John
S. Shabani ni mzaliwa wa kijiji cha Kirando katika kitongoji cha
Nyankima, kata ya sunuka, Wilaya ya Kigoma Vijijini, Nchini Tanzania. Ukoo
wake ni waumini wazuri wa dini ya kiislam (Islamic Religion).
Baada
ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi kirando, alijiunga na elimu
ya sekondari, lakini kutokana na itikadi za kidini, alijikuta akiwa katika
wakati mgumu wa kupigwa vita na wazazi, ni baada ya uamuzi wake wa kujiunga na
Dini ya kikristo. Hivyo John ameishi miaka mingi akiwa mbali na wazazi wake,
lakini hata hivyo hakukata tamaa.
Mwaka
1992, John akiwa kijana mdogo, alipata ufadhili wa kwenda nchni Kongo (Zamani Zaire), ambako huko alijifunza muziki na kusoma
Chuo cha Biblia (Bible knowledge), na huko kipaji chake cha kutunga nyimbo na
kuimba kilijitokeza kwa kasi, hata akatokea kupendwa sana.
John
hakutaka kuona mtu yeyote akiwa katika hali ya kukata tamaa, maana alifahamu
madhara yake. Kwasababu hiyo, alianzisha vikundi mbalimbali vya vijana akiwa na
lengo la kuwaelimisha ili kujikwamua katika hali ya kukata tamaa na
kutokujihusisha na vitendo viovu kama madawa ya kulevya, Ukahaba na anasa za
kila aina, mambo ambavyo aliyapiga vita sana.
John
ameishi miaka mingi kama yatima, lakini hali
hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kuwa na tabia njema, kumheshimu na
kumthamini kila mtu, mambo yaliyompelekea kupata kibali machoni pa wengi hata
kuwa mfano wa kuigwa. Amekuwa msaada kwa Vijana wengi (Ndani na nnje ya nchi)
na kuwakwamua wengi waliokuwa wamekata tamaa na kujihusisha na vitendo viovu.
Pia kutokana na ujuzi wa muziki alioupata na pia kipaji kikubwa alichonacho cha
kutunga, kuandika nyimbo na kuimba, John amekuwa msaada kwa waimbaji mbalimbali
binafsi na vikundi ndani na nje ya nchi, hasa nyimbo za Injili. Ni mwalimu bora
na mshauri kwa waimbaji. Wengi waliopitia kwake sasa ni waimbaji wazuri na
maarufu.
Mwaka
2001 John alifunga pingu za maisha na binti aitwaye Debora Shabani na mwaka
2002 walipata mtoto wa kike. Alimwita mwanaye Joyce, akiwa na maana ya
kuyasahau maisha ya huzuni na shida na kujitabiria maisha ya furaha.
Mwaka
2004, John aliajiriwa katika kampuni ya Msama promotions ya jijini Dare
es salaam, kampuni inayojihusisha na kuinua vipaji na pia kuwainua vijana na
watu wa rika na jinsia zote waliokata tamaa ya maisha n.k, na hasa wale walioko
vijiweni wakijihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba n.k. Kampuni hiyo
imewasaidia Vijana wengi na Jamii kwa ujumla, na wengi wamejikomboa kimaisha
Tarehe
19/03/04, John alirekodi Album yake aliyoiita “Marufuku kukata tamaa”
Album
ambayo imewasaidia wengi waliokata tamaa na kuwapa matumaini mapya. Album hiyo
na nyingine alioirekodi mwaka 2009 inayoitwa “Huu ni wakati wangu”,
zimekuwa msaada mkubwa kwa kila aliye au anayezinunua, zimegusa na kuinua mioyo
ya watu wengi. Kwani amepokea shuhuda nyingi ndani na nnje, hata za wale
waliodiriki kujiua, lakini baada ya kusikiliza nyimbo hizo waliahirisha. “Nakusii
nunua kanda hizo, naamini zitakusaidia”. Pia utakuwa mchango wako kwa
kutimiza ndoto na malengo ya John.
John
ametembelea nchi mbalimbali, akijifunza maisha ya watu. Amegundua kwamba karibu
asilimia kubwa ya wanadamu, awe maskini, tajiri, msomi au asiye na elimu, wenye
vyeo au waajiriwa, watoto kwa wakubwa, wanaume kwa wanawake, awe mzungu au
mweusi n.k, wote kwa njia moja au nyingine wamepitia katika hali ya kukata
tamaa au kukatishwa tamaa na jambo fulani, mtu, watu, hali au mazingira fulani.
Ndipo mwaka 2006, alipata maono na msukumo mkubwa wa kuandika Kitabu ambacho
kitakuwa msaada kwa njia moja au nyingine kwa kila atakayekipata.
Tarehehe
11/7/08 ni siku ambayo John hawezi kuisahau. Siku ya huzuni na majonzi, siku ya
kilio na kuomboleza. Ni siku alipofariki mke wake mpendwa na mwimbaji maarufu
wa muziki wa Injili, Debora Shabani, mwimbaji aliyegusa mioyo ya watu
wengi ndani na nnje ya nchi, mwimbaji ambaye msiba na mazishi yake
yalihudhuriwa na maelfu ya watu, wakiwepo Maaskofu, Wachungaji, Waimbaji
binafsi, Kwaya pamoja na viongozi mbalimbali wa serekali. Hata hivyo, John
hakukata tamaa.
Tarehe
26.04. 2009, John alitunukiwa tuzo ya heshima pamoja na cheti (certicate of
appreciation) kwa kutambua mchango wake kwa ajili ya kuinua vipaji na pia
kuchangia kuinua muziki wa Injili Afrika mashariki na kati. Pamoja na hayo
amekua akianzisha makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu maisha ya
kujitegemea, kujishughulisha na kuhepukana na vitendo viovu kama wizi,
ujambazi, utumiaji madaswa ya kulevya, ukahaba n.k. Tuzo hiyo ilitolewa na
kampuni moja maarufu Tanzania
yenye makao makuu jijini Dar es salaam
(Christian promoters Ltd).
John
ameanzisha huduma inayoitwa Never give up “Usikate tamaa” Ambayo
anategemea kuisajili wakati wowote. Huduma hii, inalenga kuinua vipaji, mipango
na mbinu za kuwakwamua vijana au watu kujihusisha na madawa ya kulevya,
ukahaba, utapeli wizi, ujambazi nk, mambo yanayosabisha magonjwa kama vile ukimwi, kufungwa jela au kufa kabla ya
wakati, matokeo yake kuacha wototo wengi yatima na wajane nk. Pia kutafuta
ufadhili kwa ajili ya kuaendeleza vijana ki-elimu pamoja na kuwawezesha pale
inapobidi. Kwa sasa anayo program inayoitwa Touching voice program
(Darasa la uhimbaji)
Ni
kwa ajili ya kwaya, Band/vikundi na waimbaji binafsi
0 comments:
Post a Comment