HAYA NDIO MATUKIO MUHIMU YA PAPA BENEDICT XVI
Papa Benedict wa 16, ameainisha wazi kuwa anastaafu uongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani mwishoni mwa mwezi huu, na hivyo kutoa nafasi kwa mchakatow a kumpata Papa mpya kuanza.
Yafuatayo ni matukio muhimu katika maisha yake, kama ambavyo GK imeyakusanya kwenye mtandao.
April 16, 1927: Kuzaliwa kwa Alois Ratzinger huko Marktl am Inn, Ujerumani, mtoto wa mwisho wa Joseph na Maria Ratzinger.
1943 - 1945: Amekuwa msaidizi wa majeshi ya ulizni nchini Ujerumani,
kikosi cha kuzuia mashambulizi ya anga na askari wa miguu. Alifungwa
jela mwaka 1945 kwenye kambi ya Wamarekani kwenye mji wa Neu Ulm,
Bavaria, Ujerumani.
Juni 29, 1951: Akasimikwa rasmi sanjari na kaka yake, Georg Ratzinger huko Freising, Bavaria, Ujerumani.
1969 - 1977: Akawa Professa katika Chuo Kikuu cha Regesnburg, kilichopo Bavaria, huko huko Ujerumani.
Novemba 25, 1981: Akateuliwa kuwa kiongozi mkuu kwenye kusanyiko la
kiimani linaloongozwa na Papa Yohane Paulo wa pili, na hatimaye kuchukua
nafasi hiyo ilipofikia Machi 1892 akaichukua rasmi nafasi hiyo.
Aprili 2, 2005: Papa Yohane Paulo II anafariki dunia, siku sita baadae,
yaani Aprili 8 2005, Ratzinger akiwa kama 'dean' wa chuo cha
makardinali, anasimamia msiba wa Papa.
April 19 2005: Ratzinger anachaguliwa kuwa Papa wa 265, katika mkutano
wa siri ambao ulifanyika haraka kuliko yoyote iliyowahi kufanyika, siku 5
baadae, yaani Aprili 24, 2005, anasimikwa rasmi mbele ya umma.
Agosti 18-21, 2005: Afanya safari yake ya kwanza, atoka kwenda siku ya
vijana duniani, Cologne, Ujerumani. Septemba 24, 2005: akutana na
mwanazuoni mpinzani wa utawala katika makazi yake ya kipindi cha
kiangazi, na Disemba 25, 2005: Akasaini waraka wa kwanza kwa viongozi wa
makanisa, ujumbe ukisema, "Mungu nu Pendo", na ukasambazwa Januari 25,
2006.
Mei 28, 2006: Katika safari yake Poland, kambi ya Auschwitz, kambi
mojawapo zilizokuwa za kutesea mateka wa kivita, hasahasa Wayahudi. Na
Septemba 12, 2006: wakati anatembelea Ujerumani, akatoa hotuba katika
chuo kikuu cha cha Regensburg ambapo ilizua hasira kwa Waislamu, kwa
kunukuu kiongozi mmoja wa Byzantine, ambaye alihusisha mafundisho ya
Mtume Muhammad kama uovu na kinyume na ubinadamu, hasahasa "amri yake ya
kuezeza kwa upanga imani"
Aprili 16, 2007: Toleo la kwanza la "Yesu wa Nazarethi" lakamilika
kwenye sherehe yake ya kuzaliwa ya umri wa miaka 80. Kikatolewa Aprili
13, na ilipofika Mei 27, 2007 akasaini barua kwa Kanisa Katoliki nchin
China, akiwataka kuungana chini ya mamlaka yake, ikachapwa Juni 30.
Julai 7, 2007: Akaondoa vizingiti katika kusheherekea siku ya Umma ya
Latin. Aprili 20, 2008: katika safari yake nchini Marekani, akawaombea
wahanga wa shambulio la ugaidi la Septemba 11, 2001.
Julai 19, 2008: Wakati akiwa safarini Australia, kwa ajili ya siku ya
vijana duniani, akakutana na wahanga walioingiliwa kimaumbile na
viongozi wa kidini, na akawaomba msamaha kwa kutaabika kwao. Januari 21,
2009: akaongeza adhabu ya kuwatenga maaskofu wanaopinga kuwa kulikuwa
na mateso kwa wakristo na Wayahudi kutoka kwa askari wa utawala wa
Hitler. Maaskofu hawa ni Richard Williamson na wengine watatu. Lakini
Januari 24, akaondoa adhabu yake.
Machi 10, 2009: Akubali makosa ya kwenye suala la Williamson, na kusema
kuwa ni lazima Vatican watumie vizuri vyombo vya mitandao ili kuepusha
utata kwenye jamii. Barua ikatolewa Machi 12 - Machi 17, 2009 akiwa
njiani kwenda Cameroon, akawaambia waandishi waliokuwepo kwenye ndege,
kuwa kondom sio suluhisho la UKIMWI, na kwamba linaweza kuleta madhara
zaidi, jambo ambalo likazua kukosolewa.
Mei 11, 2009: Akitembelea Mji Mtakatifu, akaweka taji la maua kwenye
kumbukumbu ya Yad Vashem, na kusema kuwa wahanga wa mauaji ya halaiki
"wamepoteza maisha yao, lakini hawatopoteza majina yao kamwe."
Juni 29, 2009: waraka wa tatu kwa viongozi wa dini wasainiwa, "Sadaka katika Kweli", na kutolewa Julai 7, 2009.
Julai 17, 2009: Akavunjika mkono wa kuume alipoanguka usiku kwenye nyumba yake ya kipindi cha kiangazi.
Okotba 20, 2009: Vatican yatangaza kuwa Papa amerahisisha kwa Waanglikana kubadili na kujiunga na Katoliki.
Machi 19, 2010: Akawashukia maaskofu wa Ireland kwa kushindwa kutoa
hukumu nzuri katika kesi iliyohusu unyanyasaji kwa watoto, bila kueleza
majukumu ya Vatican kwenye suala hilo katika barua iliyotlewa Machi 20.
Mei 1, 2010: Aamuru mabadiliko makubwa ndani ya Jeshi la Kristo baada ya kubaini kuna ubadhilifu kwa aliyeanzisha
Septemba 16-19, 2010: Karika safari yake ya kwanza ya kitaifa
kuitembelea Uingereza, akutana na Malkia Elizabeth II, Askofu Mkuu wa
Canterbury, Rowan Williams na kutangaza utakatifu kwa John Henry Newman
wa Anglikan.