Upinzani Wamtega Rais Magufuli....Watumia Njia Mbadala Bungeni Kukumbushia Uuzwaji wa Nyumba za Serikali, Wadai MV Dar es Salaam Ni Jipu Lililoiva

Kambi ya Upinzani imelizidi maarifa  Bunge na kurejesha sakata la kuuzwa nyumba za Serikali ambalo juzi lilisababisha kiti cha Spika kuagiza yaondolewe maneno yanayomtaja Rais katika hotuba ya maoni mbadala.


Juzi, Kamati ya Kanuni za Bunge ilihariri hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ikiondoa maneno yanayomtaja Rais John Magufuli na badala yake kuweka neno Serikali kwenye sakata la uuzwaji nyumba za Serikali.

Kamati hiyo pia iliondoa suala la mkataba wa Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises, rushwa, mauaji ya wanasiasa, mwenendo wa Rais na Bunge kulinda wahalifu, jambo lililomfanya msemaji wa kambi hiyo, Godbless Lema kukataa kusoma hotuba yake.

Lakini jana katika hotuba ya kambi ya upinzani kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mbunge wa Vunjo, James Mbatia alilirejesha sakata hilo akieleza kuwa ni muda sahihi kwa Rais John Magufuli kurekebisha kasoro zilizojitokeza wakati akiwa waziri ili kurejesha imani katika jamii.

Mbali na sakata hilo, pia Mbatia alizungumzia sakata la kivuko cha Mv Dar es Salaam ambacho kinatakiwa kifanye safari kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, akikielezea kuwa “ni jipu ambalo limeiva kwa viwango vyote na sasa linatakiwa litumbuliwe mara moja”.

Suala la Mv Dar es Salaam liliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Zitto alisema kuwa hoja ya kivuko hicho lazima ichukuliwe hatua ili iaminike kuwa kuna nia ya dhati ya kupambana na ufisadi nchini.

“Naona suala hili linakwepwakwepwa, hivyo litolewe maamuzi,” alisema Zitto.

Pia mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alisema suala la Mv Dar es Salaam kuwa iko chini ya kiwango, liliwahi kusemwa na mbunge wa upinzani lakini Serikali ikakataa.

Hata hivyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) amesema ukweli katika ripoti yake. “Hili suala inabidi liangaliwe kwa kuwa kuna watu wanahitaji kutumbuliwa hivyo hao watu waangaliwe,” alisema Selasini.

Akisoma hotuba ya maoni mbadala ya kambi ya upinzani, Mbatia alisema wakala wa majengo nchini ndiye muhusika mkuu katika kuhakikisha nyumba za Serikali zinakuwa katika hali nzuri kwa watumishi wa Serikali kuishi.

“Katika muktadha huo, kambi ya upinzania inalikumbusha Bunge kwamba kati ya mwaka 2002 mpaka 2004 Serikali iliuza nyumba 7,921 na mpaka mwaka 2008 ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,” alisema Mbatia.

Alisema katika biashara hiyo ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tamisemi, Serikali ilipata Sh252 milioni lakini sasa inahitaji kusaka zaidi ya mara mbili ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.

Mbatia alisema Serikali ingetumia Sh677.6 milioni kujenga nyumba mpya ili zirejeshwe Tamisemi.

“Kwa vile hata wale waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kati yao wapo walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo, kambi ya upinzani inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.”

Mbatia alisema kumbukumbu rasmi za Bunge zinaonyesha Serikali ilitoa taarifa kuwa kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba hizo na ilitarajiwa kumaliza kazi Februari 2007, lakini hadi leo hakuna taarifa iliyotolewa na Serikali na kuitaka Serikali ya Awamu ya Tano izirejeshe.

Akinukuu kumbukumbu rasmi za Bunge za Aprili 25, 2008 wakati wa kikao cha 18 cha Mkutano wa 11, Mbatia alisema baada ya mjadala mkubwa wa hoja binafsi iliyowasilishwa na mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, Bunge kwa kauli moja lilipitisha azimio kuwa nyumba hizo zirejeshwe serikalini.

“Bunge linaazimia kwamba Serikali ifanye yafuatayo: Itekeleze mara moja bila kusita, agizo la Rais kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha utaratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa Serikali wakati huo na vilevile nyumba ambazo hazikupaswa kuuzwa kama zile zilizopo kwenye maeneo ya utawala wa Serikali,” alisema akinukuu azimio hilo.

Mbatia aliitaka Serikali itafsiri kaulimbiu ya “hapa kazi tu” kwa kuelekeza azimio hilo, akisema Kikwete alikosa uthubutu wa kusimamia msimamo wake.

“Tunajua uuzwaji huo ulisimamiwa na wizara aliyokuwa akiiongoza yeye (Rais Magufuli) na kuna uwezekano mkubwa kwamba alisimamia maamuzi ambayo hakuwa na uwezo wa kuyakiuka,” alisema Mbatia.

“Sasa ni muda sahihi Rais Magufuli kurekebisha kasoro alizozisimamia katika mchakato huo ili kurejesha imani katika jamii.”

Kivuko cha Bagamoyo
Kuhusu kivuko cha Bagamoyo, Mbatia alisema kilinunuliwa na Temesa chini ya uongozi wa Waziri wa Ujenzi wa Serikali ya Awamu ya Nne ambaye ndiye Rais wa sasa.

Mbatia alisema kwa mujibu wa ripoti ya CAG katika hesabu za Serikali Kuu za mwaka ulioishia Juni 30, 2015 iliyotolewa Machi 2016, alibaini ununuzi wa boti ‘feki’ na mbovu uliofanywa na Temesa na kugharimu dola 4,980,000 za Marekani (sawa na Sh7.9 bilioni).

Alisema CAG alibaini masuala makuu mawili ambayo ni kasi ya kivuko hicho ni tofauti na kasi iliyotakiwa kuwapo na pia cheti cha kukikubali kivuko hicho kilikuwa kinyume na Kanuni ya 247 ya Sheria ya Manunuzi ya Umma.

“Tabibu wa kutumbua jipu hili yuko wapi? Au msemo usemao kuwa ‘mganga hajigangi’ unatumika hapa?” alihoji.

Juzi jioni hali kama hiyo ya kuzungumza masuala yaliyozuiwa na Kamati ya Kanuni za Bunge, ilijitokeza wakati wabunge wakijadili Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili......Wenzao Wabaki Vinywa Wazi Kikaoni

Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni.
"Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....
"Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.

“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.
Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Magufuli alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana. Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho

Rais Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.

Utendaji wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisadi.

Bavicha Walaani Hotuba ya Godbless Lema Kuzuiwa Bungeni........Wataka Waziri Kitwanga Ajiuzulu na Akigoma Awajibishwe

Wakati uchunguzi wa kampuni ya Lugumi inayodaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye vituo vya polisi ukiendelea, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga kujiuzulu wadhifa wake kupisha uchunguzi huo.

Limesema haiwezekani waziri anayetajwa kuhusika katika sakata hilo kuendelea na kazi huku Jeshi la Polisi linalodaiwa kutapeliwa na kampuni hiyo likiwa chini ya wizara yake.

Hata hivyo, waziri huyo amewajibu vijana hao wa upinzani kwa kusema hawezi kubishana na watoto na hayo waliyoyatoa ni mawazo yao binafsi wana haki ya kuyasema.

“Nimeshasema mara nyingi, siwezi kuzungumza tena kuhusu haya mambo. Wao kama wamesema waache waseme,” alisema.

Baraza hilo lililoibuka na hoja tatu jana, limesema kama waziri huyo atagoma kujiuzulu kupisha uchunguzi unaofanywa na kamati ndogo ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Rais John Magufuli anapaswa kumwajibisha ingawa suala hilo ni gumu kutokana na uswahiba uliopo kati ya kiongozi huyo mkuu wa nchi na Kitwanga.

Kampuni ya Lugumi ilibainika kutotimiza matakwa ya mkataba wake baada ya kufunga mashine 14 tu kati ya 108 zilizotakiwa kufungwa, licha ya kulipwa zaidi ya asilimia 90 ya fedha kwa mujibu wa mkataba ambazo ni Sh37 bilioni.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14 ndiyo iliyofichua udhaifu huo na baadaye Bunge kuanza uchunguzi baada ya kutoridhishwa na maelezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani na polisi kuhusu mkataba huo.

HATIMAYE MUNGU AMFUTA MACHOZI MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI LEMBO JUNIOR MZEE WA UWE KILA KITU.



                   HUU NI UJUMBE KUPITIA UKULASA WAKE WA FACEBOOK.
#MERCIFUL_GOD_HAS_SURPRISED_US!
NINA SHINDWA NIANZIE WAPI!
MWAMKE NI WAKUPENDWA NA KUTHAMINIWA NA KUPEWA "RESPECT"
LEO NI OUR 2ND ANNVERSARY NA JANA SAA TANO ASUBUHI MUNGU ALITUBARIKI a VERY VERY HEALTHIER BABY GIRL named REGINA(Queen)
#MUNGU_UNAUJUA_MOYO_WANGU_ASANTE_SANA_YESU! KWA KUNILETEA MAMA MAVOCAL ATAKUTUMIKIA MAISHA YAKE YOTE!#ANNA_EMMANUEL_LOVES_YOU_VERY_MUCH!hahahaaaaa kwa WENYE dhawadi tigopesa na mpesa ziko active

           
               DENIS NYALI BLOG INAKUPONGEZA KWA BARAKA HIYO.

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI UGANGA YA MAKETE MKOANI NJOMBE ASHINDA LAKI NANE KATIKA DROO YA NMB.

hili ndilo gurudumu la bahati na sibu. 


meneja wa benki ya nmb tawi la iringa  kulia pichani akifurahia jambo


meneja wa nmb akimtambulisha mshindi kutoka makete aliyeingia kwenye droo.



baadhi ya wafanyakazi na wateja wa nmb.




na denis nyali.
shindano la pata patia linaloshindanishwa na benk ya nmb nchini hii leo limeendelea baada ya mshindi mmoja kuibuka kwa kujinyakulia laki nane.
akizungumza kuhusu shindano hilo meneja wa benki ya nmb tawi la iringa sumka mbuba amesema katika mkoa wa iringa kulikuwa na washindi wa tatu ambao wa ni miongoni mwa washindi 24 wa nchi nzima
katika shindano hilo lilifanyika katika benki ya nmb tawi la iringa yuda kiluswa mwalimu wa shule ya msingiuganga wilaya yamakete mkoa wa njombe ameibuka mshindi kwa kujinyakulia laki nane .
akizungumza mara baada ya kushinda fedha hizo kiluswa ameishukuru benki ya nmb na kuahidi kuziwekeza katika kupanda miti.

Wakurugenzi Katavi Kikaangoni ......Mkuu wa Mkoa Awataka Warejeshe Milioni 200 Walizolipa Watumishi Hewa

Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Katavi, wameagizwa kurejesha Sh200 milioni wanazodaiwa kuwalipa watumishi hewa ndani ya siku 21.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali mstaafu, Raphael Muhuga alitoa agizo hilo jana katika kikao baina yake na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na waandishi wa habari.

Alikuwa akitoa taarifa ya kubainika kwa watumishi hewa wapya mkoani humo.

Muhuga alisema kuendelea kubainika kwa watumishi hao hewa, itawabidi wakurugenzi kuhakikisha fedha zote zilizolipwa kwa watu hao zinarejeshwa serikalini kwa muda aliowataka wazirejeshe na wampatie taarifa itakayothibitisha fedha hizo kurejeshwa.

Pia, mkuu huyo wa mkoa aliagiza maofisi wa ofisi ya utumishi wachukuliwe hatua ya kinidhamu kwa kusababisha watumishi hao hewa kulipwa fedha.

“Hili siyo suala la bahati mbaya, bali hawa watu walidhamiria kulipa mishahara hiyo hewa naimani wapo wenye maslahi juu ya jambo hili,”alisema Muhuga.

Aliagiza wakurugenzi wote wa halmashauri, wahakikishe maofisa utumishi wanawafuta watumishi hewa wote kwenye leja zao na wawachukulie hatua wote waliohusika na suala hilo.

Hata hivyo, aliishukuru kamati ya watu wanne iliyoundwa kufanya kazi ya uhakiki wa watumishi mkoani humo.

Aliitaka iharakishe kukamilisha uchunguzi wa watumishi 15 ambao taarifa zao zimebainika kuwa na utata

Serikali Yabaini tani 4,579.2 za Sukari zilizokuwa zimefichwa.

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) imebaini kuwepo kwa sukari iliyofichwa  tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari Kilombero.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa Taasisi  hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi ilitembelea maghala yaliyopo Tabata Jijini Dar es salaam na kubaini uwepo wa sukari hiyo.

TAKUKURU tayari imetembelea  Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo.

Aidha uchunguzi  uliofanywa na Taasisi hiyo ulibaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza  sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari  hiyo ili iweze kusambazwa.

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika eneo la Kitumbini  kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji  bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa  licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.

Katika uchunguzi wake TAKUKURU pia  imebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.

Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni  kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.

TAKUKURU  inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa Sheria

Baba Aua Mtoto wa Kambo chumbani.......Yadaiwa ni Baada ya kumtuma mkewe Dukani kununua Dawa Watu wawili wamekufa katika matukio mawili tofauti, akiwamo mtoto Ma


Watu wawili wamekufa katika matukio mawili tofauti, akiwamo mtoto Mariam Haule (2) kwa kunyongwa na baba yake wa kambo baada ya kumtuma mama yake dukani kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea Mei 2.

Issa alisema kuwa mtuhumiwa huyo mkazi wa Kijiji cha Usimba, Wilaya ya Kaliua mkoani humo kabla ya kufanya mauaji hayo, alimtuma mkewe, Kalunde Malugu kwenda dukani kununua dawa .

Alisema baada ya mkewe kwenda dukani, alipata mwanya wa kufanya mauaji hayo kisha kutokomea kusikojulikana.

“Tunawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano ili tuweze kumkamata mtuhumiwa afikishwe kwenye mkondo wa sheria,” alisema Issa.

Kamanda huyo alisema jeshi hilo litahakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Mama wa mtoto huyo alisema alitumwa na mumewe dukani kununua dawa, lakini aliporudi alikuta mlango umefungwa na alipoingia ndani alibaini mtoto wake ameuawa.

Alisema hafahamu sababu za mauaji hayo na wala hakukuwa na malalamiko au madai yoyote kutoka kwa mumewe kuhusiana na mtoto huyo.

Katika tukio la pili; Mkazi wa Kijiji cha Rwamkoma wilayani Butiama, Magesa Machera (46) amekutwa ameuawa kwa kunyongwa baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema tukio hilo lilitokea Mei 3, mwaka huu saa tisa usiku.

Alisema inadaiwa kuwa siku ya tukio hilo, mpenzi wake, Remmy Samwel (35) alitoka nje kwenda kujisaidia, lakini aliporudi alimkuta Machera akiwa chini amekufa.

Ng’anzi alisema mpenzi wake huyo ambaye ni mgeni katika kijiji hicho huwa na mazoea ya kwenda kumsalimia mara kwa mara na walikuwa wakinywa pombe za kienyeji. “Uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea na polisi inamshikilia mpenzi wake,” alisema.

Mume Amuuwa Mke Wake Pamoja Na Mtoto Kwa Kuwachinja Na Kisu Wilayani Bagamoyo Mkoa Wa Pwani

JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Frowin Peter Mbwale (26) mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuua kwa kuwachinja mkewe Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emanuel Frowin (3) kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:30 jioni eneo la Zinga kata ya Dunda Tarafa ya Mwambao wilayani Bagamoyo.

Mushongi alisema kuwa katika hali isiyo kuwa ya kawaida juzi siku ya tukio mtuhumiwa akiwa na mwenzake alijulikana kwa jina la Rajabu Juma (20) Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam waliwaua watu hao kwenye vichaka vilivyopo kwenye eneo hilo la Kaole.

“Muda huo mtuhumiwa akiwa na mwenzake alimhadaa mke wake kuwa waende kwenye nyumba yao ambayo inaendelea kujengwa kwa lengo la kuitazama ambapo mke wake alikubali na kumbeba na mtoto wao na kwenda huko ambako aliwachinja shingoni,” alisema Kamanda Mushongi.

Alisema kuwa mtuhumiwa kumbe lengo lake halikuwa kuangalia ujenzi wa nyumba yao huko Kaole kumbe alikuwa na lengo lingine la kufanya unyama huo ambao aliutekeleza akiwa na rafiki yake huyo ambaye walishirikiana kumchinja mke na mtoto wake.
“Chanzo cha mauaji hayo ni mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa ana uhusiano na mwanaume mwingine aitwaye Hamza mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam na kusababisha mauaji hayo ya kusikitisha ambayo yamewaumiza watu wengi,” alisema Mushongi.

Alibainisha kuwa miili ya marehemu hao ilikutwa ikiwa imechinjwa na watu hao umbali wa mita 100 kutoka barabara ya magari itokayo Kaole kwenda eneo la Mbegani.

Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa majira ya saa 3:30 usiku baada ya wananchi Zinga kuwatilia mashaka walipokuwa wakijaribu kutaka kutoroka na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika, miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kusubiri ndugu kwa ajili ya mazishi.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog