HAYA SASA WAPENZI WA MZIKI WA GOSPEL HHEBU SASA MFAHAMU HUYU

Solomon ambaye pia ni mchungaji anasema kuwa kipaji chake amepewa na Mungu japo anaweka na jitihada zake binafsi. 
Nyimbo zake nyingi anajifunza kutoka kwa waimbaji wa injili Tanzania kwani wana nafasi ya kwanza katika soko la muziki huo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Solomon mwenye asili ya DRC akitokea Goma Mashariki mwa mji huo akizaliwa katika familia ya kumjua Mungu japo anasema kuwa baba yake alikuwa na wake wawili. 
Anasema kuwa aliondoka nchini Congo na kuachana na wazazi wake mwaka 2003 ambapo alielekea nchini Uganda na kukaa kwa miaka mitatu na nusu ndipo alipokutana na marehemu Angela Chibalonza aliyemuwezesha na kumpokea Nairobi nchini Kenya. 
“Angela Chibalonza ndiye aliyefungua njia katika maisha yangu ya uimbaji japo wakati nakutana nae nilikuwa katika harakati za kurekodi albamu yangu ya Sijaona rafiki kama Yesu, nimesalia sana katika kanisa la Chibalonza mpaka mauti yanamkuta na siwezi kumsahau ameninyanyua,” anasema. 
Mwimbaji huyo mwenye ndoto nyingi ikiwemo ya kutaka kufungua kituo cha watoto yatima nchini Tanzania anasema kuwa anaipenda sana nchi hii na ndio sababu ya kutoa misaada mara kwa mara. 
“Watanzania hawana mioyo ya kinafiki, ni wakarimu, wacheshi na wenye upendo ndio sababu mimi napenda kuwa Tanzania na kutoa misada ikiwemo kuweka kituo cha kulea watoto yatima” anasema Solomon. 
Solomon Mukubwa anasema akiwa na miaka 12, alipata matatizo ya uvimbe katika mkono wake wa kushoto. 
“Uvimbe huo ulikuwa wa ajabu sana na hakuna aliyefahamu chanzo kilikuwa ni nini? Niliugua kwa muda wa miaka mitatu,”anasema solomon. 
 
Muimbaji huyo anasema wazazi wake walihangaika kumpeleka kwa wataalam wa hospitali mbalimbali na hata kwa waganga wa kienyeji bila mafanikio, na anasema kuwa baada ya muda huo kupita ilianzishwa hospitali moja na Wazungu karibu na nyumbani kwao, na ndipo wataalam wa hapo waliposhindwa na kushauri akatwe mkono kwa lengo la kunusuru uhai wake. 
Solomon anasema ugonjwa wa mkono wake ulitokana na mama yake wa kambo kuwachukia yeye na ndugu zake ndipo mama huyo alitaka kuwaua. 
“Mkono wangu ulivimba sana na baadae ukaoza hiyo ndio sababu ya kukatwa mkono wangu, unajua shetani ni mjinga sana alinitesa kwa miaka mitatu ndiyo sababu ya kuimba wimbo wa Mungu mwenye nguvu,” anasema.
 
 Solomoni aliendelea kusema kuwa hakuna mtu aliyejua kuwa uvimbe huo umetokana na nini lakini hapo baadae ilidhihirika wazi kuwa mama yake wa kambo ndie aliyemroga na kumsababishia tatizo hilo kwani baadae alikuja kukiri na kueleza ukweli. 
Solomoni ambaye kwa sasa maskani yake yapo jiji la Nairobi nchini Kenya anasema wimbo wake wa Mfalme wa Amani aliutunga ili kumtukuza Mungu baada ya kumuepusha na kifo ambacho kingempata baada ya mama yake wa kambo kumroga na kusababisha mkono wake kuvimba na kutibiwa na madaktari bingwa bila mafanikio na hata alipoenda kwa waganga wa kienyeji pia hakupona. 
“Wimbo wangu wa Mfalme wa amani niliamua kuuimba baada kuvuka katika shida hizo na albamu yangu kuipa jina la Mungu mwenye nguvu, na kuna maneno niliweka kwenye kibao hicho kwamba, ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia, mwite mfalme wa amani, yeye anajibu maombi,” anaeleza Solomoni Mukubwa. 
 
 Baada ya kupona mkono wangu, mama yangu wa kambo alikiri kunifanyia kitendo hicho, lakini mimi nilipookoka nilimsamehe, baada ya muda mfupi naye aliokoka kutokana na pigo kali alilopata kwani mwanaye aliumia jicho alipokuwa anachezea chelewa kwenye moto ambalo uliruka na kuharibu kabisa jicho lake,”anasema. 
Solomoni Mukubwa ambaye ni moja ya waimbaji maarufu wa muziki wa injili Afrika ya Mashariki na Kati alizaliwa miaka 33 iliyopita na ameoa, anasema kuwa anaililia nchi yake na hasa eneo analotoka ndio maana amepanga kwenda kuhubiri ili vita iishe.
“Nawaomba viongozi wa nchi yangu wakae waone ni jinsi gani watasuluhisha na kuwasaidia watu wangu wa Kongo hasa Goma ambako kuna machafuko,”anasema. 
Akizungumzia muziki wa injili kutumika kama biashara anaeleza kuwa huduma ya injili ni kazi kama kazi nyingine lakini cha muhimu ni mtu atawale fedha sio fedha zimtawale. 
Anaeleza pia kuingia studio kunahitaji fedha ila fedha haziwezi kumtenga mtu na Mungu nivema watu wakatambua kuwa muziki wa injili ni ajira tosha kabisa na kusema kuwa kwakwe yeye akipata mahitaji ya muhimu inatosha kabisa kumtumikia Mungu. 
Solomoni ana albamu mbili ambazo ni ‘Sijaona Rafiki, ‘Mungu mwenye nguvu’ na ‘Kwa utukufu wa Mungu.’
 
 

HABARI ZAIDI ZA PADRI ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR USIKU WA JANA


HABARI ZAIDI ZA PADRI ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR USIKU WA JANA

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema Father amepigwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wahusika walifanya uhalifu huo kwa madhumuni gani kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Sisi tunahesabu kuwa kitendo hiki ni kitendo cha kihalifu na tunawatafuta wahalifu waliofanya kitendo hiki kwa hivyo bado ni mapema kusema kwamba kitendo hiki kimefanywa na nani kwa kuwa bado uchunguzi wetu unaendelea na hadi sasa hakuna mtu tuliyemshika kuhusikana na tukio hili” alisema Kamanda.



Kamanda Aziz akisimulia tukio hilo alisema walipata taarifa majira ya saa 2 na kwenda katika eneo la tukio ambapo Father alikuwa akitokea kanisani na kutaka kuelekea nyumbani kwake wakati akiwa ndani ya gari ndipo aliposhambuliwa na watu wasiojulikana na kuanguka.

“Tumekuta mabaki ya risasi ndani ya gari yake na katika vioo vyake vya gari vimevunjika na tumekuta damu chini pale” alisema Kamanda.

Aidha Kamanda Azizi alisema Father Ambros yeye ni mhasibu pale kanisani na hivyo mara nyingi watu wananaamini kwamba katika siku za krismass mara nyingi sadaka hukusanywa fedha nyingi na hivyo wanamini kwamba alikuwa fedha mikononi na ndipo inawezekana waliamua kumpiga risasi wakitaka kuchukua fedha hizo.

Hata hivyo alisema uchunguzi wa awali ndio utakaoeleza ni suala gani lililopelekea kupigwa risasi lakini wanaendelea na uchunguzi huo ambapo uchunguzi ndio utakaojulikana sababu kamili ya tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan la Mkunazini amesema wamesikitishwa na wamepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo hasa kwa kuzingatia matukio kama hayo hayajawahi kutokea ya kuwahujumu viongozi wa dini.


Alisema tukio hilo ni miongoni mwa matukio ya kushtusha na yanaashiria hali mbaya ya kiusalama na kuwaomba viongozi wa serikali kuchukua hatua za tahadhari kubwa kwani matukio kama hayo yameanza kutokea kwa viongozi wa dini ambapo mwanzo ilianzia kwa Sheikh Soraga na baadae kutokea kwa Father Ambros.

“ Hii ni hali ya hatari katika nchi yetu na haipendezi lakini serikali lazima ijue sisi hatuwezi kujua wala hatuwezi kujilinda lakini serikali inapaswa kutulinda sisi ndio wananchi wake” alisema Askofu Hafidh.

MAMIA WAMIMINIKA KATIKA KONGAMANO LA MAOMBI NA MAOMBEZI KWA KATUNZI

Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake wanamiminika katika kongamano kubwa la maombi na maombezi lililoandaliwa na kanisa la E.A.G.T City Centre chini ya mchungaji wake kiongozi Florian Katunzi katika ukumbi wa PTA uliopo viwanja vya mwalimu JK Nyerere zamani Sabasaba.

Kongamano hilo la siku nane lililoanza siku ya jumapili nakutarajiwa kumalizika jumapili hii linatarajia kupambwa na waimbaji mbalimbali wa gospel nchini wakiongozwa na Bahati Bukuku, Masanja Mkandamizaji, Flora Mbasha, Martha Mwaipaja, Solomon Mukubwa, Madam Ruti, Bonny Mwaitege na waimbaji wengine lukuki zikiwemo kwaya za kanisa hilo.

Ambapo toka jumapili tayari uwepo wa Mungu umeanza kujidhihirisha ukumbini hapo kwa watu mbalimbali kupokea uponyaji na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali vya ibilisi ambapo kwa watu wasiofika katika ukumbi huo wanapata yanayojiri kwakusikiliza Wapo Radio FM inayorusha matangazo ya moja kwa moja kutoka ukumbini hapo.

  CHEKI BAADHI YA PICHA KUTOKA KATIKA KONGAMANO HILO TOKA LILIPOANZA.
Mchungaji Florian Katunzi akiwaongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar katika maombi.
Solomon Mukubwa kutoka Kenya akiita uwepo wa Mungu katika kongamano hilo.

Martha Mwaipaja wa John Saidi akimtukuza Mungu.
Solomon Mukubwa akimpiga picha Martha Mwaipaja wakati akiimba.
Picha ya Juu ni Waimbaji Madam Ruth pamoja na Martha Mwaipaja wakiwa na Solomoni Mukubwa kwa Pamoja wakimsikiliza Mtumishi wa Mungu wa Mungu Mchungaji Frolian Katunzi wakati akitamka Neno la Baraka kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Mchungaji mtarajiwa a.k.a Masanja Mkandamizaji akipiga gombo la uimbaji katika kongamano hilo.
Sio utangazaji tu hata uimbaji ni balaa, anaitwa Silas Mbise ambaye pia ni mtangazaji wa Wapo Radio Fm akimtukuza Mungu katika kongamano hilo,
Flora Mbasha na mumewe mpenzi Emanuel Mbasha wakimsifu Mungu kwa pamoja.
Eveline Msoome nayeye hakuwa mbali katika kumsifu Mungu.
Kijana mwenye mavocal Samuel Limbu akimsifu Mungu katika kongamano hilo.
Mchungaji Yohana Mwegoha akimsifu Mungu. picha kwa hisani ya Yonathanlanda.blogspot.com

MAMA AMCHOMA MTOTO MOTO NA KUMLISHA KINYESI CHA MAMA MDOGO WAKE

 mtoto anety akionesha jeraha alilounguzwa na mama yake

 mama ambaye jina lake halikufahamika akiwa amembeba mtoto tayari kwa kumpeleka hospitalini
MTOTO aliyejulikana kwa jina moja la Aneth (pichani) anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili, mkazi wa eneo la Majengo Kaskazini jijini Mbeya ameunguzwa vibaya mwili wake na kulazimishwa kula kinyesi na Mama yake Mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Revina.

Tukio hilo la kikatili liligundulika jana eneo hilo majira ya saa tano asubuhi ambapo mwandishi wa habari hizi alifika eneo la tukio na kuukuta umati wa watu na mtuhumiwa akimuogesha mtoto huyo.

Mtoto huyo alipoulizwa kuwa ilikuwaje, aliongea kwa woga akisema kuwa alikuwa amefungwa mkono na kumwagiwa maji na kupigwa.

Mtuhumiwa huyo alipohojiwa alikataa kusema chochote na kuishia kutaja jina lake moja la Revina, kisha wananchi wakaamua kumchukua mtoto huyo na mtuhumiwa na kuwapeleka kituo cha Polisi cha Kati.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa baada ya kutomuona mtoto huyo mwenye historia ya kuteswa na mama yake huyo mdogo anayeelezwa kuwa mama yake mzazi, Bahati Mkandara alifariki, wakaamua kumuuliza binti huyo ambapo aliwajibu kuwa mtoto huyo alikuwa kucheza na walipompiga ndipo akaamua kukimbilia chumbani na walipoingia wakamkuta mtoto amesimama akiwa uchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti  wa Mtaa wa Majengo Kaskazini, Shack Mwakanyamale alisema kuwa binti huyo amezoea kumtesa mtoto huyo huku mtoto wake akiwa na afya njema ambapo aliwatuliza wananchi wenye hasira kali na kuongoza msafara wa kumpeleka katika kituo cha polisi mtuhumiwa huyo

HAKIKA KUMTEGEMEA MUNGU INALIPA


 HEBU MWANGALIE MWIGIZAJI MFILIPINO AMBAYE NI MTU ANAYE MJUA MUNGU KWELIKWELI

Mwigizaji huyu ni kati ya waigizaji wanaompenda Mungu ambapo mpaka sasa bado yupo katika ndoa yake na mkewe mpenzi Glydel Mercado ambaye pia ni mwigizaji, kabla ya ndoa uhusiano wao ulidumu miaka 6 kisha alimvalisha pete ya uchumba mkewe baadaye ndani ya miezi 2 aliweza kufunga naye ndoa. Wasimamizi wao ni marafiki wao wakubwa mwanamama Lorna Tolentino (Red Butterfly) pamoja na marehemu mumewe Rudy Hernandez. Mwigizaji huyu ametoka katika familia ya wasanii baba yake mzazi Eddie Gutierrez na mama yake pamoja na ndugu zake waigizaji kama yeye.











Msanii Lorna Tolention(Red Butterfly) wa kwanza baada ya bibi harusi, pamoja na marehemu mumewe baada ya Eduardo bwana Rudy Hernandez walikuwa ndio wasimamizi wa harusi hiyo.



                                

PADRI AFARIKI BAHARINI WAKATI AKIOGELEA



Mkuu wa Shirika la Kitawa la Consolata la Kanisa Katoliki nchini, Padri Salutaris Massawe (pichani) amefariki Dunia baada ya kuzidiwa na maji ya Bahari wakati akiogelea katika ufukwe wa Pwani ya Bagamoyo Oktoba 25.


Padre huyo ambaye alikuwa yupo Bagamoyo kwa shughuli za shirika lake, alizidiwa na maji hayo ambayo yalimchukua majira ya alasili ya siku hiyo wakati alipokuwa akiogelea pamoja na wageni wa shirika hilo walioitembelea Bagamoyo. 


Mwili wa Marehemu Padri Salutaris Massawe ulipatikana jana asubuhi katika fukwe hiyo ya Bagamoyo.
Akizungumzia tukio hilo mbele ya Ripota Wetu, Katibu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Joseph Masenge alikiri kutokea kwa kifo cha Padri huyo, ambapo padri huyo alifariki baada ya kuchukuliwa na maji alipokuwa akiogelea juzi saa tisa alasiri (kwa saa za Afrika Mashariki) na mwili wake kuonekana jana asubuhi ufukweni.


Padri huyo alikuwa akiogelea baharini karibu na Msalaba Mkuu wa Bagamoyo
Hadi jana mchana Padri Masenge alisema walikuwa katika maandalizi ya kuusafirisha mwili wa Padri Salutaris Massawe kuja Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuuhifadhi wakati mipango ya mazishi ikiandaliwa.


Naye, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Eusebius Nzigirwa alisema kifo cha padri huyo kimeacha pengo kubwa kwani wamepoteza mtu mchapakazi na aliyefanya kazi kwa mipango.
Alisema anamfahamu Padri Massawe kwani aliwahi kufanya kazi katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam kabla ya kuchaguliwa kuwa Mkuu wa shirika hilo ambapo aliwajibika vizuri katika kusimamia majukumu yake.


Alisema kwa taarifa alizozipata awali, Padri huyo alikwenda Bagamoyo na wageni wa shirika ambao walitaka kupata historia ya jinsi Ukristo ulivyoingia nchini pamoja na historia nzima ya Ukristo.

ASKOFU MKUU WA TANZANIA ASSEMBLIS AZINDUA MAABARA YA KISASA KATIKA SHULE YA SEMINARY EBENEZER MKOANI IRINGA

Wito umetolelewa kwa wanafunzi wanao hitimu kidato cha nne hapa nchini kuweza kuendeleza nidhamu zao hata baada ya kuhitimu kwani hiyo ndo njia pekee itakayowawezesha wanafunzi kufaulu na kukamilisha malengo yao ya hapo baadae.

Wito huo umetolewa na Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania assemblia of god   Dr Barnabas Mtokambali katika mahafali ya tatu ya kidato cha nne ya shule ya seminary ebenezer iliyopo nduli jirani na uwanja wa ndege manispaa ya iringa.

Ambapo mbali na maafari hayo Askofu Mtokambali aliweza kuzindua rasmi maabara ya kisasa itakayo wasaidia wanafunzi wote wanaosoma masomo ya sayansi Mtokambali alisema iwapo wanafunzi watafuata nidhamu waliyofundishwa na kuionyesha  katika jamii zao hakika hakutakuwa na mwanafunzi wa kufeli hata mmoja kwa anaamini kuwa nidhamu ndio chanzo kikuu cha mafanikio.

Hata hivo alimpongeza mwalimu mkuu wa shule hiyo bw.makweta na kuaahidi kusaidiana katikachanga moto mbalimbali zinazohusu shule hiyo kama tatizo la maji ambapo askofu mkuu aliahidi million mbili katika kufanikisha na kutatua jambo hilo, na zaidi ya millioni sita zilichangiashwa katika kutatua sual;a la maji .

Kwa upande wake  mkuu wa shule ya ebenezer alimpongeza askofu mkuu pamja na uongozi wa jimbo  la iringa uliongozwa na Askofu Jonas Mkane pamoja na makamu wake Edward Tom Matipa kwa uwepo wao katika kufanikisha zoezi zima la mahaafari pamoja na uzinduzi wa maabara ya kisasa kwa wanafunzi wa shule hiyo.




Askofu mkuu wa tanzania assemblis of god wakati akiwasili katika shule ya ebenezer




Askofu mkuu wakati akizindua rasmi maabara ya kisasa


Asikofu  wa jimbo la iringa jonas mkane akifungua kwa maombi sherehe


makamu askofu wa jimbo la iringa rev edward tom matipa




baadhi ya majengo ya shule ya ebenezer seminary

wahitimu wakicheza kwaito kwa pamoja



KANISA LA BETHEL PENTECOSTE BUZA NALO LAPATA KISANGA CHA MOTO

Wakati jeshi la polisi na lile la wananchi (JWTZ) waliweza kutuliza hali ya uvunjifu wa amani ikiwa pamoja na maandamano yaliyokuwa yamepengwa kufanywa na waumini wa dini ya kiislamu kuelekea ikulu ili kushinikiza kuachiwa huru kwa sheikh Ponda Issa Ponda na waumini wengine wa dini hiyo waliokamatwa kwa tuhuma za kuchochea vurugu za kidini nchini.

Huko Buza njia panda ya kuelekea Kitunda jijini Dar es salaam, watu wasiofahamika wamelichoma moto upande mmoja kanisa la Bethel Pentecoste linaloongozwa na mchungaji Emanuel Kapama majira ya usiku wakati waumini wakiwa tayari majumbani mwao.

Kwa mujibu wa mchungaji Kapama amesema jana walikuwa na ibada kuanzia majira ya saa 1 usiku hadi saa 2 kisha kutawanyika lakini waliporejea asubuhi wakashangaa kukuta kanisa lao limechomwa moto upande mmoja na kukuta chupa ya mafuta ya taa ambayo imechukuliwa na jeshi la polisi kwa  ushahidi ikiwa ndani ya kanisa hilo huku watu hao wakiwa wameshamwaga mafuta ya taa kanisa zima ambalo limezungushiwa kwa mabati pamoja na mifuko migumu aina ya viroba.

Ambapo kwa mujibu wa mchungaji huyo amesema jeshi la polisi tayari limefika na kuangalia kilichotokea na kuchukua vitu ambavyo vitatumika kwa ushahidi ikiwemo chupa hiyo ya mafuta ya taa.
Moja ya kanisa lililochomwa moto huko mkoani Kigoma wiki hii. picha by Fungo Omary.

MAKANISA 2 YOMBO NUSURA KUCHOMWA MOTO, MAASKOFU LUTHERAN WATOA SALAMU JUU YA VITENDO HIVYO

Watu wasiofahamika usiku wa kuamkia leo wamevamia kanisa la kilutheri Yombo jijini Dar es salaam kwa lengo la kufanya uharibifu kanisani hapo majira ya saa 9 kasoro za usiku lakini walinzi wa kanisa hao walifanikiwa kuzuia zoezi lao hilo.

Kwa mujibu wa mmoja wa watu waliofika kutoa msaada baada ya walinzi hao kugonga kengele iliyowaamsha wakazi wa eneo hilo ambaye pia husaidia kazi ya ulinzi kanisani hapo bwana Hosea Mbwambo amesema vijana wapatao saba waliingia kanisani humo kwa kuruka ukuta kwa nia ya kwenda madhabahuni lakini mlinzi aliyekuwepo aliwaambia mnataka nini ndipo walipomfuata nakusema kwamba tunakutaka wewe nakuanza kumpiga kabla mlinzi mwingine aliyekuwepo gorofani kushuka ili kusaidia ndipo vijana hao wakagundua kwamba kuna walinzi wengi hivyo kuamua kutimua mbio lakini wakiwa wamemuachia jeraha mlinzi Nkya ambaye alipelekwa hospitali ya Buguruni kisha Amana kwa matibabu zaidi hali yake inaendelea vizuri pia ulinzi ukiwa umeimarishwa kanisani hapo.


Pia habari ambazo GK imezipata kutoka kwa chanzo kingine cha habari ikiwemo Wapo Radio Fm inasema kwamba watu wasiofahamika waliwasha moto katika kanisa la Faraja International Gospel lililoko huko huko Kiwalani ingawa watu waliweza kuudhibiti baadaye. Wakati huo huo maaskofu wapatao 20 wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT) wakiongozwa na mkuu wa kanisa hilo Dkt. Alex Gehaz Malasusa, wamekutana hii leo katika kanisa lililofanyiwa uharibifu la Mbagala na kutoa tamko zito juu ya vitendo vilivyofanywa na waumini wa dini ya kiislamu dhidi ya makanisa ya eneo hilo.








Baadhi ya picha za tukio la leo huko Mbagala kama zilivyotolewa na Samsasali.blogspot.com

JE? MWIMBAJI WA ''MY GOD IS GOOD'' PASTOR UCHE AMEJITOA JOYOUS CELEBRATION?

Pastor Uche akiimba Solid Rock ndani ya Joyous 15 part 2.
Baada ya kuwemo ndani ya kundi la Joyous Celebration kwa takribani miaka 5, mwimbaji aliyejipatia umaarufu sana duniani ikiwa pamoja na kulitangaza vyema kundi hilo Pastor Agu Uchechukwu au unaweza kumuita Pastor Uche a.k.a Double double yawezekana album ya 16 ndio ilikuwa ya mwisho kwa mwimbaji huyo akiwa na kundi hilo.

Hali hii yakujiuliza maswali kama haya ni hivi karibuni JC imetangaza tarehe ya kurekodi album yao mpya ya 17 ambayo itafanyika mwezi December, mwimbaji Pastor Uche siku chache kabla kupitia katika moja ya kurasa zake za Facebook aliaga kwamba anaelekea nchini Marekani na kuongeza kuwa kurudi kwake nchini Afrika ya kusini hadi mwezi wa tatu mwakani 2013 jambo ambalo linatafsiri kama mwimbaji huyo hayumo tena kundini humo.

Tangu JC ianze tour ya kutangaza album yao ya 16, pastor Uche hakuweza kuhudhuria takribani maonyesho yote kutokana na mialiko anayoipata huko nchini Marekani. Ambapo kwasasa anapanga kurekodi DVD yake ya pili Live huko Houston nchini Marekani, kama ni kweli atakuwa ameachana na kundi hilo inamaanisha atakuwa amebakia kijana mzimbabwe Mkhululi anayeimba nyimbo zinazo kwenda sambamba na Uche au kundi hilo litakuwa mbioni kutafuta mtu wa kuchukua nafasi yake.

Moja ya ratiba zake alizoweka katika ukurasa wake wa FB inaonyesha kabisa kwamba hatarekodi album mpya na JC mwaka huu kwani siku ambayo kundi hilo linarekodi yeye atakuwa na show sehemu nyingine

WANANCHI RUKWA WATEKETEZA SHAMBA LINALOMILIKIWA NA KANISA LA EFATHA

Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya mashamba hayo ijulikanayo kama sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa mawili aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba zilizopo katika kambi hiyo.

Mchungaji kiongozi Michael Meela wa kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo amesema hasara iliyopatikana kutokana na tukio hilo ni zaidi ya shilingi milioni 228 na tukio hilo lilitokea baada ya mbunge wa jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo na kuwahamasisha wanachi watumiee nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.

MWIMBAJI ANAYEIBUKIA KATIKA UIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KIJANA DANNY SANGA AFANYA MAKUBWA IRINGA KATIKA UKUMBI WA IDYDC



                                  Hapa mwimbaji danny akionesha utundu aliopewa na mungu
 hakika ukumbimni palikuwa hapatoshi kila mmoja alitamani kuruka hadi juu




 baadhi ya umati wa watu waliohudhuria katika huduma ya overcomers power center

NIWAKATI WA KUOMBA DUNIA SASA IMEHARIBIKA

HIVI NDIVYO MWANANCHI WA KIJIJI CHA WENDA ALIVYOCHUNWA NGOZI


Hivi ndivyo  mkazi  wa Wenda  alivyochunwa  ngozi na  watu  wasiojulikana (Tunaomba Radhi kwa  picha hizi )

Hii  ndio  nyumba  ulimokutwa mwili  wa  mkazi huyo

eneo la  tukio



Baada ya siku mbili mtandao huu kuripoti tukio la kusikitisha kilichohusisha mauaji ya kinyama ya dereva wa bodaboda sadiki mbelwa (26) katika kijiji cha wenda, Tanangozi Iringa ambapo mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa na majeraha sehemu za kichwani huku ikisadikiwa kupigwa na kitu chenye ncha kali.
eo katika tukio lingine la kusikitisha ambalo limetokea katika kijiji cha wenda kitongoji cha Lupeta amekutwa mwili mwanakijiji aliyetambulika kwa jina la Leornad Kutika (49.

Mwili wa marehemu kutika umekutwa katika nyumba aliyokuwa akiishi huku ukiwa umechunwa ngozi, kunyofolewa macho pamoja na kukatwa sehemu za siri.

Akingea na mtandao huu wa huzuni baba mdogo wa marehemu Martin Kutika mkazi wa lupeta anaeleza kuwa usiku wa kuamkia jana alipigiwa simu ndugu wa marehemu aliyefahamika kwa jina Kibadeni kutika kuwa ndugu yake huyo ambayekwa mujibu wa maeezo yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la akili alikutwa katika nyumba aliyokuwa anaishi huku akiwa amefariki na kuondolewa sehemu za siri na kuchunwa ngozi. Zwadi mwenga ambaye pia ni ndugu wa marehemu anaeleza kuwa alipata taarifa za tukio hilo jana na ndipo alipofika katika nyumba ya marehemu na kukuta akiwa amefariki.

Akilelezea kuhusu tatizo alilokuwa nalo marehemu Mwenga amesema marehemu alianza kusumbuliwa na tatizo la kurukwa akili tangu alipokuwa mdogo japo hakuwahi kufanya vurugu yoyote na wao kama familia wamekuwa wakimpatia chakula na siku mbili kabla ya tukio marehemu alionekana lakini baada ya hapo hawakumuona tenda ndipo wifi yake alipofika nakukuta marehemu amekufa huku akiwa ametendewa unyama huo.
 Afisa mtendaji wa kijiji cha wenda Dismas Ngweta anaeleza kuwa alipigiwa simu na mwenyekiti wa kjjij cha lupeta Geofrey Dugange nakumweleza kuwa hakuna amani katika kijiji hicho kuwa kuna mwanankijiji ambaye ameuawa. Akielezea baada ya kufika eneo la tukio Ngweta anaeleza kuwa walipouangalia mwili wa marehemu waligundua kuwa amechunwa ngozi, kunyofolewa macho, kukatwa sehemu za siri pamoja na kutobolewa katika sehemu ya mguu. Akilinganisha tukio hili na lililotokea siku chache zilizopita Ngweta ameeleza kuwa tukio la dereva wa bodaboda limetokea wakati wa usiku na kusema kuwa inasemekana kuwa tukio la pili limetendeka usiku kwani kwa mujibu wa wanakiji walieleza kumwona marehemu jioni kabla ya tukio.

 Je nijuhudi gani zimefanywa na jeshi la polisi mpaka sasa? Ngweta ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hilo alipiga simu kwa mkuu wa kituo cha ifunda naye akajibu kuwa awasiliana na wa kituo kikubwa Iringa. Mpaka mtandao huu unatoka eneo la tukio hakuna afisa usalama aliyekuwa amefika katika eneo hilo.

Tukio hili ni la mara ya pili kutokea baada ya tarehe 25 Septemba kuripotiwa kuuwawa kinyama kwa dereva wa bodaboda na pikipiki yake kutoonekana.

MADAM RUTI ALIA NA MAKANISA



Mwimbaji wa muziki wa injili nchini, Madamu Ruti Mwamfupe amedai kulizwa na makanisa yanayoshindwa kuwasaidia watu wenye uhitaji kama wagonjwa waliolazwa hospitalini.

Akizungumza  Dar es salaam jana, Madamu Ruti alisema hospitalini kuna baadhi ya watu ambao hawana fedha za kununua hata chakula, wakati watumishi wa Mungu wanakula na kusaza.''
Hata vitabu vitakatifu vinasema; dini iliyosafi isiyo taka mbele za Mungu Baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao ya kujilinda na dunia,'' alisema Madamu.

Mwimbaji huyo alisema, endapo makanisa hayo yangejiwekea utaratibu wa kuwasaidia wagonjwa kila wiki, ingewawezesha baadhi yao kupona haraka. Alisema wagonjwa wengi wanachelewa kupata uponyaji kutokana na kushindwa kupata mlo bora, licha ya kutumia dawa zinazohitaji kula chakula kingi.

Mwimbaji huyo hivi karibuni alikwenda kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road na kutoa misaada ya vitu mbalimbali, vyenye thamani ya sh. 700,000 na fedha taslimu sh. 500,000.

ASKOFU MWASOTA AVUNJA UKIMYA TUHUMA ZA KUNASWA NA KUNDI LA FREEMASON

Askofu David Mwasota, katibu wa baraza la makanisa ya kipentekoste nchini CPCT.
                         
Hatimaye Katibu Mkuu wa Baraza la makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) Askofu David Mwasota, amevunja ukimya wa tuhuma zilizosambazwa sehemu mbali mbali zikieleza kuwa amenaswa na kundi la siri la waabudu shetani Freemasons.

Akiongea na chanzo cha habari cha blogger kwa uchungu, Askofu Mwasota alisema:

“Ndugu yangu naona haya ni mashambulizi, nimezushiwa mengi achilia mbali yaliyoandikwa na magazeti, jumbe zinasambazwa kwa watumishi wa Mungu (wachungaji) wakae mbali na mimi eti nimekuwa freemason, lakini haya yote ni mashambulizi tu…”

Akifafanua zaidi alisema: “Nakwambia ukweli kutoka moyoni mwangu, sijui hata kiongozi mmoja wa kundi la Freemasons, wala sijui hata hekalu lao liko wapi, mimi nilikuwa nafundisha kanisani nikawaonya wapentekoste wakae mbali na watu wasiowajua kwa kuwa wengine ni waabudu shetani, na wanawajia kama watu wema ili kuwarubuni,”alisema kiongozi huyo na kuongeza:

“Nikatoa mfano wa waumini wangu na mimi mwenyewe, nakumbuka niliwaambia kuwa niliwahi kuhudhuria semina moja na baada ya kukamilika nilipewa nishani ambayo  baadaye nilikuja kubaini kuwa ilikuwa na nembo nisisozielewa, sikusema ni nembo za Freemasons, nilisema  nisizozielewa, nikaamua kuitupa hiyo nishani, lakini naona waandishi waliamua kunimaliza, namwachia Mungu aamue kati yetu…”

Alipoulizwa ni semina gani hiyo na kama anauhakika kuwa nembo alizoshtukia sio za kundi hilo, alijibu:

“Sikia ndugu…nilichosema kilikuwa ni mfano tu wakati nahubiri, nilimaanisha kuwa nembo hizo sikuwa na uhakika nazo, hiyo haimaanishi zilikuwa ni za kundi la Freemasons, nimekwisha kueleza sijui hata kiongozi mmoja wa kundi la Freemasons,  wala sina haja nao, mimi nimeokoka naenda mbinguni waabudu shetani ni wanini?”

“Jambo la kustaajabisha zaidi ni kuwa wewe ndio Mwandishi wa kwanza kuongea nami, kuhusu jambo hili kwa mapana yake, wengine walinipigia simu nikawaambia waje ofisini sikuwaona, lakini nikashtukia habari kubwa imeandikwa, hii inaniuma sana…”

Askofu Mwasota, alisema kuwa ameshauriwa juu ya jambo la kufanya na anajiandaa kuchukua hatua kwa kuwa anaona kuwa kuna njama mbaya dhidi yake, huduma anayoiongoza na kanisa la Mungu kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa katika ibada hiyo lengo la mahubiri yake lilikuwa ni kuwaonesha wapentekoste hatari iliyopo mbele yao kwa kuwa makundi hayo ya waabudu shetani yapo na yanawawinda.

“Mimi ni Askofu na kiongozi wa baraza la Wapentekoste, ilikuwa ni wajibu wangu kuonya wenzangu, lakini mifano yangu ilipinduliwa kwa makusudi. Nadhani wakati nahubiri kulikuwa na mwandishi wa (jina linahifadhiwa) ambaye aliichukua kama alivyotaka,” alisema Askofu Mwasota.

Kwa karibu wiki nzima kumekuwa na jumbe mbali mbali zinazosambazwa kupitia simu zikieleza kuwa Askofu Mwasota amenaswa na kundi la Freemasons na kuwataka wapentekoste kukaa mbali naye.

Baadhi pia ya waumini wa makanisa ya Kipentekoste na hata wachungaji wamekuwa wakiulizana huku na kule wakitaka ukweli kuhusu habari za kiongozi huyo wa ngazi ya juu katika baraza la Wapentekoste kutajwa na kundi hilo.

Kutokana na kiu hiyo ya watu wa Mungu, Blog hii  liliamua kuchunguza ukweli wa jambo hilo kuanzia kwa Askofu mhusika na vyanzo vingine vya habari ili kutoa jibu kwa wenye kuguswa na mkanganyiko huo.

Baadhi ya watu wa karibu na Askofu Mwasota, waliofanya mahojiano ya siri nachanzo kimoja cha blog wameeleza wasi wasi wao kuwa kuenea kwa kasi kwa habari hiyo na mazingira yake vinaashiria kuwa huenda kuna mbegu ya chuki inayochochea jambo hilo.

Mmoja wa watu waliohudhuria ibada siku Askofu Mwasota alipohubiri na kuwaonya watu kukimbia makundi ya wale wanaowajia ghafla kama malaika wa nuru, alisema:

“Mimi nilikuwa kwenye ibada siku Askofu Mwasota alipohubiri na kutoa mifano; nilichosikia akisema ni kuwa alihudhuria semina na mwisho akapewa nishani ambayo baadaye alibaini kuwa na nembo, ambazo hakuwa na  uhakika nazo na kwa kutotaka kujichanganya akaamua kuitupa, wala hakusema kuwa amehudhuria mkutano wa Freemasons.”

Katika siku za karibuni kumekuwa na mlipuko wa makundi ya vijana wanaosaka jinsi ya kujiunga na kundi la Freemasons wakidai eti ni suluhisho la maisha magumu.

Habari za kuenea kwa kasi kwa kundi la Freemasons zimekuwa zikivuta hizia za watu wengi, wengine wakidhani kuwa kujiunga nao kunaweza kuwafanya kuwa tajiri.

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO


Mtuhumiwa alijifunika kwa kofia akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi
Gari lililomleta mtuhumiwa
Siku ambayo Daudi Mwangosi alipouwawa kwa bomu katika kijiji cha Nyololo Mufindi
Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa mahakamani.

mwandishi maalum wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Iringa anaripoti kuwa ,Mtuhumiwa huyo amefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu Michael Luena, amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.

Amesema mtuhumiwa huyo mnamo Septemba 02mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.


Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 26 Septemba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Hata hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jambalo limewaletea ugumu waandishi waliokuwapo baada ya kusukumwa ovyo kuzuia mtuhumiwa huyo asipigwe picha.

Kila wakati waandishi walipotaka kupika picha walikuwa wakisukumwa na askari hao huku mtuhumiwa akiwa amejifunika kichwa na kuziba uso kuhakikisha kuwa sura yake haionekanai na waandishi hao.

Katika hali isiyo ya kawaida mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa gari binafsi la kifahari lenye namba za usajili T 320 ARC Toyota Land cruiser GX tofauti na watuhumiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog