Watoto Wanne wa Familia Moja Wateketea Kwa Moto Wakiwa Usingizini

HUZUNI imetanda katika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, baada ya ajali ya moto wa kibatari kuteketeza watoto wanne wa mama mmoja, waliokuwa wamefungiwa chumbani na dada anayewalea.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika mtaa wa Nyerere, mji mdogo wa Kibaigwa wilayani Kongwa, wakati mama wa watoto hao aliposafiri kwenda shambani Kiteto mkoani Manyara, kwa ajili ya kuvuna mazao na kuwaacha watoto wake mikononi mwa dada, aliyekuwa akimsaidia kuwalea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema chanzo cha ajali hiyo ni mlipuko wa kibatari kilichokuwa ndani ya chumba walicholala watoto hao, ambacho kilichoma godoro na kuteketeza nyumba yote.

Moto huo ulioanzia katika chumba hicho, umeelezwa kuteketeza nyumba yote ya vyumba sita iliyojengwa kwa tofali za udongo mali ya Nelson Mdachi.

Kamanda Mambosasa aliwataja watoto hao kuwa ni Elizabeth Nelson (11) mwanafunzi wa darasa la saba, Samweli Mdachi (7) anayesoma darasa la kwanza na Nase Mgomba (9) anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Miembeni na Peter Lema (9) mwanafunzi darasa la tatu shule ya msingi St Paulo.

Kutokana na ajali hiyo, Kamanda Mambosasa amewakumbusha wazazi wasiache watoto peke yao nyumbani kwa kuwa ni hatari kwani ajali ikitokea ni vigumu kuokolewa.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na majirani wa familia hiyo, zimedai kuwa mama wa familia hiyo alikwenda shambani kuvuna mazao katika wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara na kuwaacha watoto hao chini ya uangalizi wa msichana aliyefahamika kwa jina moja la Ester.

Kwa mujibu wa madai yao, ilipofika usiku Ester anayetajwa kuwa na jukumu la kulea watoto hao, alitoka na kwenda kusikojulikana huku akiwafungia watoto hao kwa nje.

Mkazi wa Kibaigwa, Denis Luhunga, alipozungumza na mwandishikuhusu ajali hiyo alidai kuwa kibatari kilipolipuka, kilisababisha godoro kushika moto na kuteketea kwa watoto hao. 

“Aliwafungia watoto ndani akaacha kibatari kinawaka, baada ya kulipuka moshi mwingi ulijaa ndani,” alidai Luhunga.

Kuhusu alipo baba wa familia hiyo, mkazi mwingine wa eneo la tukio hilo, Paulo Sauli alisema baba wa watoto hao, aliyemtaja kwa jina la Nelson Mdachi, alishakufa miaka mitatu iliyopita na jukumu la kuwalea aliachiwa mama yao.

Alifafanua kuwa baba huyo ambaye wakati wa uhai wake alifahamika kwa jina maarufu la ‘Moja kwa moja’, alikufa baada ya kuanguka kutoka juu ya mti alipokuwa akirina asali na tangu hapo, jukumu la kulea likabaki kwa mama mzazi wa watoto hao.

“Tukio hilo limetusikitisha sana ni tukio baya maana wameteketea kabisa hajulikani nani ni nani,” alisema Sauli na kuongeza, “Hata Ester hafahamiki alipo, kuna watu wengi lakini tumemuangalia hapa msibani hatumuoni.”

Taarifa nyingine kutoka eneo la tukio, zilidai kuwa Mdachi alizaa na mama huyo watoto wawili na baada ya kufariki, mama huyo alizaa watoto wengine wawili na wanaume wengine.

Taasisi 680 Kufutwa.....Zipo za Kidini na za Kisiasa

WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), inakusudia kuzifutia usajili bodi za udhamini 680 za taasisi mbalimbali; ambazo zimekiuka masharti, ikiwa ni pamoja na kutokuwa hai.

Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe ameuruhusu wakala huo kuanza kusajili bodi za udhamini; huku akiutaka kuhakikisha bodi zitakazosajiliwa zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Akizungumza jana Dar es Salaam katika mkutano wa Bodi ya Wadhamini ya Rita, Dk Mwakyembe alisema, wakala huo unatakiwa kuzifuta haraka bodi hizo ili kuwepo na bodi chache ambazo ziko hai.

“Mmefanya kazi nzuri ya kuhakiki baadhi ya hizi bodi, endeleeni kuhakikisha tuna vyombo vichache ambavyo viko hai…kuna bodi kama 500 ambazo haziko hai na mnakusudia kuzifuta, zifuteni haraka,”alisema Dk Mwakyembe.

Alisema serikali imedhamiria kudhibiti mapato na ndio sababu katika mkutano wake na Bodi ya Rita alitoa agizo kwa wakala huo kusitisha usajili mpya wa wadhamini wa asasi, vyama, misikiti, makanisa na taasisi mbalimbali huku akitoa siku 90 wakala huo ukamilishe uhakiki wa bodi hizo.

Alisema baadhi ya vikundi hivyo ambavyo vingine vimekuwa vikiibuka wakati wa kampeni na uchaguzi vimekuwa vikitumika vibaya kupata misamaha ya kodi na vingine kuomba ruzuku.

Dk Mwakyembe alifafanua kuwa katika kikao chake na mamlaka zote zinazohusika na usajili wa vikundi vya kijamii, mashirika, kampuni na asasi mbalimbali ulikuwa na lengo la kuimarisha taratibu za usajili ili kudhibiti utitiri wa vikundi hivyo.

Aidha, alisema mkutano huo pia ulikuwa na lengo la kufanya maboresho kwa mamlaka hizo ili mifumo yao iweze kuwasiliana ili kulinda maslahi mapana ya Taifa. 

Awali Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Emmy Hudson alisema, tayari tangazo la kusudio la kuzifutia usajili bodi za wadhamini limeshaandaliwa na litatolewa muda wowote kuanzia sasa.

Alisema jumla ya bodi za wadhamini zilizosajiliwa ni 5,262 ambazo kati ya hizo zilizohakikiwa ni 1,544 na kwamba katika uhakiki huo walikumbana na changamoto ya malalamiko kutoka kwa bodi hizo kuwa nyingine ziko mbali.

Hudson alisema kati ya hao 5,262 ambao wako kwenye kanzi data ya wakala huo walichambua na kubaini walioko hai ni 4,287 pekee.

“Bodi za Udhamini 500 zimebainika kuwa haziko hai…zoezi la kuingiza taarifa kwenye databae (kanzidata) linaendelea lakini pia tunaomba tuongezewe muda au ikiwezekana liwe endelevu,” alisema.

Alisema kabla ya kuanza kwa uhakiki wa bodi hizo tayari walikuwa na idadi ya bodi 200 ambazo zilitakia kufutiwa usajili na zilipelekewa notisi za kufutiwa usajili wao ambapo kati ya hizo 20 tu ndizo zilizojibu na kuomba kutofutiwa usajili wao.

Hata hivyo, alisema wakala huo umekuwa ukikabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo za taasisi kumiliki mali bila kuwa na idhini ya bodi ya wadhamini kinyume cha sheria, muda wa kutembelea taasisi hizo kuwa mdogo, baadhi ya taasisi kubadili majina na anuani zao bila kutoa taarifa.

“Lakini pia tumebaini kuwepo kwa baadhi ya bodi ambazo hazitambui wajibu wao na pia mkanganyiko wa tafsiri ya sheria kutoka katika taasisi mbalimbali zinazoshughulika na usajili,” alisema Hudson.

Kazi kubwa zinazofanywa na bodi za udhamini ni kusimamia rasilimali fedha pamoja na uendeshwaji wa kampuni au taasisi husika.

DIWANI WA KATA YA NDULI ASHIRIKI MAENDELEO YA KUCHIMBA BARABARA NA KUREKEBISHA MAENEO KOROFI AKISHIRIKIANA NA WANAINCHI.



        PICHA ZA WAKAZI WA KIGONZIRE WAKISHIRIKI SHUGHULI ZA KIMAENDELEO.










Diwani wa kata ya nduli manispaa ya iringa wa kwanza katika picha akiwajibika kwa wanainchi.



mtangazaji wa nuru fm na mwakilishi wa efm na wapo radio akiwajibika pia  denis nyali mwenye tisheti ya njano.




NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog