KWAYA YA FAITH IS ACTION T.A.G MLANDEGE IRINGA WAZINDUA ALBAMU YA DALADALA KWA KISHINDO HUKU MGENI RASMI AKITOA ZAIDI YA MILLION TANO.
Wa kwanza kushoto ni mama maona moja kati ya akinamama wanaoipendezesha kwaya hiyo kwa kucheza jana pia alivunja record ya kucheza.

bishop mkane pamoja na mkewe wakiendelea kufuatilia tamasha kwa umakini zaidi


RISALA KWA MGENI RASMI IKISOMWA NA KATIBU WA KWAYA DENIS KISITU




UMATI WA WATU ULIOFURIKA KATIKA UZINDUZI HUO



MGENI RASMI MWENYEKITI WA CCM MKOA BI JESCA MSAVATAVANGU AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI HUO.

Askofu wa jimbo la Iringa wa Jonas Mkane akimshukuru mgeni rasmi

Makamu askofu mchungaji Edward Matipa akiomba wakati wa kuairisha uzinduzi huo

 
                     KILA MTANZANIA ANADAIWA  600,000 SASA
 
Wakati Serikali ikibanwa na wabunge kwa kushindwa kutekeleza Bajeti ya mwaka 2013/14 kutokana na kutegemea fedha za wahisani, Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara imesema deni la taifa limeongezeka kwa Sh8.2 trilioni kwa kipindi cha miezi saba tu.

Ilisema jana kuwa hadi Juni, mwaka jana deni hilo lilikuwa Sh21.2 trilioni lakini hadi Januari mwaka huu, deni hilo lilipaa hadi Sh29.4 trilioni na fedha hizo zimekopwa kwa ajili ya kuendeshea warsha, semina, safari, mafunzo na matengenezo ya magari.

Akiwasilisha taarifa ya kambi ya Upinzani, Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia alisema ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi atakuwa anadaiwa Sh600,000.

Kati ya Sh5.8trilioni za bajeti ya Wizara ya Fedha mwaka 2014/15, Sh4.3trilioni zimetengwa kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa

Akiwasilisha taarifa ya Kamati, Mwenyekiti wake, Luhaga Mpina alisema Sh24.18trilioni ni deni la Serikali, Sh3.75trilioni ni deni la sekta binafsi na Sh1.15trilioni ni deni la Benki Kuu Tanzania (BoT).

“Ongezeko hili la deni haliendi sambamba na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ujenzi wa miundombinu ya uchumi. Hali hii inajenga hofu kuwa huenda deni hili limekuwa ni uchochoro wa ubadhilifu wa fedha za umma,” alisema Mpina.

Alisema licha ya Serikali mara kadhaa kueleza kuwa deni hilo ni himilivu, kuna viashiria vinavyoonyesha kuelemewa kwa taifa na mzigo mkubwa wa madeni.

“Mfano ni mapato ya ndani yamezidiwa na matumizi ya kawaida hivyo kuifanya Serikali kukopa hata kwa ajili ya warsha, semina, safari, mafunzo na matengenezo ya magari,” alisema Mpina.

“Deni la Taifa sasa limefikia asilimia 47 ya Pato la Taifa na kwa kipimo cha bei ya sasa deni la taifa limefikia asilimia 24, huku deni la nje pekee likiwa ni asilimia 19” alisema Mpina na kuongeza:

“Licha ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuahidi kwa muda mrefu kufanya ukaguzi maalumu wa deni la taifa, hadi sasa taarifa yake haijawasilishwa. Ni lini taarifa hiyo itawasilishwa bungeni ili kuwawezesha wananchi kufahamu undani wa jambo hili?” alihoji.

Kamati hiyo pia iliilipua Serikali kwa kuuza mashine za elekroniki (EFD), kati ya Sh600,000 hadi 700,000 kwa maelezo kuwa kiwango hicho ni kikubwa kwa mzunguko wa biashara ya mtaji wa Sh14 milioni kwa sababu mtaji wake hauzidi Sh5milioni.

Mpina alisema mashine hizo zinatakiwa kugawiwa bure kwa wafanyabiashara wenye kipato chini ya Sh40milioni na kufafanua kuwa chombo hicho chenye taarifa muhimu za mapato ya Serikali hakitakiwi kuuzwa na kufanyiwa matengenezo na mtu binafsi.

MAHAKIMU WA MAHAKAMA ZA MWANZO MUFINDI WAPEWA PIKIPIKI

Jaji Mary Shanghai akikata utepe wakati akikabidhi pikipiki hizo

Pikipiki zilizotolewa kwa mahakimu wa mahakama hizo
JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mary Shanghai amekabidhi pikipiki nne kwa mahakimu wa mahakama za mwanzo za Ifwagi na Kibao, Malangali, Kasanga na Mgololo, zote za wilaya ya Mufindi.

Kutolewa kwa pikipiki hizo, kumeelezwa na mahakimu wa mahakama hizo kwamba kutarahisisha utendaji kazi wao na kuongeza ufanisi katika idara hiyo muhimu ya utoaji haki.

Jaji Shanghai alikabidhi pikipiki hizo juzi katika ziara yake ya a kufahamiana na watendaji wa mahakama na kukagua shughuli mbalimbali za mahakama zinazofanywa wilayani humo.

Katika ziara hiyo, Shanghai alitembelea mahakamaa ya wilaya ya Mufindi na mahakama ya mwanzo Mafinga, Sadani, Mlangali, na Iramba.

Akisoma taarifa ya jumla ya mahakama ya wilaya hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi  Mfawidhi, Victoria Nongwa alisema mahakama hiyo inasimamia jumla ya mahakama za mwanzo zilizoko katika maeneo mbalimbali wilayani Mufindi.

Alizitaja mahakama hizo kuwa ni Mahakama ya Mafinga mjini, Mufindi (Kibaoni), Kasanga (Igowole) Malangali (Isimikinyi), Kibengu, Mapanda, Sadani (Utosi), Iramba (Itulavanu) Mgololo, Ihanu (Ibwanzi) na Ifwagi.

Alisema mahakama hiyo isiyo na mhasibu ina watumishi wa kada mbalimbali 31 ambao kati yao wanne ni mahakimu wakazi wa mahakama ya wilaya na watatu ni mahakimu wakazi wa mahakama za mwanzo.

Aliwataja watumishi wengine kuwa ni mahakimu watatu wa mahakama za mwanzo wasio mahakimu wakazi, mahafisa kumbukumbu watano ,wapiga chapa wawili, wahudumu wanne, walinzi nane na dereva mmoja.

Katika kuboresha utendaji wa mahakama hiyo, Nongwa ameomba msaada wa ujenzi wa mahakama ya mwanzo Ifwagi na ukarabati wa nyumba ya hakimu wake.

Wakati mjini Mafinga panatakiwa kujengwa upya mahakama yake ya mwanzo, alizitaja mahakama zingine zinazohitaji ukarabati kuwa ni Mufindi (Kibao), Kasanga (Igowole) na Malangali inayotakiwa kukarabatiwa choo na jengo la kutunzia vielezo.

Alisema mahakama hiyo inahitaji pia kujengewa chumba cha mahabusu Malangali na fedha ya kuwezesha kupatikana kwa umeme mbadala katika mahakama ya mwanzo Kibengu

Pamoja na maombi hayo, wazee wa baraza la Mahakama ya Mwanzo Mafinga wameulalamikia uongozi wa mahakama ya Wilaya hiyo kwa kutowalipa fedha zao za vikao vinavyohusisha kesi zilizofutwa.

Akiwatia moyo kwa kazi wanazofanya Jaji Shanghai alisema: “kuanzia sasa baraza la wazee litalipwa fedha zao kwa wakati hata kama kesi wanazohudhuria zitahirishwa au kufutwa.

Akizungumzia utendaji wa mahakama, Shaghai aliwaomba  mahakimu  kujiepusha na rushwa kwa kuwa ni moja ya sababu inayokwamisha upatikanaji wa haki katika chombo hicho.

Aliahidi kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kukabiliana na watendaji wenye tabia za kuomba na kupokea rushwa.

MCHUNGAJI MWASUMBI AACHILIWA HURU BAADA YA HUKUMU YA MIAKA 30 JELA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI, MAGEREZA WALIA KUMKOSA MHUBIRI WAO

Mchungaji Mwasumbi akiwa mahakamani mwaka jana.
Hatimaye Mchungaji Daniel Mwasumbi ambaye mwaka jana alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Mbeya kifungo cha miaka thelathini (30) jela Julai mwaka 2013 kwa tuhuma za ubakaji hapo jana tarehe 3 Juni ameachiwa huru na Mahakama kuu kanda ya Mbeya  huku akiwa anatetewa na wakili wa kujitegemea Benjamini Mwakagamba mbele ya jaji Atuganile Ngwala, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na Prosista Paul.

Kwa mujibu wa WAPO Radio FM 98.1 kupitia kipindi cha Yaliyotokea kinachorushwa saa moja usiku, ripota kutoka mkoani Mbeya bwana Ezekiel Kamanga ambaye alifika mahakamani hapo, anasema kwa upande wa utetezi wakili Benjamini Mwakagamba aliwasilisha sababu saba ambazo zilikuwa zikiomba mahakama hiyo kumwachia huru kutokana na hakimu kukosea kuzingatia moja ya mashahidi ambaye alikuwa ni shahidi wa kwanza.

Ameongeza kuwa pili ni kuwa hakimu alikuwa ameegemea ushahidi wa upande mmoja tu hivyo mahakama haikuwa na haki ya kumfunga kifungo hicho cha miaka thelathini . La tatu ni kuwa hakimu alitumia maoni yake binafsi kumfunga mshtakiwa hali ambayo ni kinyume cha sheria. Sababu ya nne ambayo ilitolewa na upande wa utetezi ni kutumika kwa kivuli cha kadi ya kliniki hali ambayo haikuwa ni halali kuweza kuwakilisha kama upande wa ushahidi.

Lakini  sababu nyingine ni kuhusu kuchelewa kwa vipimo vya DNA kutumwa jijini Dar es Salaam huku pia sababu nyingine ikielezwakuwa kubwa ni kukosewa au kutozingatia muda wa kesi hiyo mara baada ya kufikishwa polisi kutumia mda mrefu tangu kukamatwa, kwani ilichukua takribani miezi minne ndipo alipokamatwa mtuhumiwa hali ambayo mahakama ilitilia shaka na hivyo kwa upande wake jaji Atuganile Ngwala kuamua kumwachia huru kutokana na sababu hiyo ni kwamba hivi sasa mchungaji Daniel Mwasumbi atakuwa huru  ambapo kesi hiyo ya rufaa namba 59  ya mwaka 2013 ikimalizikia hapo, ali iliyopelekea watoto wa Mchungaji Daniel Mwasumbi kuangua kilio cha furaha mahakamani.

HAKIKA MUNGU NI MWAMINIFU NA AHADI ZAKE NI ZA MILELE MWANAMKE SUDAN ALIYEHUKUMIWA KIFO, KUACHILIWA HURU


Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya maswala ya kigeni nchini Sudan amesema kuwa mwanamke aliyepewa hukumu ya kifo kwa kubadili dini yake ya kiislamu,Meriam Ibrahim atawachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo.

Abdullahi Alzareg ambaye ni katibu katika wizara hiyo amesema kuwa Sudan inatilia maanani uhuru wa kuabudu na kwamba serikali itamtetea mwananmke huyo.

Kumekuwa na shutma za kimataifa kuhusu hukumu aliyopewa mwanamke huyo.

Meriam Ibrahim anazuiliwa katika jela moja ambapo alijifungua mtoto wa kike juma hili.

Ameolewa na mkristo na pia amehukumiwa kuchapwa viboko mia moja kwa kuzini kwa sababu mwanamke wa kiislamu kuolewa na mkristo ni haramu kulingana na sheria za Sudan.

chanzo BBC Swahili.

Soma HAPA ZAIDI 

Daniel akiwa amembeba motto wake aliyezaliwa wiki iliyopita.
Meriam akiwa amebeba motto wake aliyejifungua huko gerezani
Meriam na mumewe, pembeni mtoto wao wa kiume anayeishi naye jela.

  SOLOMONI MKUBWA AING'ARISHA TANZANIA KWENYE TUZO ZA GROOVE NCHINI KENYA BAADA YA MWAKA JANA KUCHUKULIWA NA CHRISTINA SHUSHO.

Siku ya jumapili kulifanyika utolewaji wa tuzo maarufu za injili nchini Kenya ziitwazo Groove Awards, katika tuzo hizo ambazo zilikuwa zikifanyika kwa mara ya tisa. Safari hii tuzo iliyokuwa ilishikiliwa na mwanamama Christina Shusho mwaka jana ya mwimbaji bora Afrika mashariki na kati safari hii imechukuliwa na mwanakaka Solomon Mukubwa ambaye ametambulishwa kuwa anatokea nchini Tanzania, huku kwa upande wa Afrika ya magharibi mwanakaka aliyetamba na kundi la Joyous Celebration mchungaji Agu Uchechukwu au mwite Uche Double double ameondoka na tuzo hiyo.

Hata hivyo kwa upande wa nchini Kenya mwanamama Sarah Kiaire ameondoka na tuzo mbili, huku mwanadada matata aliyempa Kristo maisha yake aitwaye size 8 aliondoka na tuzo ya video bora ya mwaka kupitia video ya wimbo Mateke. Kwa watu wengine waliopata tuzo hizo, soma orodha chini.

GROOVE AWARDS 2014 WINNERS


Collabo of the Year … Ngai Ti Mundu by Betty Bayo ft Mr. Seed
Size 8 akizungumzia tuzo yake.



Western Song of the Year … Khwekanile by Geoffrey Kwatemba



East and Central Africa Artiste of the Year … Solomon Mkubwa



Central Song of the Year … Busy Busy by Betty Bayo


Ragga/ Reggae song of the Year … Live up by Hopekid


Western African Artiste of the Year … Uche


Audio Producer of the Year … Jacky B
Mtoto wa kiume wa Sarah K akipokea tuzo kwaniaba ya mama yake.




Nyanza Song of the Year … Christine Otieno



Southern Africa artiste of the Year … Pompi



Lifetime Achievement Award … the Late Peter Kaberere



Radio Presenter of the Year … And the Radio Presenter of the Year is Anthony Ndiema of Radio Maisha


Album of the year … Kirathimo


Pwani Song of the Year … Ahadi za Bwana by Pastor Anthony Musembi



Dance Group of the Year … Gospel Warriors
Baadhi ya umati uliohudhuria, wakifurahia jambo.



Rift Valley Song of the Year … Laleiyo by Shiro Wa GP and L Jay Maasai



Video of the Year … Mateke



Worship Song of the Year … Hakuna Silaha by Sarah K.



Songwriter of the Year … Sarah K.



Eastern Song of the Year … Kitole by Stephen Kasolo

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog