MGOMBEA
urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, amewahakikishia wana-CCM na
Watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa Tsunami
na si wa kishindo wala kimbunga.
Dk
Magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani Mtwara juzi
alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza
kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa
CCM ni lazima na upo pale pale.
Alisema
ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama
na kwamba watu hao wameiacha CCM ikiwa safi na salama zaidi.
Alisema
watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa
mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ambapo chama kiliwakata na
kukimbilia vyama vingine vya upinzani.
Aliwataka
wana-CCM wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake
washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya
kampeni za kisayansi.
Aidha,
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema ni kazi rahisi
kumnadi Dk Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.
Mwigulu,
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema walioshindwa kwenye
mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha
kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi,
lakini wataumbuka mapema.
Akizungumza
na mamia ya wana-CCM waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama
ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua
kuwa mgombea na kumdhamini, Dk Magufuli aliwataka makada hao na
Wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa Watanzania walio wengi bado
wanakipenda Chama.
“Ushindi
wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa Tsunami, watapiga kelele sana,
watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa CCM ni lazima. Ni
lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani,” alisema.
Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, CCM ina kundi moja tu la ushindi.
“Hako
ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka
upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao
safi.
“Lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM.
"Hata
ukiangalia tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wapo
waliotoka wako akina Kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine
walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao,” alisema.
Alisema
iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu,
asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atimize
matarajio yao.
Dk
Magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na
kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata
kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.
Aliwataka wana-CCM wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda Chama.
Dk
Magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya CCM, alisema alikuwa mbunge
katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila
kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.
Alisema
anaifahamu vizuri Mtwara, Tanzania, CCM na kero za Watanzania
anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya
utendaji kwa maendeleo ya taifa.
“Nilichaguliwa
na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale
walionichagua waliwakishia Watanzania wote. Niwahakikishie kuwa mwaka
huu, tutashinda zaidi,” alisema.
Aliwataka
wana-CCM katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo
kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si
maneno matamu bila vitendo.
“Chama
nakifahamu, shida za wana-CCM nazifahamu, matarajio yao nayafahamu,
shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa
uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo,” alisema.
0 comments:
Post a Comment