mkono wake wa kulia.

Aidha  kamanda mungi amewataja watuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni mjuto mgwilanga (36) mtoto wa marehem na Erick mhenzi (25) mjukuu wa marehem  watuhumiwa wanatafutwa na jeshi la polisi huku chanzo cha tukio hilo kikiwa ni ugomvi wa mashamba.

 

Wakati huohuo askari wa  hifadhi wanyama pori ya ruaha wakiwa doria wamewakamata ADAM ISSA mkazi wa kihesa KENETH MZENGO (46) na EWALO NZABILO (28)wakiwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilo 3.5 watuhumiwa wamekamtwa


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

MMOJA AFARIKI DUNIA 28 WAJERUHIWA KWA AJALI MKOANI IRINGA


AJALI MBAYA YA ANOTHER G YAJERUHI 28, MAFINGA



MTU mmoja amefariki dunia na wengine 28 kuheruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya Mafinga, mjini Iringa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutangata kupita daladala na kugongana na fuso, katika eneo la Kisolanza, Wilayani Mufindi.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Ramadhani Mungi alisema tukio hilo limetokea leo, majira ya saa nne asubuhi, wakati basi hilo aina ya Another G, likisafiri kutoka mjini Iringa kwenda Mbeya.
Amemtaja aliyefariki kuwa ni utingo wa fuso, ambaye jina lake halijapatikana na kuwa majeruhi wane hali zao mbaya wamekimbizwa hospitali ya rufaa ya Mafinga.

SAKATA LA ESROW KUENDELEA TENA LEO

MBUNGE wa Mwibara (CCM), Alphaxard Kangi Lugola wakati akichangia katika Ripoti ya PAC kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow bungeni leo, ameomba kuchangia  akiwa amevaa 'Kininja' ili kutowaangalia usoni wahusika wa sakata hilo. 

Mbali na kuvaa hivyo, Lugola pia aliomba kama kanuni zinaruhusu achangie tena akiwa amevaa nguo za chama chake cha CCM ili kuonyesha kuwa CCM haiungi mkono vitendo viovu japo alikataliwa na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Zungu.


BON MWAITEGE AJA NA KITU KIPYA CHA DAKIKA 45 SOMA MWANANGU AKISHIRIKIANA NA BAHATI BUKUKU


Mwanzoni mwa wiki hili mwanamziki wa nyimbo za injili bon mwaitege amesikika redioni kuwa anatarajia kuja na ujio mpya baada ya kutamba na albamu ya mama ni mama sasa amekuja na wimbo ambao unajulikana kama {soma mwanangu} akiwa ameshirikiana na bahati bukuku,
akizungumza na gospel za iringa na habari bon amesema kuwa wimbo huo ambao umelenga zaidi kwa upande wa elimu ameuandaa ili watanzania hususa wanafunzi watambue umhimu wa elimu katika nyakati za sasa,
aidha bon amesema kuwa video ya wimbo huo inatarajia kukamilika ndani ya wiki mbili zijazo ikiwa na dk 45 hivyo wanainchi wajiandae kuipokea.

HATIMAYE MWIMBAJI NA MWALIMU WA KWAYA YA LULU GEOGY NJABILI AZIKWA LEO JIJINI MBEYA

Marehemu George 'Bonge' Njabili
Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Bima karibu na Shule ya St Mary's ambapo watu mbali mbali wanaweza kufika kutoa pole kwa familia ya Marehemu.

Ratiba ya kuuaga mwili itaanza kesho saa 4 kamili aubuhi nyumbani kwa marehemu hadi hapo itakapo ishia kisha msafara utaanza kuondoka kuelekea katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mtoni ambapo watu watapata nafasi ya kuaga tena kabla ya safari ya kuupeleka mwili Tukuyu, mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa mtoa ratiba, Benjamin Kihogo ambaye pia ni mwalimu wa kwaya ya Mtoni, ameeleza kwamba pia watu wanaweza kuchangia kwa kupitia namba ya kaka wa marehemu Tigopesa 0654 02 14 23 Mpesa 0754 46 41 02.
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/11/ratiba-ya-maazishi-ya-marehemu-george.html#sthash.HmUSumMi.dpuf
Na Joseph Msami,
GK Author.
Marehemu George bonge, Joseph Msami na Ritha Chuwalo.
Nimesikitishwa sana na msiba wa huyu mutumishi na rafiki yangu! Nilipomwona zaidi ya miaka kumi iliyopita nilimpenda na kumwomba awe rafiki yangu. Wakati huo hata simu za mikononi zilikuwa siyo nyingi akanipa no ya mezani ofisini kwake.
Niliwasiliana naye sana na hata mara nyingine nahisi nilikuwa namsumbua. Lakini nimejifunza sana unyenyekevu wake mkuu ambao siwezi kuusahau na namna alivyokuwa akimpokea mtu yeyote utadhani wanafahamiana naye kwa muda mrefu!

Imeniuma sana kumpoteza mtu huyu muhimu. Pia nimetiwa changamoto ya kujiandaa muda wowote (Zaburi119:1-5) ili andiko likitimia niwe tayari.

Natamani ningekuwa Dar nishuhudie safari ya mwisho ya rafiki yangu. Nawaombea sana hususani shemeji (mke wa George). Mungu hatawapungukia.
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/11/kwaheri-rafiki-george-nasi-tunafuatia.html#sthash.Ner8dmWg.dpuf
POLENI SANA NDUGU ZETU WA ARUSHA KWA AJALI MBAYA  ANGALIA PICHA HAPA
Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru. Akiongea na mwandishi wetu mmoja ya mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani -Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na lori hilo. Habari kamili zitawajia punde. 









NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog