LIVING WATER YAITEKA SHINYANGA

Huduma ya Living Water Centre Ministry chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi yenye makao yake makuu Kawe Jijini Dar es Salaam wikiendi iliyokwisha ilikuwa ikihitimisha mkutano wa Injili katika Kanisa lake Mkoani Shinyanga. 

Semina hiyo ilidumu kwa siku 5 na Apostle Ndegi aliyekaribishwa na mwenyeji wake Mch. Nazareth Manase wa Living Water Centre Shinyanga, Mkutano huo ulio uliohudhuriwa na watu wengi kutoka katika kila kona za mji wa shinyanga kuja kusikiliza Neno la Mungu. 

Katika Mkutano huo waimbaji wa Nyimbo za Injili kama Bahati Bukuku, Mwanakondoo Kwaya ambao ni wenyeji, St. Joseph Kwaya RC, Gosheni kwaya toka Mwanza na Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji walikuwepo kuhudumu, kitu kilichotokea kuhusu uwepo wa Masanja Mkandamizaji ni pale watu walipokuja kwa wingi kumuona Masanja lakini ndipo mahala Bwana Yesu alipo wakamatia na Kumpa maisha yao kuokoka.
Add caption

Kwa siku tano za mkutano huo waliokoka watu wengi wadogo kwa wakubwa, wake kwa waume Pia maombezi na ushauri vilifanyika katika wale waliokuwa wanahitaji msaada zaidi maana ilionekana kwa asilimia kubwa watu wengi wamevamiwa na nguvu za giza hasahasa watoto

MSIBA WA ASKOFU KULOLA KUWA EAGT TEMEKE, MWILI KUSAFIRISHWA MWANZA, FLORA MBASHA AZIMIA

Taarifa za mwendelezo kuhusu msiba wa Askofu Dr. Moses Kulola zinasema kuwa msiba utakuwa kanisa la EAGT Temeke kwa Mchungaji Ngowi, mahali ambapo kila mwaka amekuwa akifanya mkutano wa injili, na kwamba kwa wale ambao watapenda kuhudhuria wafike mahali hapo.
Mwili wa Askofu Kulola tayari umehamishwa kutoka hospitali ya AMI kwenda Hospitali ya Kumbukumbu ya Hurbet Kairuki iliyopo Mbezi jijini Dar. Mwili utasafirishwa kuelekea Mwanza, na mipango ya shughuli hiyo bado inafanyika.

Kwa mujibu wa Emmanuel Mbasha, mume wa Flora Mbasha (mjukuu wa marehemu Kulola) ameieleza Gospel Kitaa kuwa maandalizi bado yanaendelea na taarifa rasmi aitaendelea kutolewa kwa kadri ya muda unavyosonga.

Na taarifa ambazo zimefika hivi punde zinaeleza kuwa mjukuu wa Moses Kulola, Flora Mbasha, amezimia kwa muda sasa na anashughulikiwa na madaktari hospitalini, maombi yako yanahitajika ili apate kurejea kwenye hali ya kawaida.

Una habari kuwa Askofu Kulola hakuwahi kunyoa nywele tokea mwaka 1966? Bofya hapa ili kujua

AMBWENE MWASONGWE NA TUMSIFU RUFUTU, FREDY NDUMBALO KUITIKISA IRINGA WIKI HII

albamu mpya ya ambwene mwasongwe ambaye pia anatarajia kutikisa mji wa iringa wiki hii

     Tumsifu rufutu pichani akiimba wimbo wake wa mwambie farao katika moja kati ya mikutano yake.

Wiki hili kuanzia alhamisi wakazi wa iringa watapata baraka za mwaka kutoka kwa waimbaji wa injili ambwene mwasongwe pamoja na tumsifu katika kongamano la maombi na maombezi linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mwembetogwa manispaa ya iringa
mkutano huo unaosubiriwa kwa hamu mhubiri ni mtume na nabii ezekiel fungo kutoka jiji la mwanza ndiye atalkaye hubiri gospel za iringa itaendelea kukuhabarisha matukio yote

MASANJA AMPONGEZA MATUMAINI KUOKOKA AMTAKA KUFUMUA BREKI ZOTE ILI ASONGE MBELE


Masanja kushoto akiwa na pacha wake Silas Mbise.
Wiki moja tangu mchekeshaji maarufu nchini aitwaye Matumaini kutoa wimbo wake wa kwanza wa injili wa kumshukuru Mungu kwa kumponya na ugonjwa mbaya ambao ulimpata akiwa nchini Msumbiji, mchekeshaji mwenzake Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji amempongeza mwigizaji mwenzake huyo kusonga mbele na kutokatishwa tamaa na watu wengine juu ya uamuzi wake wa kumpa Kristo maisha yake.

Masanja amesema anajua Matumaini ametendewa jambo kubwa na Mungu la uponyaji wa afya yake na kumtaka kuendelea kung'ang'ania wokovu huo kwakuwa uamuzi wake si kutaka kufurahisha watu bali Mungu na kwamba watu wengi wataanza kumsema vibaya juu ya uamuzi huo, na kwambia kama ameamua kuokoka anatakiwa kufumua breki zote ambazo zitamzuia katika maisha yake ya wokovu. Masanja ameendelea kusema kwamba kumekuwa na wasanii wengi waliotangaza kuokoka lakini wakarudi nyuma, lakini ni maombi yake kuona Matumaini anasonga mbele na asubiri kuona baraka za Mungu juu ya maisha yake "jiandae kuolewa hata kama watu watasema hana umbo namba nane ataolewa tu na hao wenye namba nane watabaki wakishangaa, watu wakisema hutaolewa kwasababu ni mweusi wala usiwasikilize kwakuwa utaolewa na watabaki na weupe wao bila kuolewa.

 matumaini kikazi zaidi

MAKALA : SIZE 8 ALIKOSA AMANI MOYONI KUIMBA NYIMBO ZA KIDUNIA



Tarehe 12 April mwaka huu ilikuwa siku ya kipekee sana kwa wapenzi wa muziki wa gospel na wale ambao wameokoka baada ya mwimbaji maarufu aliyekuwa akitengeneza pesa nyingi na kupendwa na mashabiki wa muziki wa nje ya kanisa kuamua kumrudia Mungu wake na kutangaza kuachana na muziki huo aliokuwa akiufanya awali na kurudi kanisani.

Huyu si mwingine bali mwanadada Linet Munyeli ama mwite size 8 jina lake maarufu huyu ni mwimbaji wa gospel kutoka pale nchini Kenya, mwimbaji huyu aliyetamba na nyimbo mbalimbali nchini humo hasa wimbo unaojulikana uitwao vidonge.

Mapema mwaka huu aliamua kumpa Yesu maisha yake baada ya kuishi maisha yakutokuwa na furaha na amani kwa muda mrefu licha ya kuwa na vitu ambavyo watu hudhani ukiwa navyo umewezea maisha. Linet alikaririwa akisema kwamba licha ya kwamba alikuwa akipata fedha nyingi na kuwa na mashabiki wengi sana lakini moyo wake haukuwa na amani hata kidogo jambao ambalo lilikuwa likimuhuzunisha hivyo kuamua kumrudia muumba wake.




Linet ambaye ni mtoto wa sita katika familia yao ambayo wazazi wake wote ni wahubiri na kwamba katika muda wote aliokuwa akiimba mziki wa dunia mama yake alikuwa akimuombea kila siku ili abadilike na kumwimbia Mungu wake jambo ambalo liliwezekana na Mungu kumuokoa binti huyo mapema mwaka huu. Linet alisimama kwa muda kuimba muziki wa dunia kumbe wakati huo alikuwa anarekodi wimbo ambao unatamba kwasasa uitwao "Mateke" ambapo wakati wote wa kurekodi amesema alifanya siri kubwa ili watu wasijue ili ije kuwa kama kuwastukiza watu ambapo amesema alirekodi wimbo huo "Mateke" chini ya Jack B wa Tamu sana records kisha video yake akarekodi na Princecam media.

Kwa wakati wote huo aliweza kutunza siri hiyo ambayo haikuvuja mpaka pale wakati alioutaka yeye kuwaambia Wakenya na watu wengine kwamba yeye ameokoka, siku hiyo ndiyo ilikuwa tarehe 12 April 2013 siku ambayo ilitangazwa na DJ Mo wa NTV kwamba mwimbaji huyo ameachana na muziki wa kidunia kwasasa anaimba muziki wa injili akiwa na ushahidi pia wa wimbo huo wa "Mateke" ambao umemtambulisha vyema kwenye uimbaji wa kumsifu Mungu.

UTAJIRI WA DHULUMA NA KAFARA HAUNA BARAKA WALA AMANI

Askofu Paul Akyoo. picha kwa hisani ya elct.org
Askofu Paul Akyoo wa Dayosisi ya Meru kanisa la Kilutheri nchini amekemea vikali utajiri wa dhuluma na kafara kwakuwa hauna baraka. Askofu Akyoo ameyasema hayo hapo jana wakati wa ibada ya mazishi ya mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite jijini Arusha marehemu Erasto Msuya aliyefariki kwakupigwa risasi Agosti 7 mwaka huu.

Askofu Akyoo katika mahubiri yake alisema utajiri wa dhuluma na kafara hauna baraka wala amani kwa wahusika kutokana na dhamira zao kuwasuta kila wanapokumbuka uhalifu walioutenda. Aidha kwa upande wa mkuu wa mkoa Arusha Magesa Mulongo akisema “Waliomuua Msuya wataumbuka mchana kweupe wiki ijayo watakapofikishwa mahakamani. Nawahakikishia kuwa vyombo vya dola viko kazini na ukweli kuhusu waliohusika na tukio hili la kinyama utajulikana hadharani wiki ijayo wahusika watakapofikishwa mahakamani,” alisema Mulongo katika ibada hiyo.

WWI EAGT IRINGA WAPANIA KUFUNGUA BENKI YAO

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog