UKATILI WA KUTISHA TIZAMA HABARI UJIONEE INASIKITISHA SANA
Posted by Unknown
Posted on 8:02 AM
with No comments
Posted by Unknown
Posted on 3:54 PM
with No comments
DAS JOSEPH CHINTIKA: ISMANI HAKUNA NJAA
Na Fredy Mgunda,Iringa
KATIBU tawala wa wilaya ya Iringa
Joseph Chintika amesema kuwa tarafa ya ismani haina njaa kama ambavyo maneno
yanayozagaa mitaani kuwa ukanda wa ismani kuwa kuna njaa.
Akizungumza na blog hii
Chintika alisema kuwa kumekuwa na wanasiasa wanaoeneza kuwa tarafa ya ismani
kuna njaa wakati hali halisi sio hiyo na kuongeza kuwa eneo hilo linachakula
cha kutosha na hakuna tatizo la njaa.
“Angalia mvua zinanyesha kwa
wingi na wananchi wamelima kwa wingi na mazao yanakuwa vizuri hivyo ismani
hakuna njaa na sijapokea taarifa yoyote ile ya kuwepo kwa njaa kwa kuwa
nimekuwa nikifanya ziara katika maeneo hayo mara kwa mara na nimejihakikishia
kuwa hakuina njaa hali ya chakula ni nzuri na kuwaomba wananchi kuacha
kuwasikiliza wanasiasa”.alisema Chintika
Chintika aliwataka wananchi
kuacha kutumia mazao ya mahindi,mtama na uwele kupikia pombe kwa kuwa kufanya
hivyo kutapunguza uwepo wa chakula katika eneo hilo.
Unakuta mtu anashawishiwa
kuuza mahindi kwa mpika pombe wakatyi anajua kuwa hana chakula cha kutosha
nasema ni marufuku kwa wananchi kupika pombe kwa kutumia mahindi,uwele na mtama
ili kuendelea kutunza chakula hicho.
Aidha Chintika alisema kuwa
sasa ni fursa kwa wafanyabiasha kuuza mahindi katika maeneo mbalimba ya wilaya
ya iringa kwa kuwa bei ya mahindi kwa sasa ni nzuri.
Hivi hawa wanansiasa
wanayatoa wapi maneno ya uongo kuwa ismani kuna njaa naomba waje na takwimu na
sio kuposha wananchi serikali ndio inaweza kutangaza kama sehemu kuna njaa na
sio mtu mwingine yoyote.
“Serikali ndio chombo cha
mwisho kuthibitisha kuwa ismani kuna njaa sio kila mtu anaweza kuongelea mambo
ya serikali naomba hawa wanansiasa waache mara moja kupotosha wananchi na
wakiendelea kupotosha jamii tutawachukulia hatua za kisheria maana hatuna
tatizo la chakula katika tarafa ya ismani”.alisema Chintika
Posted by Unknown
Posted on 3:52 PM
with No comments
AUAWA KWA KUTENGANISHWA SHINGO NA KIWILIWILI NA KUTOMEA NA KICHWA KUSIKOJULIKANA
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo
Na Fredy Mgunda,Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya iringa kuacha tabia ya kuamini na
kujihusisha na maswala ya imani za kishikina pamoja na kujichukulia hatua
mikononi.
Ameyasema hayo baada ya
kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mikong’wi kata ya
kihologota wilaya ya iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na
kutelekeza kiliwili chake.
“Kwanini watu wajichukulie
hatua mkononi wakati serikali,jeshi la polisi,mahakama,makanisa na misikiti
huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote
na haya mambo ya kishikina serikali haiamini da nasikitika sana kwa
tukio la leo ni baya sana”alisema Kasesela
Kasesela alisema kama wilaya
wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia
sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la
polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.
“Wilaya ya Iringa ilikuwa
imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa keli lazima jeshi la polisi lifanye
uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha mikong’wi na
lazima tukomeshe na kuwa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina
kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela
Kasesela ameeleza kuwa tukio
hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni hasani
nyalusi mkazi wa kijiji cha mikong’wi tarafa ya Isman mkoani Iringa.
Aidha Kasesela amewaomba
viongozi wa dili mbalimbali kutoa elimu ya mungu na kukemea maswala ya
kishikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji cha Mikong’wi Majorino Muyinga Anaeleza kuwa Mnamo tarehe 06/04/2017 huko kitongoji cha Utitiri kijiji cha Mikong’wi kata ya Kihorogota tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa vijijini Mkoani Iringa alisema kuwa Hassan Nyalusi alikutwa akiwa ameuawa nje ya nyumba yake na mtu/watu wasiofahamika na mwili ukiwa hauna kichwa na uchunguzi wa daktari umefanyika na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehehemu kwa taratibu za mazishi laiki mtu mmoja Jackson Nyalusi anashikiliwa na polisi kuhusishwa na mauaji haya,bado upelelezi unaendelea
http://www.malunde.com/2017/04/majambazi-watatu-waliovaa-hijabu-wauawa.html
Posted by Unknown
Posted on 10:55 AM
with No comments
Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kukaidi amri ya kutakiwa kusimama eneo la kizuizi cha Mwembe Muhoro wilayani Rufiji, mkoani Pwani.
Watu hao walikuwa wamepakiana kwenye pikipiki moja huku wakiwa wamevaa hijabu.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pikipiki nyingine mbili zilifanikiwa kukimbia.
Akielezea juu ya tukio hilo alifafanua,lilitokea Aprili 2 mwaka huu majira ya mchana ,Muhoro ,Rufiji barabara kuu ya Dar es Salaam Lindi.
“Siku ya tukio askari walipata taarifa kuwa kulikuwa na pikipiki tatu zikitokea Kibiti kwenda mikoa ya Kusini zikiwa zimebeba watu watatu kila moja “
“Miongoni mwa pikipiki hizo kati yake mbili wamebebwa watu waliovaa hijabu,” alisema Lyanga.
Alisema askari wa barabarani walipewa taarifa katika kizuizi cha Mparange na kuwasimamisha ili wawahoji lakini walikataa na kupita ambapo waliwajulisha wenzao kwenye kizuizi cha Ikwiriri lakini walikaidi kusimama.
“Baada ya hapo walifika kizuizi cha Ikwiriri lakini bado walikaidi kusimama na kuendelea kukimbia ndipo walipofika kituo cha Muhoro “
“Hata hivyo hawakusimama na askari waliokuwa doria wakiwa kwenye gari waliwafuatilia na wakavuka daraja la Mkapa na waliwapa onyo kwa kupiga risasi hewani,” alisema Lyanga.