Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''
KWA TAARIFA YAKO''
ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la
kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia
yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au
kuna sehemu haina ukweli utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment
yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo kwa mwanadada aliyetokea kuteka masikio ya wakazi wa Afrika Mashariki kupitia wimbo wake "
AHADI ZAKE" uliomtambulisha vyema na kumpatia tuzo huko nchini kwao Kenya, huyu si mwingine bali ni Marion Wyali Shako.
KWA TAARIFA YAKO kama ukuwahi kufahamu hili au kusoma makala
tuliyowahi kuandika kuhusu mwimbaji huyu na wimbo wake wa huo ambao
wengi waliousikia mara ya kwanza walidhani mwimbaji ni Beatrice Muhone
ni kwamba, kupitia Wapo Radio Fm akihojiwa katika kipindi cha ''Safari
ya jioni'' alisema wimbo wa
AHADI ZAKE ambao upo ndani ya album yake ya ''
MSAADA WANGU''
alipewa neno la kinabii na nabii Teresia Wairimu kwamba Mungu atampa
wimbo utakaobadilisha maisha yake na watu wengine,wakati anapewa unabii
huo alikuwa katika hali ya uhitaji sana na album yake hiyo mpaka
anaifanikisha kuirekodi ni Mungu mwenyewe alimsimamia kwani alimaliza
salio lake lote alilokuwa nalo na pia alipitia mapito magumu sana.
KWA TAARIFA YAKO Marion Shako ambaye licha ya kuwa ni mwajiriwa
pia anajihusisha na biashara huko kwao Mombasa Kenya kutokana na kupata
maswali mengi ya watu kila anakokwenda kuhudumu kuhusu lini ataolewa
ilibidi adanganye kwenye moja ya shoo ya mchekeshaji maarufu wa Kenya
aitwae Churchill ambako aliulizwa swali kuhusu harusi yake lini bila
kusita Marion alijibu itakuwa hivi karibuni kitendo ambacho alijutia
baadae kwakuwa alidhani amepunguza maswali kumbe ndio yalikuwa
yameongezeka na watu kutaka kujua undani zaidi wa harusi yake itafanyika
lini na ninani muhusika mkuu, kitendo cha kuulizwa sana maswali ikabidi
aweke jibu hadharani kwamba hawezi kuzungumzia masuala yake ya uhusiano
hadharani na kwamba hategemei kufunga harusi kwa mwaka huo(ilikuwa
2011, GK haijui kama amefunga kwasasa pia) na kusema kwamba aliamua
kusema anafunga harusi karibuni ili kuwaridhisha mashabiki na watu
waliokuwa wakimuuliza maswali hayo kwakuwa walitaka jibu kama hilo. kama
alivyofafanua kwenye mahojiano na gazeti la
The Star