Wito umetolelewa kwa wanafunzi wanao hitimu kidato cha nne hapa nchini kuweza kuendeleza nidhamu zao hata baada ya kuhitimu kwani hiyo ndo njia pekee itakayowawezesha wanafunzi kufaulu na kukamilisha malengo yao ya hapo baadae.
Wito huo umetolewa na Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania assemblia of god Dr Barnabas Mtokambali katika mahafali ya tatu ya kidato cha nne ya shule ya seminary ebenezer iliyopo nduli jirani na uwanja wa ndege manispaa ya iringa.
Ambapo mbali na maafari hayo Askofu Mtokambali aliweza kuzindua rasmi maabara ya kisasa itakayo wasaidia wanafunzi wote wanaosoma masomo ya sayansi Mtokambali alisema iwapo wanafunzi watafuata nidhamu waliyofundishwa na kuionyesha katika jamii zao hakika hakutakuwa na mwanafunzi wa kufeli hata mmoja kwa anaamini kuwa nidhamu ndio chanzo kikuu cha mafanikio.
Hata hivo alimpongeza mwalimu mkuu wa shule hiyo bw.makweta na kuaahidi kusaidiana katikachanga moto mbalimbali zinazohusu shule hiyo kama tatizo la maji ambapo askofu mkuu aliahidi million mbili katika kufanikisha na kutatua jambo hilo, na zaidi ya millioni sita zilichangiashwa katika kutatua sual;a la maji .
Kwa upande wake mkuu wa shule ya ebenezer alimpongeza askofu mkuu pamja na uongozi wa jimbo la iringa uliongozwa na Askofu Jonas Mkane pamoja na makamu wake Edward Tom Matipa kwa uwepo wao katika kufanikisha zoezi zima la mahaafari pamoja na uzinduzi wa maabara ya kisasa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
|
Askofu mkuu wa tanzania assemblis of god wakati akiwasili katika shule ya ebenezer |
|
Askofu mkuu wakati akizindua rasmi maabara ya kisasa |
|
Asikofu wa jimbo la iringa jonas mkane akifungua kwa maombi sherehe |
|
makamu askofu wa jimbo la iringa rev edward tom matipa |
|
baadhi ya majengo ya shule ya ebenezer seminary |
|
wahitimu wakicheza kwaito kwa pamoja |