MAHAKIMU WA MAHAKAMA ZA MWANZO MUFINDI WAPEWA PIKIPIKI
Jaji Mary Shanghai akikata utepe wakati akikabidhi pikipiki hizo |
Pikipiki zilizotolewa kwa mahakimu wa mahakama hizo |
JAJI
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mary Shanghai amekabidhi pikipiki nne
kwa mahakimu wa mahakama za mwanzo za Ifwagi na Kibao, Malangali, Kasanga na
Mgololo, zote za wilaya ya Mufindi.
Kutolewa
kwa pikipiki hizo, kumeelezwa na mahakimu wa mahakama hizo kwamba kutarahisisha
utendaji kazi wao na kuongeza ufanisi katika idara hiyo muhimu ya utoaji haki.
Jaji
Shanghai alikabidhi pikipiki hizo juzi katika ziara yake ya a kufahamiana na
watendaji wa mahakama na kukagua shughuli mbalimbali za mahakama zinazofanywa
wilayani humo.
Katika
ziara hiyo, Shanghai alitembelea mahakamaa ya wilaya ya Mufindi na mahakama ya
mwanzo Mafinga, Sadani, Mlangali, na Iramba.
Akisoma
taarifa ya jumla ya mahakama ya wilaya hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Victoria Nongwa alisema mahakama
hiyo inasimamia jumla ya mahakama za mwanzo zilizoko katika maeneo mbalimbali
wilayani Mufindi.
Alizitaja
mahakama hizo kuwa ni Mahakama ya Mafinga mjini, Mufindi (Kibaoni), Kasanga
(Igowole) Malangali (Isimikinyi), Kibengu, Mapanda, Sadani (Utosi), Iramba
(Itulavanu) Mgololo, Ihanu (Ibwanzi) na Ifwagi.
Alisema
mahakama hiyo isiyo na mhasibu ina watumishi wa kada mbalimbali 31 ambao kati
yao wanne ni mahakimu wakazi wa mahakama ya wilaya na watatu ni mahakimu wakazi
wa mahakama za mwanzo.
Aliwataja
watumishi wengine kuwa ni mahakimu watatu wa mahakama za mwanzo wasio mahakimu
wakazi, mahafisa kumbukumbu watano ,wapiga chapa wawili, wahudumu wanne,
walinzi nane na dereva mmoja.
Katika
kuboresha utendaji wa mahakama hiyo, Nongwa ameomba msaada wa ujenzi wa
mahakama ya mwanzo Ifwagi na ukarabati wa nyumba ya hakimu wake.
Wakati
mjini Mafinga panatakiwa kujengwa upya mahakama yake ya mwanzo, alizitaja
mahakama zingine zinazohitaji ukarabati kuwa ni Mufindi (Kibao), Kasanga
(Igowole) na Malangali inayotakiwa kukarabatiwa choo na jengo la kutunzia
vielezo.
Alisema
mahakama hiyo inahitaji pia kujengewa chumba cha mahabusu Malangali na fedha ya
kuwezesha kupatikana kwa umeme mbadala katika mahakama ya mwanzo Kibengu
Pamoja
na maombi hayo, wazee wa baraza la Mahakama ya Mwanzo Mafinga wameulalamikia
uongozi wa mahakama ya Wilaya hiyo kwa kutowalipa fedha zao za vikao
vinavyohusisha kesi zilizofutwa.
Akiwatia
moyo kwa kazi wanazofanya Jaji Shanghai alisema: “kuanzia sasa baraza la wazee
litalipwa fedha zao kwa wakati hata kama kesi wanazohudhuria zitahirishwa au
kufutwa.
Akizungumzia
utendaji wa mahakama, Shaghai aliwaomba
mahakimu kujiepusha na rushwa kwa
kuwa ni moja ya sababu inayokwamisha upatikanaji wa haki katika chombo hicho.
0 comments:
Post a Comment