Wazazi,
watoto na watu mbali mbali wameshindwa kujizuia na kumwaga chozi
walipokuwa wakiwapokea watoto Sadia Ismail, Doreen Eribariki na Wilson
Tarimo, ambao wamerejea rasmi nchini wakitokea nchini Marekani
walikokuwa wakipatiwa matibabu.
Watoto
hao ambao ni manusura wa ajali iliyoua takriban wanafunzi 32 wa shule
ya msingi Lucky Vicent, wamepokelewa na viongozi mbali mbali wa serikali
wakiwemo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Anna Mghwira, Mbunge wa
Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, wazazi na wanafunzi wa shule ya Lucky
Vicent, waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA).
Watu
mbali mbali walihudhuria uwanjani hapo wakiwa na mashada ya maua
kuwalaki huku kukiwa na burudani mbali mbali kutoka kwa sanii Mercy
Masika wa Kenya, Angel Bernad wa Tanzania na Kwaya ya Shangwe kutoka
jijini Arusha.
Shirika
la Samaritan Purse la Marekani lilijitolea kusaidia watoto hao kuanzia
usafiri na gharama za matibabu kwa muda wote ambao walikuwa nchini humo
wakitibiwa, katika Hospitali ya Sioux City tangu mwezi Mei 15, kufuatia
majeraha makubwa kwenye ajali kubwa waliyoipata tarehe 6 Mei 2017,
wakitokea hospitali ya Mt. Meru Arusha.
0 comments:
Post a Comment