mchakato wa kutafuta vipaji katika mkoa wa iringa maalufu kama holly search umeanza leo huku washiriki wakiwa na hamu kubwa ya kuwania zawadi mbalimbali kama vile kurekodi albamu pamoja na singo au wimbo mmoja
zifuatazo ni baadhi ya picha za washiriki katika holly gospel search iringa
jane kalinga akisikiliza kwa makini maneno kutoka kwa majaji hawapo pichani
Opeki Peter akimsifu Mungu
Daudi akiimba kwa hisia wakati wa ufunguzi wa shindano hilo
denis nyali
Katika kuhakikisha vijana wanasaidiwa kutoka katika hali duni za kimaisha mkurugenzi wa jesus my life band bi.kazinyolo ameandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji ambayo yameanza leo kwa usail na kuanza lasmi ni tare 16march 2013 ambapo zaidi ya vijana 30 wamejitokeza kuwania nafasi mbali mbali siku ya leo
Akizungumza na mtandao huu amesema kuwa lengo la kuandaa shindano hilo sio kuibua vipaji pekee bali ni kuwafanya vijana waweze kuhubiri zaidi kupitia uimbaji kwani kuna shuhuda mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kuhusu watu kuokolewa kwa njia ya uimbaji
kwa upande wa washiriki wamemshukuru mkurugenzi huyo kwa kutambua kuwa kuna watu wamesahaulika na kujiingiza katika matendo maovu ambayo yangesababisha kuongezeka kwa maambukizi ya vvu
mashindano hayo yanatarajia kuenderea jumamosi ijayo tare 16.march 2013