Makala Maalumu: kumbukumbu ya safari ya kundi la Christ ambassadors kutoka Rwanda kuja Tanzania na kuwapoteza wenzao watatu katika ajali ya Gari.
Ambassadors of
Christ Choir ni kwaya ambayo kwa sasa inafanya Vizuri sana na nyimbo zake
zimekuwa Gumzo hapa nchini. Kundi hili lenye maskani yake nchini Rwanda katika
jiji la Kigali hivi sasa limetimiza miezi takribani miwili tangu baadhi ya
wanakikundi hicho kufariki dunia tarehe 9/05/2011 walipokuja nchini kwa
mualiko wa kwaya ya Acasia Mwenge SDA ya jijini Da es salaam.
Baada ya kupata
Mualiko huo, tarehe 5/05/2011 Kundi hilo lilianza safari ya kuja jijini Dar es
salaam kwa ajili ya Uzinduzi wa DVD ya kwaya ya Acasia ambao ulipangwa
kufanyika katika ukumbi wa PTA ulio katika viwanja vya Sabasaba jijini Dr es
salaam.
Ambassadors of Christ walifanikiwa kufika Dar es salaam tarehe
6/05/2011. Kundi hili liliweza kushiriki ibada ya sabato siku ya jumamsi ya
tarehe 7/5/2011 na lilialikwa katika Interview katika kituo cha Redio cha
Morning Star Adventist Radio of Tanzania kilichoko jijini Dar-es salaam
kwenye kipindi kiitwacho “LULU ZA INJILI” ambacho hungozwa na Bro
Emmanuel Maduhu.
Wakiwa Redioni hapo, kundi hili lilivutia
wasikilizaji wengi hasa kwa uwezo wao wa kuimba Live. Tarehe 8/05/2011 ndio
siku iliyokuwa ikisubiriwa kwani ilikuwa siku Maalumu kwa kwaya ya Acasia
Mwenge SDA Kufanya uzinduzi wa dvd yao
ya Pili iitwayo “MNAZARAYO” katika ukumbi wa PTA.
Kundi hilo
likiimba wakati wa uzinduzi wa dvd ya acasia choir katika ukumbi wa PTA
jijini Dar es salaam
|
Watu kutoka kona tofauti tofauti za jijini
Dar walifurika kutaka kuwaona vijana hawa Live wakiwa jukwaani wakimtukuza
Mungu. Muda uliwadia na ndipo vikundi mbalimbali vya injili vilitangulia kuimba
wakiwemo Voice of Victory wakifuatiwa na Triumph Generation pamoja na
Harvesters vyote vya jijini Dar es salaam.
Muda uliwadia ambapo ukumbi mzima ulizizima
kwa furaha na vifijo pindi Ambassadors of Christ walipotajwa kuwa ndio
wanafuata kupanda jukwaani. Taratibu huku ala ya nyimbo yao maarufu iitwayo Twapaona vijana hawa walipanda jukwani na ukumbi mzima ulizidi
kupiga kelele za furaha.
Miongoni mwa nyimbo ambazo Ambassadors of
Christ walizimba Live siku hiyo ni pamoja na Kazi Tufanye, Yesu Ndiye Njia, Twapaona, Kuna Siku, Huyo ni Yesu, pamoja
na nyimbo yao
maarufu iitwayo Kwetu Pazuri. Watu wote waliofika ukumbini hapo walibarikiwa na kazi za kundi hili kwa
utukufu wa Mungu.
Kuhusu Ajali
Baada ya
kumaliza huduma tarehe 8/05/2011, kundi zima la Ambassadors of Christ lilianza
safari ya kurudi Kigali asubuhi ya tarehe 9/05/2011 kwa njia ya basi. Walipofika
Wilaya ya Kahama mkoani shinyanga mnamo saa tatu usiku walikutana na Lorry
likiwa limepaki barabarani likiwa halina reflector yeyote. Dreva wa gari la
kundi hilo hakuweza kulina lorry hilo na pindi alipoliona na kutaka
kuliovatake ndipo lorry lingine lilikuwa likija kwa kasi hivyo wakakutana
uso kwa uso na ajali ikatokea.
Baada ya ajali
hiyo iliyotokea kilometa kadhaa kabla ya kufika Rwanda, wanakwaya watatu
wa kundi hil Filbert Manzi, Gatare Ephraim
pamoja na mtanzania Amos Fares
ambaye nayee ni muimbaji wakundi hilo aliyekuwa mbele akielekeza njia
walifariki papo hapo.
Muda mfupi
baada ya ajali hiyo kutokea serikali ya Rwanda ilituma Helkopta ya Jeshi la
ulinzi la nchi hiyo [RDF] pamoja na Ambulance mbili kwa ajili ya kusafirishia
wagonjwa kutoka Kahama kwenda Hospitali ya Mkoa wa shinyanga. Baada ya kufika
Hospitali ya shinyanga wahanga hao waliweza kupata huduma ya kwanza na hatimaye
walikimbizwa nchini Rwanda katika Hospitali iitwayo King Faisal kwa matibanu
zaidi.
Kwa msaada wa
Mungu majeruhi wane wa ajali hiyo walipata nafuu na hatimaye kurutuhusiwa
kutoka Hospitali. Taratibu za mazishi zilifanywa ambapo Marehemu Filbert Manzi
aliyekuwa mmoja wa vingozi wa kwaya hiy na pia mtangazaji wa kitu kimoja cha
Redio nchini Rwanda, pamoja na Gatare Efraimu ambaye alikuwa ni muanzilishi na kiongozi wa kwaya hiyo
wa walizikiwa nchini Rwanda, wakati Mtanzania Amos Fares yeye alizikiwa
nyumbani kwao mkoani Kigoma.
Zifuatazo ni
baadhi ya matukio ya kundi hilo wakati wakiimba jijini Dar na baada ya ajali
hiyo.
Majeruhi
Waliotangulia
Hili ndio kava la Album yao ambapo kushoto
mstari wa juu vijana hao watatu Ephraim, Filbert, na Mtanzania Amos hawako
nasi tena
|
Mungu anabaki kuwa Mungu kwa lolote
afanyalo juu yetu kwa ajili ya Utukufu wake
Hii ni kazi yao iitwayo NI VEMA ambayo inafanya Vizuri sana hapa nchini
Hii ni kazi yao iitwayo NI VEMA ambayo inafanya Vizuri sana hapa nchini
0 comments:
Post a Comment