Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa |
=====================================
Na Gustav Chahe, Iringa
RAIS wa Baraza la Maakofu
Tanzania (TEC) Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka waamini
wakristo kutokuwa na moyo wa kuhamaki kutokana na kitendo kilipuliwa Kanisa
Katoliki huko Arusha.
Amezungumza hayo katika mahojiano
maalum mtandao huu wa www.matukiodaima.com mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake Iringa juu ya vitendo vinanyoendelea
kutokea nchini vikiwemo vya kuchomwa makanisa na kuuawa wachungaji wa kiroho
huku vikihusishwa na imani za kidini.
Amesema kama ilivyoutamaduni wa
Kikristo, yanapotukia matukio ya kusikitisha kama hayo silaha iliyo kubwa ni
sala kumuomba Mungu atoe jibu kwa wanaohusika na mateso kama
hayo.
“Kasi ya sala iendelee, ili Mungu
wetu wa Amani ajenge fikira za upendo na haki katika mioyo yetu” alisema.
Amesema waamini wasikate tamaa na
kuacha kusali kwa kuwa Mungu ndiye mwenye jibu na atatoa majibu kadiri atakavyo
kwa wale wote wanaowatesa wenzao kwa sababu zao binafsi.
Hata hivyo alisema licha ya kuwa
kila mtu amepokea kwa mshituko na maumivu makubwa, roho za watu zinazoteswa na
wengine Mungu atazifariji na kuziponya lakini mtesaji atapata majibu yake.
Alisema waliopoteza maisha katika
mlipuko huo Mungu atawarehemu na kuwafariji majeruhi wote.
“Waliopoteza maisha wapokee Rehema
ya Mungu na waliojeruhiwa wafarijiwe na uwezo wa Mungu” alisema.
Hali kadhalika amesema upendo na haki
ni zawadi kutoka kwa Mungu na hivyo, anayedhurumu wengine zawadi hiyo atapata pigo
kubwa.
Aidha amesema wakati uliopo sasa ni
wakutafakari na kumkabidhi Mungu yale yote yanayowasumbua wanadamu na kuongeza nguvu
ya sala ili majibu ya Mungu yapatikane kwao.
“Tulieni na kufanya tafakari kasha
mwambie Mungu hayo yote ayafanyie kazi kwa uweza wake. Sisi binadamu tunategemea
nguvu kutoka kwake” alisema.
0 comments:
Post a Comment