Posted by Unknown
Posted on 9:53 AM
with No comments
Magereza yaaswa kuruhusu wafungwa kujiandikisha bvr.
JESHI
la Magereza nchini limeshauriwa kuhakikisha wanaruhusu wafungwa
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa
kielektroniki (BVR), unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Hatua hiyo ni kuwawezesha kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi katika uchaguzi ujao.
Rai
hiyo ilitolewa jana na Mratibu wa marafiki wa Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa, Noel Nnko wakati walipotembelea Gereza la Wilaya ya Same
na kutoa misaada mbalimbali kwa wafungwa ikiwemo utoaji wa elimu ya
kujiandikisha.
Nnko
alisema licha ya kutolewa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa
kujiandikisha katika daftari la wapiga kura makundi mbalimbali katika
jamii yamekuwa yakisahaulika ikiwemo wafungwa waliopo magerezani katika
maeneo mbalimbali nchini.
Alisema
kutokana na hali hiyo ni vema viongozi wa Jeshi la Magereza nchi
wakatupia macho suala hilo kwa kuhakikisha wafungwa wanaoruhusiwa
kujiandikisha katika daftari hilo wanapata haki hiyo kwa mujibu wa
sheria.
“Tumepitia
sheria tumejiridhisha kuwa wafungwa wasioruhusiwa kujiandikisha katika
daftari la wapiga kura na kupiga kura ni wafungwa waliohukumiwa vifungo
vya maisha na kifo.
“Hivyo
natoa rai yangu kwa viongozi wa magereza kutenda haki kwa wafungwa
wengine kwani kundi hili limekuwa halipewi kipaumbele katika masuala
mbalimbali ya kijamii,” alisema Nnko.
Katika
hatua nyingine, Nnko aliwataka wafungwa hao kuacha tabia ya kushabikia
viongozi wa kisiasa bali kujiandikisha katika daftari hilo hatua ambayo
itawawezesha kupata viongozi bora kwa ustawi wa taifa kwa ujumla.
Posted by Unknown
Posted on 9:50 AM
with No comments
Akina Mama Waandamana Kudai miili ya Waliouawa na Askari Kwa Kupigwa Risasi Mkoani Simiyu
KINAMAMA
kutoka Kata ya Bukundi Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, wameandamana
hadi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Erasto Sima, kushinikiza wapewe miili ya
vijana wao wawili waliouawa na askari Mei 29, mwaka huu.
Vijana
hao Gineu Gidahasi na Gitienga Gidahasi ambao ni ndugu wa familia moja
wanadaiwa kupigwa risasi na askari wa Kampuni ya ulinzi ya Mwiba Holding
kwa madai ya kuingiza mifugo eneo pori la makao ambalo kampuni hiyo
imewekeza.
Kinamama
hao walifika katika ofisi ya Mkuu huyo wa wilaya saa mbili juzi
asubuhi ambapo walilalamikia kitendo cha vijana wao kuuawa na kisha
miili yao kutoonekana na kumwomba Sima kuagiza kupatiwa miili hiyo ili
waweze kuifanyia mazishi na iwapo itashindikana watakwenda kwa Rais
Jakaya Kikwete kuomba msaada huo.
“Tumechoka
na manyanyaso kutoka kwa mwekezaji huyu, kilichotuleta hapa tunahitaji
tupatiwe miili ya vijana wetu tukaifanyie mazishi kwa heshima zote za
kabila letu na iwapo utashindwa kufanya hivyo basi tutakwenda Ikulu
tumuombe Rais Kikwete atusaidie,” alisema Udamulela Gitasori mkazi wa kijiji cha Lukale.
Walisema
hadi sasa zaidi ya vijana sita wameuawa tangu mwaka 2013 kwa madai ya
kuingiza mifugo katika eneo la pori hilo ambalo linapakana na vijiji vya
Mwabagimu, Lukale na Bukundi na hivyo wamekuwa wakiishi kama wakimbizi
ndani ya nchi yao.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Meatu, Meshack Opulukwa (Chadema), aliitupia lawama
serikali kwa kushindwa kulipatia ufumbuzi suala la wafugaji kuuawa kwa
kupigwa risasi na askari wa mwekezaji huyo licha ya kupatiwa taarifa na
hivyo alimwomba Sima kusitisha shughuli zinazofanywa na Mwiba hadi hapo
miili hiyo itakapopatikana.
Akijibu
malalamiko hayo kwa kifupi Sima alisema serikali wilayani humo
imeshaanza kulishughulikia suala hilo na tayari wote waliohusika na
mauaji hayo wameshakamatwa.
Posted by Unknown
Posted on 8:29 AM
with No comments
Lowassa Avunja Rekodi Mkoani Shinyanga.......Wananchi Waumizana Wakigombea Kumuona, Avuna Wadhamini 7,114
Mh.
Lowassa, akipokea fomu zilizojazwa na wana CCM waliomdhamini mkoani
Shinyanga, kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Shin yanga mjini Charles
Sangula, Juni 11, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh.
Edward Lowassa, akipungia mkono wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga,
alipokuwa akiondoka ofisi za chama hicho wilaya ya Shinyanga mjini mara baada
ya kupata wana CCM wa kumdhamini .
Mh.
Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, jana amevunja
rekodi ya kupata wadhamini 7,114, idadi ambayo ni kubwa kuliko
mgombea mwingine yeyete ndani ya CCM hadi sasa.
Furaha ya kumuona Mh. Lowassa, ilitawala ukumbi mzima
Wana CCM waliofika kumdhamini Waziri Mkuu wa
zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, wakishangilia wakati akiingia
ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga, wakisukumana ili wapate
kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa,
alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11,
2015, ili kuomba wanachama wenzake wa chama hicho wamdhamini.
Posted by Unknown
Posted on 6:39 AM
with No comments
Wakazi Wa Mgao Wamvaa Halima Mdee Kwa Kuwadhalilisha......Wamtaka Afute Kauli Yake
KUFUATIA
taarifa iliyotolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kuhusu utoaji wa ardhi kwa bilionea
Alhaji Aliko Dangote, wakazi wa kijiji cha Mgao, Halmashauri ya Mtwara
Vijijini wamemtaka kufuta kauli yake.
Wakitoa
malalamiko yao kwa vyombo vya habari, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho
ambao walijitambulisha kwa majina ya Seif Said na Mohamed Njiti,
walisema kuwa kitendo cha ardhi yao kulinganishwa na kaniki na kipande
cha kanga kimewasikitisha.
Walisema
uthamini wa ardhi umeshaanza, wanatarajia kulipwa Sh milioni 10 kwa
ekari moja, huku wakipata malipo ya mimea iliyopo kwenye mashamba yao,
zoezi ambalo bado linaendelea katika maeneo ya vijiji vya Kisiwa na
Mgao.
Kwa
upade wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abdulahman Shaha, alisema
amesikitishwa na taarifa iliyotolewa kwa kulinganisha ardhi yao na
kipande cha kaniki.
“Ile
kauli sio sahihi, ilibidi aje Mgao apate taarifa sahihi ili akatoe
bungeni, sisi tuko katika tathmini ya ardhi, kila mwananchi atalipwa
stahiki yake, walipaji wa ardhi hii ni Mamlaka ya Bandari Tanzania siyo
Dangote,” alisema Shaha.
Naye
Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Mtwara, Hebel Mwasenga, alisema
mamlaka hiyo inamiliki eneo la hekta 1,000, ambapo mwekezaji huyo
amepewa eneo la hekta 25 kwa ajili ya ujenzi wa bandari ndogo.
Posted by Unknown
Posted on 6:39 AM
with No comments
Mwanamke Atiwa Mbaroni Akituhumiwa Kumuua Mwanae Mchanga Kwa Kumtumbukiza Chooni
JESHI
la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Dainees Fredrick (30), mkazi
wa Kambi ya Raha, wilayani Hai, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mchanga
muda mfupi baada ya kumzaa kwa kumtumbukiza chooni.
Inadaiwa
kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho siku moja baada ya
kujifungua ambapo alimfunga mtoto huyo wa kiume kwenye kanga na kumweka
kwenye mfuko wa plastiki kisha kumtumbukiza chooni.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, katika taarifa yake
alisema tukio hilo lilitokea Juni 10, saa tatu usiku, Mtaa wa Kambi ya
Raha, ambapo waliofanikisha kukamatwa kwake ni majirani anaoishi nao.
Alisema
Rose Komely alisikia sauti ya kichanga kikilia ndani ya choo baada ya
kwenda kujisaidia, ndipo alipowaeleza wapangaji wengine na kwenda
chumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumkuta akiwa amekaa huku akiwa hana
ujauzito analalamika maumivu ya tumbo.
Ngonyani
alisema kuwa mtoa taarifa alimuacha mtuhumiwa akiwa na mwenzake kisha
kutoa taarifa kwa balozi Editha John ambaye alitoa taarifa kwa Jeshi la
Polisi.
Hata
hivyo, licha ya Jeshi la Polisi kufanikiwa kufika nyumbani kwa
mtuhumiwa huyo na kumtoa mtoto katika choo alichokuwa ametupwa tayari
mtoto alikuwa amekufa.
Mtuhumiwa
wa tukio hilo la mauaji ya kichanga anashikiliwa na Polisi na kwa sasa
anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Hai, huku
akiwa chini ya ulinzi akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Posted by Unknown
Posted on 6:37 AM
with No comments
Kortini kwa Kulawiti Mtoto
MKAZI
wa Mbezi Beach Dar es Salaam, Tuntutye Mwasyete (25), amefikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za
kumlawiti mtoto (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa mwaka mmoja.
Mbele
ya Hakimu, Lilian Rutehangwa, Wakili wa Serikali Masini Musa alidai
kwamba tukio hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu huko Kawe.
MIAKA HAMSINI YA UHURU WAKAZI WA VIWENGI IRINGA WALIA NA MAJI
Posted by Unknown
Posted on 8:56 PM
with No comments
MAGUFULI AENDELEA KUSAKA WADHAMINI....ISHU IKAWA KUZUNGUMZIA!!
Posted by Unknown
Posted on 12:53 PM
with No comments
Waziri
wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri ambaye pia ni miongoni mwa wagombea
waliochukua fomu za kuwania mbio za uraisi wa awamu ya tano amesema
hawezi kuthubutu kuzungumza chochote mbele ya hadhara ya wananchi katika
kipindi hiki kigumu cha kutafuta wadhamini na kwamba kufanya hivyo
nikukiuka maadili ya chama chake.