AL AHLY YAPANGWA KUNDI LA ‘KIFO’ KOMBE LA SHRIKISHO, KUNA ETOILE NA SEWE SPORT YA IVORY COAST

Na Princess Asia, Dar es Salaam
VIGOGO wa Misri, Al Ahly wamepangwa katika Kundi B la Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2014 pamoja na Sewe Sport ya Ivory Coast, Etoile du Sahel ya Tunisia na Nkana FC ya Zambia.
Katika droo iliyopangwa leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), wababe wa Cameroon, Coton Sport wametupwa Kundi A pamoja na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, AS Real ya Mali na AC Leopards ya Kongo Brazzaville.
Kundi la kifo; Al Ahly imepangwa kundi gumu Kombe la Shirikisho Afrika 


Mechi zinatarajiwa kuchezwa kuanzia kati ya Mei 16 na 18 na Juni 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na 22-24 na washindi wawili wa kila kundi watasonga Nusu Fainali.MAKUNDI KOMBE LA SSHIRIKISHO:
KUNDI A: AC Leopards, ASEC Mimosas, AS Real Bamako na Coton Sport
KUNDI B: Al Ahly, Etoile du Sahel, Sewe San Pedro na Nkana FC

REAL MADRID 'ILIVYOIHARIBU SURA' BAYERN MUNICH JANA ALLIANZ ARENA

Shughuli imekamilika: Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia ushindi wao wa mabao 4-0 jana dhidi ya Bayern Munich katika Nusu Fainali ya pili ya Ligi Mabingwa Ulaya Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani. Real imetinga fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-0 baada ya awali kushinda 1-0 Santiago Bernabeu.
All sewn up: Cristiano Ronaldo fires home a free-kick to complete Real Madrid's victory over Bayern
All sewn up: Cristiano Ronaldo fires home a free-kick to complete Real Madrid's victory over Bayern
Ecstatic: Ronaldo wheels away to celebrate with Gareth Bale (left) and Luka Modric after scoring
Ecstatic: Ronaldo wheels away to celebrate with Gareth Bale (left) and Luka Modric after scoring
On the attack: Cristiano Ronaldo fires the ball past Bayern goalkeeper Manuel Neuer to score Real's third
On the attack: Cristiano Ronaldo fires the ball past Bayern goalkeeper Manuel Neuer to score Real's third
Victory: Goalscorer Ronaldo is congratulated by Gareth Bale during Real Madrid's comprehensive win
Victory: Goalscorer Ronaldo is congratulated by Gareth Bale during Real Madrid's comprehensive win
Opener: Sergio Ramos climbs highest in a crowded box to head Real Madrid into the lead against Bayern

ASKARI POLISI WAWILI WAUWAWA NA MAJAMBAZI KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI HUKO TA

Baadhi ya askari Polisi wakiutoa mwili wa askari Polisi kwenye Wodi namba moja aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko katika Tarafa ya Ussoke wilayani Urambo askari huyo aliyefahamika kwa namba F.5179 PC JUMANNE,walipigwa risasi wakiwa na askari mwenzake ambaye pia alifariki papo hapo namba G.3388 PC SHABAN. Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA akizungumza...

BINTI ASHUSHIWA KIPIGO NA MAMA YAKE BAADA YA KUWEKA PICHA ZA UCHI MTANDAONI

Binti alipost picha yake ambayo imeelezwa kuwa ni ya nusu uchi kwenye page yake ya facebook na kama kawaida ya internet ikasambaa ghafla. Mama wa binti huyo baada ya kusikia hizo habari hakuweza kujizuia na kumpa kichapo kikali kwa kuchapa na mkanda binti yake huyo mwenye umri wa miaka 12. Baada ya video hii kusambaa mama huyo raia wa Trinidad and Tobago amesema hajilaumu kumchapa...
 
 
 
 
 
 

ASKARI POLISI WAWILI WAUWAWA NA MAJAMBAZI KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI HUKO TABORA



Baadhi ya askari Polisi wakiutoa mwili wa askari Polisi kwenye Wodi namba moja aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko katika Tarafa ya Ussoke wilayani Urambo askari huyo aliyefahamika kwa namba F.5179 PC JUMANNE,walipigwa risasi wakiwa na askari mwenzake ambaye pia alifariki papo hapo namba G.3388 PC SHABAN.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji ya askari Polisi wawili ambao waliuawa wakati wakijitayarisha kukabiliana na Majambazi watatu waliovamia nyumbani kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la IBRAHIMU MOHAMED mkazi wa Ussoke ambapo walipora zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili pamoja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi laki moja na ishirini elfu.Kamanda SUZAN alisema majambazi hayo yalikuwa yakitumia bunduki aina ya SMG.


Mwili wa askari namba F.5179 PC JUMANNE ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete,askari huyo alifariki dunia wakati madaktari wakijaribu kuokoa uhai wake kufuatia kujeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na majambazi matatu huko Ussoke wakati askari huyo akiwa anajipanga na mwenzake kukabiliana na majambazi hayo yaliyovamia nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja Ibrahimu Mohammed.
- See more at: http://www.farajimfinanga.com/2014/04/askari-polisi-wawili-wauwawa-na.html#sthash.7JCzslKo.dpuf
 

ASKARI POLISI WAWILI WAUWAWA NA MAJAMBAZI KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI HUKO TABORA



Baadhi ya askari Polisi wakiutoa mwili wa askari Polisi kwenye Wodi namba moja aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko katika Tarafa ya Ussoke wilayani Urambo askari huyo aliyefahamika kwa namba F.5179 PC JUMANNE,walipigwa risasi wakiwa na askari mwenzake ambaye pia alifariki papo hapo namba G.3388 PC SHABAN.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji ya askari Polisi wawili ambao waliuawa wakati wakijitayarisha kukabiliana na Majambazi watatu waliovamia nyumbani kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la IBRAHIMU MOHAMED mkazi wa Ussoke ambapo walipora zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili pamoja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi laki moja na ishirini elfu.Kamanda SUZAN alisema majambazi hayo yalikuwa yakitumia bunduki aina ya SMG.


Mwili wa askari namba F.5179 PC JUMANNE ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete,askari huyo alifariki dunia wakati madaktari wakijaribu kuokoa uhai wake kufuatia kujeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na majambazi matatu huko Ussoke wakati askari huyo akiwa anajipanga na mwenzake kukabiliana na majambazi hayo yaliyovamia nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja Ibrahimu Mohammed.
- See more at: http://www.farajimfinanga.com/2014/04/askari-polisi-wawili-wauwawa-na.html#sthash.7JCzslKo.dpuf

ASKOFU DR SOLLO AMSHAURI RAIS KIKWETE KULIVUNJA BUNGE LA KATIBA, AWASHANGAA UKAWA KWA VURUGU

Rais Dr Jakaya Kikwete
Viuongozi  wa UKAWA

   Askofu Dr Boaz Sollo akiwa katika moja kati ya mikutano  yake ya  kuliombea Taifa amani 



UMOJA  wa  katiba ya  wananchi (UKAWA)  wazidi  kukaliwa kooni baada yaaskofu  wa  kanisa la Overcomers Power Centre Iringa Dr  Boaz Sollo kupinga vikali uamuzi  wa UKAWA kutoka bungeni na kwenda kwa wananchi kabla ya kuifanya kazi  waliyotumwa  bungeni kama  wajumbe wa  bunge la katiba na  hivyo  kumshauri  Rais wa jamuhuri ya muungano  wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete kulivunja bunge  hilo ili kuepusha amani kuvurugwa  nchini.

Huku akisema kuwa akiwa kama mtumishi  wa Mungu anaamini kabisa kuwa  serikali mbili ni jibu la watanzania  katika  endeleza umoja ,amani na mshikamano ulioachwa na waasisi  wa Taifa  hili hayati Baba wa TaifaMwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Rais waKwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kuendelea  kuvurungwa na wanasiasa  wachache wasiopenda amani ya nchi  hii .

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kwa njia ya  simu kutoka jijini Dar es salaam ambako amealikwa kwa  huduma za kanisa , askofu Dr  Solloa  alisema  kuwa tayari  kanisa lake  limeanza kufunga na kuomba kwa ajili ya amani nchini na kuliombea  bunge  hilo la katiba  ili mwenyezi  Mungu  kuliunganisha  bunge  hilo na kuepusha mgawanyiko  ulioanza  kujitokeza na kundi   hilo la wana Siasa wanaojiita  wana UKAWA .

" Watamzania tulipongeza uteuzi  wa Rais wetu mpendwa Dr Jakaya Mrisho  Kikwete kwa  kuteua  miongoni mwa  watanzania  wachache kati  ya  wengi kwa ajili ya kwenda kushiriki  bunge  hilo kuandaa katiba ya nchi huku  tukiamini  kuwa walioteuliwa wangetufikisha pazuri zaidi tofauti na ilivyo  sasa ambapo wajumbe  hao  wameanza kuhatarisha amani na utulivu nchini "

Kitendo  cha  wajumbe  wa bunge  hilo kutoka nje ya ukumbi na kutaka kuanza  kuzunguka mikoani ni sawa na kuwasaliti  wananchi  ambao walikuwa  wakisubiri kwa hamu wajumbe hao kuwaletea katiba mpya ila  sasa wameanza kutishia amani ya nchi kwa kutafuta  huruma ya  wananchi katika kuungwa mkono wao  na  vyama  vyao.

" Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais Dr Kikwete  ni kulivunja kabisa  bunge  hilo ili kunusuru amani ya nchi  hii ambavyo  dalili ya  kuvurugwa imeanza  kujitokeza kupitia UKAWA ....tulitegemea wajumbe  hao wangebaki ndani ya bunge na kutuandalia katiba  bila kuunda umoja wa  kuanzisha  vurugu nchini kwani wote  bila kujali vyama vyao na taasisi  zao  walizotoka walipaswa  kuwa kitu  kimoja katika  bunge  hilo kwa kuwasilisha hoja za kuwa na katiba  bora si vinginevyo "

Alisema  kuwa ni  vema kuendelea na katiba  iliyopo kuliko  kusubiri katiba ya  wajumbe hao ambayo mwelekeo  wake  si mzuri  bali  upo kwa ajili ya matakwa ya wachache  kisiasa .

Askofu  huyo  alisema  kuwa wananchi wa Zanzibar wanachanganywa na wana siasa  hao  ila ukweli wazanzibar   na  watanzania  wanapenda  kuona amani iliyopo  inaendelea  kuwepo na suala la maendeleo linaendelea  na sio utitiri  wa serikali hali maisha  yao kiuchumi ni duni .

Hata  hivyo  alisema kutokana na mwenendo  wa  bunge  hilo kwa  sasa  kanisa lake  limetangaza mfungo wa maombi maalum kwa ajili ya Tanzania  ili kuepuka chuki kupandikizwa na wachache kwa lengo la kuvuruga amani  yetu .
source. francis godwini.
ANNA DAT KUTOKA MOSHI NA YERONIMO MWALO KUTOKA DAR WAITIKISA IRINGA KATIKA SEMINA ILIYOANDALIWA NA HUDUMA YA OVERCOMERS POWER CENTER MJINI IRINGA.
     Anna dat kutoka moshi akimsifu mungu katika semina hiyo.

 yelonimo mwalo mume wa mwimbaji wa nyimbo za injli stera joel akimsifu mungu katika semina hiyo.
wanakwaya ya agape wakimsindikiza bwana mwalo wakati akimtukuza bwana.

katika kutokomeza nguvu za giza uchawi na laana opareshesheni iliyoongoza
wa na askofu wa huduma ya overcomers powercenter ya mjini iringa ambayo imedumu kwa siku thelamini wiki hii kumeshuhudiwa na na semina na kongamano kubwa la kihistoria ambapo mhubiri  kutoka jijini dar professa  ikongo amehudumu sambamba na mwenyeji wake askofu boaz sollo .
miongoni wa mambo makubwa yaliyojitokeza katika semina hiyo ni pamoja na watu kufunguliwa kwa watu waliokuwa wakiteswa na nguvu za giza laana na mikosi ambapo kwa jina la  yesu wote hao wamepokea uponyaji.
semina hiyo ilipambwa na waimbaji kutoka dar na moshi akiwemo yelonimo mwalo pamoja na anna dat kutuka moshi.
semina hiyo inatarajiwa kuisha siku ya pasaka ambapo oparation haribu itakuwa inahitimishwa.

TAHADHARI KUTOKA JESHI LA POLISI KATIKA KUSHEREHEKEA PASAKA

Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa
wananchi kuwa makini katika suala la usalama wa maisha na mali zao.

Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na endapo vitajitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka.

Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Vilevile, Jeshi la Polisi linawataka madereva na watu wote watakaokuwa wakitumia barabara, kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka kwenda mwendo kasi, kujaza abiria kupita kiasi na

kutumia vilevi wawapo kazini.

Wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na
uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi.

Aidha, wazazi wawe makini na watoto wao, kutokuwaacha watembee peke yao ama kwenda disko toto bila kuwa chini ya uangalizi wa watu wazima ili kuepusha ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

Wananchi wakumbuke kutokuacha makazi yao bila uangalizi na endapo italazimu kufanya hivyo watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya, watoe taarifa haraka kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu yao, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.

Mwisho, Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya biashara hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, mahoteli na maeneo ya benki.

Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji wa wahalifu hao endapo uhalifu unatokea.

Tunawatakia Watanzania wote Pasaka njema.


Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.
   Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze 
 
Bagamoyo mkoani Pwani kupitia chama cha mapinduzi CCM, ameibuka kidedea kwa asilimia 86.61 katika uchaguzi huo na kuwamwaga wagombea wengine kutoka vyama vinne vya upinzani.
 
Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha Ridhiwani ameongoza akifuatiwa na CHADEMA ,CUF,NRA na ASP.

Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo April 7 majira ya saa nane usiku katika shule ya sekondari Chalinze na  Msimamizi wa uchaguzi huo  Bw.Samwel Salianga ambapo amesema CCM – Ridhiwani Kikwete amepata kura  20,828 sawa na  86.61%, Chadema -Mathayo Torongei amepata kura 2,544 sawa na asilimia 10.58,CUF- Fabian Skauki  476 sawa na asilimia 1.98,NRA Hussein Ramadhani kura 60 asilimia 0.25 huku AFP Ramadhani Mgaya amepata kura 186 sawa na asilimia 0.59.

Salianga amesema kati ya watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni watu elfu 92,waliojitokeza katika zoezi hilo ni watu 24,422 ambapo kura halali zilikuwa 24,047 na  kura 375 zikiharibika.

Wagombea waliokuwepo wakati wa kutangaza  matokeo katika uchaguzi huo na kusaini fomu ya kukubalina na matokea alikuwepo mgombea wa NRA na CCM pekee.

Aidha Wakizungumza baada ya kupokea matokeo hayo aliyekuwa mgombea wa chama cha NRA pamoja na Ridhiwani Kikwete kupitia CCM,kila Mmoja ameshukuru wananchi na kuahidi kushirikina na wananchalinze kuleta maendeleo.

JOYOUS CELEBRATION YAVUNJA REKODI AFRIKA YA KUSINI


Kundi la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini limevunja rekodi ya kuwa kwaya ya kwanza nchini Afrika ya kusini kushika nafasi ya kwanza kwenye mtandao wa kuuza muziki wa iTune kupitia album yake mpya ya 18 iitwayo 'One Purpose' ambayo imetoka rasmi jana kupitia mtandao huo.

Album hiyo ya Joyous ilianza kupigiwa debe kwenye mtandao wao wa Facebook mapema wiki mbili zilizopita kwa watu kulipia kabla ya siku yenyewe rasmi kutoka, ambapo iTune kwakushirikiana na kundi hilo waliweka shindano kwa mashabiki wa kundi hilo kueleza kwanini wanahamu na album mpya ya kundi hilo, ambapo mshindi anajinyakulia kadi ya manunuzi ya iTune ambayo inamwezesha mshindi kununua nyimbo mbalimbali katika mtandao huo kwakiasi cha kadi yake.

Album mpya ya Joyous itakuwa na nyimbo 39 kwa maana ya CD tatu za kusikiliza huku pia ikitegemewa kwamba kutakuwa na DVD mbili kama ilivyokuwa kwa toleo lao la 15 ambalo lilikuwa na sehemu ya kwanza na ya pili. Joyous ni kundi ambalo tayari limejijenga nchini Afrika ya kusini na kupendwa nje ya mipaka ya nchi hiyo tangu kundi hilo kupitia mwimbaji wake kutoka Nigeria mwenye uraia wa Afrika ya kusini pia mchungaji Agu Uchechukwu ama Uche double double kuimba wimbo wa 'My God is good' ambao ulifungua mipaka ya kundi hilo kufahamika zaidi duniani, kazi ambayo pia inaendelezwa na Mzimbabwe Mkhululi Bhebhe ambaye nyimbo zake na Uche zimetokea kupendwa na kutizamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kuliko waimbaji wengine wa kundi hilo.

NYOTA WA MUZIKI WA INJILI NCHINI KENYA AFARIKI DUNIA


Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Kenya aliyetamba na wimbo wa 'Kiburi ni chanini' aitwaye Peter Kahura Kaberere amefariki dunia baada ya kupigwa shoti ya umeme akiwa kwenye eneo lake la kusafisha magari siku ya jumapili.

Mwimbaji huyo ambaye pia alikuwa meneja wa kampuni ya Mo Sound Limited ambayo pia inasimamia tuzo maarufu za nchini humo za Groove, alipatwa na umauti wakati akisafisha gari lake tayari kuelekea kanisani eneo la Lower Kabete lakini kukawa na hitailafu ya umeme kwenye mashine ya kuoshea gari  ambayo ilisababisha umeme huo kumkausha na kukutwa sakafuni na mkewe akiwa amekufa.

Taarifa za kifo cha mwimbaji huyo zilitolewa na mkewe kupitia ukurasa wa Facebook wa mwimbaji huyo na kufuatiwa na salamu mbalimbali za rambirambi kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wapenzi wa muziki wa injili. Taarifa hizo ziliendelea zaidi kupitia ukurasa wa Facebook wa tuzo za Groove ambao pia ujumbe wao uliandikwa kuonyesha ni kwa jinsi gani wamehuzunishwa na kifo cha mwimbaji huyo

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog