Home » » BON MWAITEGE NAFURAHI KUWA NA MATUNDA YANGU

BON MWAITEGE NAFURAHI KUWA NA MATUNDA YANGU

  



Mwimbaji wa nyimbo za injili bon mwaitege amesemakuwa hana ugomvi na waimbaji chipukizi wanaotamani kuwa kama yeye katika huduma ya uimbaji.

Akizungumza na overcomers fm katika kipind cha overcomers show kinachoendeshwa na mtangazaji denis nyali katika kipengele cha  ;Tripple stage;  bon amesema´’mimi nashukuru kama kuna watu wananikubali na kufanya kama mimi na hatakama watafanya vizuri kwangu itakuwa ni furaha kwani yatakuwa ni matunda yangu,unajua mtangazaji mziki hauna mwenye nao kwa sababu majitaa yanayotumika ni yaleyale na vinanda ni vilevile kwa hiyo kuigana kwa beat au wimbo ni kitu ambacho hakiwezikukwepeka mbona watu wanaiga sauti za watu mbalimbali kama vile kikwete nyerere na viongozi wengine kwahiyo mimi watu kuniiga namshukuru mungu kwa hilo pia,;  alisema bon

Hata hivyo mwaitege amewaomba wapenzi wa mziki wa injili kuwa wengi wanasema yupo kimya lakini anajipanga kuja kivingine na anatarajia mwezi wa tano au wa sita kuachia albam yake ya tatu huku albam yake ya mama ni mama na utanitambuaje zikiendelea bado kufanya vizuri.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog