KANISA LA WINNERS CHAPEL LA MAMILIONI LIPO KATIKA HATI HATI YA KUBOMOLEWA NA SERIKALI
![[Image]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfZG0RQUZvZqDEUIyhsFWevR1spS0CcmCGQFPSneyU9zTRXntraFyDOB5IhtUAfMi39WNQmMzlVpGG-fFA2owM7uoO4uACDt20GLdgiXiT71YdBXyWZo9Dje3sRD3Wj7vhkdGsLEHmGRk/s3200/Ha-win.jpg) |
Winners Chapel la jijini Nairobi muonekano wa ndani. |
Kanisa kubwa la kisasa la Winners Chapel la jijini Nairobi nchini Kenya
liko kwenye hati hati ya kubomolewa na serikali ya nchi hiyo, kwa madai
ya kiwanja lilipojengwa kanisa hilo ni mali ya serikali na kwamba kanisa
hilo lilifanya makosa kujengwa mahali hapo.
Kanisa hilo lenye uwezo wa kubeba waumini elfu kumi na wanane (18,000)
kwa wakati mmoja ambalo ujenzi wake umechukua miaka tisa hadi kukamilika
kwake likiwa limejengwa eneo la south B estate huku likitajwa kuwa ni
moja kati ya makanisa bora kujengwa Afrika mashariki na kati liko chini
ya kanisa mama la Winners Chapel lenye makao makuu yake nchini Nigeria
chini ya kiongozi na mwanzilishi wake mchungaji David Oyedepo anayetajwa
kuwa mmoja kati ya watumishi wa Mungu matajiri duniani.
![[Image]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3jWDITUEQBS1NEvSpdruSx_ug6qgVqTHQDUhrCaEtGI6ho2WE9z8O6rfllBkjwHFppTiap8jAJ6iniRaRCYCy1NGOlHQDvO8w4P_jOWU_A5sAFLdg6qQWRSqugOBU5rI3FPZ_o04pNWI/s3200/jcbiJjx.jpg) |
Winners Chapel la jijini Nairobi nchini Kenya, katika muonekano wa nje.©skyscrapercity |
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya nchini Kenya vinasema
kwamba katibu mkuu wa kilimo, ufugaji na uvuvi wa kenya bwana Felix
Kosgey amesema serikali itatoa siku 21 kwa wamiliki wa nyumba hizo
katika kiwanja cha diamond park ambacho kimejengwa nyumba mbalimbali za
kifahari pamoja na south B ambako kumejengwa kanisa hilo kuondoka ili
zibomolewe tayari kwa matumizi mengine ya serikali.
Kiwanja hicho chenye jumla ya ekari 210 kimezua mzozo na kufikia wakazi
wake kufika ofisini kwa meneja mradi wa nyumba hizo Ahmed Rashid ili
kupata ufafanuzi juu ya kauli iliyotolewa na bwana Kosgey. Ambapo kwa
mujibu wake meneja huyo amesema toka kutolewa kwa kauli hiyo wamekuwa
katika wakati mgumu kutoka kwa watu hao na wengine wakipiga simu kutoka
nje ya nchi wakiulizia uhalali wa eneo hilo ambalo amesema lina nyumba
zipatazo 600 ambazo zipo katika eneo hilo kwa miaka 10 sasa huku kila
nyumba ikiwa inathamani ya shilingi milioni 16 za Kenya huku wengine
wakiwa wamiliki na wengine wapangaji katika nyumba hizo.
![[Image]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiwPxXxLfmN9Q8nemUsk_gm8MFpG-EqIghu9myI2cCUXsBgSUoejrTz5-uBAAa5lvqz3FlRVQ8mlBlOz65scBGqSJYsFlECgsBbGwfqL89kibUpwiwnqjaY3YMBMtt8QJkU5OZ5LNyLgDA/s3200/A1.jpg) |
Mchungaji
Oyedepo katikati na mkewe sambamba na makamu wa Rais wa Kenya bwana
William Ruto wakikata keki wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo ambalo lipo
katika hatihati ya kubomolewa.©gadiola25 |
Kwa upande wa mmoja wa wachungaji wa kanisa la Winners ambaye hakupenda
jina lake litajwe kwakuwa si msemaji wa kanisa ameiambia Nairobi news
kwamba kabla hawajaanza ujenzi wa kanisa hilo waliwakilisha nyaraka zote
muhimu kwa vyombo husika.
![[Image]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEheCBZs8VM0KtwbMXMfwvveo-WxKYPYxeClfOxuChu6cyvCP-bKGZMge0f7r0bbulr-gujM3xGVM7QdJO87Jyp0jAxMmc_qYDr92755Nkk7R4tt6-0N7eG-N0YJbN10Z7F5CkgH39MoD9Q/s3200/editor386536655396385674-598x350.jpg) |
Nyumba ambazo zipo katika hatihati ya kubomolewa katika eneo la Diamond Park jijini Nairobi ©nairobinews |
![[Image]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjlulWSGrIyiBKcr6kDcpuW3Ty1zzkDuWuClz3eC8RN_elObVUwwCB7Iq0zGavF-ByMi9RwXqqXdkc8G06wP4IP0ppBognt8zbNW-uc-vC1tlJQe2J-f893kw1McEnIAP8bR2tX06WeeVc/s3200/article-2220833-1599471C000005DC-646_634x417.jpg) |
Moja ya ndege ya kifahari ya kiongozi wa kanisa la Winners duniani David Oyedepo.©dailymail |
![[Image]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdwNKb9K0K1itUh20jiDjz8zw6SM25pt02DN84Vo6yUwf_5EUT5igpcmvEqd1cfy9F3hPMzx4LieIeFHONK1NsverTsRsSn5CVuhEMkNBXS7n9H-m9GN4b0DEr_nzJPBsOKkFG8w6iMp4/s3200/article-2220833-15994F14000005DC-51_634x416-1.jpg) |
Mchungaji David Oyedepo akiwa ndani ya ndege yake, akifurahia jambo.©dailymail |