ASKOFU MKUU WA PGC AKIMIMINIWA MAFUTA TAYARI KWA KAZI YA BWANA. |
ASKOFU MKUU WA PGC KULIA AKIWA NA ASKOFU MKUU WA EAST AFRIKA PAMOJA NA MAMA ASKOFU ALPHONCE NKANGA. |
Baadhi ya wageni waalikwa wakishuhudia tukio likiendelea la kusimikwa kwa askofu NKHANGA
Baadhi ya waumini wakimpongeza mama askofu mkuu wa kanisa la PGC Tanzania.
NA denis nyali iringa.
Askofu
mkuu wa kanisa la PENTECOSTE GOSPEL CHURCH TANZANIA ALPHONCE KHANGA amewataka
wachungaji kuwa waaminifu katika kazi ya MUNGU ili kuitenda kazi yake kwa
ufasaha .
Akizungumza
mara baada ya kusimikwa kuwa askofu mkuu wa Tanzania wa kanisa hilo amesema kwa
sasa watumishi wengi wamekuwa si waaminifu katika kuitenda ya mungu hali
inayopelekea wote kuonekana kuwa hivyo na kushindwa kuifanya kazi ya mungu.
NKHANGA
ameongeza kuwa si jambo la hekima kwa wachungaji kuandikwa na kuripotiwa na
vyombo vya habari kwa kwa matendo ambayo hayambariki mungu bali waandikwe kwa
kuihubiri injili na kuokoa roho za watu zilizopotea.
Kwa
upande wake askofu mkuu wa kanisa hilo afrika mashariki ZAKHARIA KALANJE
amewasihii wachungaji kujiendeleza kimasomo ili kuendana na kasi ya mabadiliko
ya dunia kwa kuwa mungu si wa watu wapumbavu.
Tukio
hilo la kusimikwa askofu mkuu wa Tanzania limefanyika katika ukumbi wa new life
in Christ wilolesi na kuhudhuria na viongozi wa dini ,vyama na serikali.