Ngao ya Jamii Ligi Kuu England ni Chelsea Vs Arsenal Jumapili hii,wengine je?..

Kipenga cha kuanza kwa ligi kuu ya England msimu mpya kinatarajia kupulizwa jumapili hii wakati mabingwa Chelsea watakapovaana na Arsenal katika mchezo wa ngao ya jamii.
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Wembley,London.
Ligi kuu ya Uingereza inatarajia kuanza Agosti 8 kwa michezo sita ambapo Manchester United vs Tottenham katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford wakatiBournemouth vs Aston VillaNorwich city vs Crystal palace ,Everton vs Watford naChelsea vs Swansea city.

LOWASSA Aahidi Kuishinda CCM Uchaguzi Mkuu 2015


Waziri mkuu wa Zamani Edward  Lowassa  amewaahidi wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja na wale wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.

Lowassa alisema hayo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Demkorasia na Maendeleo ambayo itampa ridhaa ya kugombea urais kupitia umoja wa Katiba ya wananchi ukawa unaundwa na vyama vinne vya siasa nchini Tanzania ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, Cuf na NLD.

Aidha, Lowassa aliyekabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe katika ofisi za Chadema makao makuu yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam jana,alichangiwa kiasi kadhaa cha pesa kitakachomsaidia katika yake ya matumaini iliyofufukia Ukawa. Katika hafla hiyo  Lowassa aliongozana na Mkewe pamoja na wana familia na ndugu wengine mbalimbali.

Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba  ili mgombea ameweze kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni lazima awe mwanachama wa chama chochote cha Siasa nchini Tanzania, hivyo Lowassa ni mwanachama halali wa Chadema pia amechaguliwa na vikao mbalimbali vya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi hadi usiku wa manane.

Uamuzi wa Lowassa kugombea Urais ulipokelewa kwa shangwe na umati wa wananchi uliohudhuria hafla hiyo makao makuu ya Chadema kinondoni jijini Dar es salaam.

Mwanasiasa huyo Mkongwe atapambana  na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi Dk.John Magufuli katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu utakaokuwa wa aina yake  mwaka huu wa 2015.

Lembeli ashinda kura za maoni Chadema, Bulaya almanusura.......Viti maalumu vyamuokoa

Wabunge wawili waliohama CCM hivi karibuni, James Lembeli na Ester Bulaya wamepitishwa katika kura za maoni kuwania ubunge kupitia chama chao kipya.

Wakati Lembeli akipitishwa kwa kura za kishindo kuwania ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini, Bulaya alishinda katika nafasi ya viti maalumu baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro cha Jimbo la Bunda Mjini.

Wanasiasa hao sasa wanasubiri uteuzi wa Kamati Kuu ya Chadema utakaofanyika Agosti 5 na 6.

Ushindi wa Lembeli
Katika uchaguzi huo wa juzi, mbunge huyo wa zamani wa Kahama aliwabwaga wenzake 13 aliogombea nao akipata kura 168 kati ya 262 zilizopigwa, akifuatiwa na John Katibu aliyepata kura 45, Peter Shita (17) na Emmanuel Madoshi aliyepata kura 10.

Wengine ni Muta Nyerere (4), Felician Maige (4), Zacharia Obadia (3), Tadeo Mwati (2), Arnold Mtajwaka (2), Prosper Denga (2), Deusdedit Madinda (1), Reuben Macheyeki (1). Victor Mbwana na Richard Makingi waliambulia patupu. Katika uchaguzi wa viti maalumu, Winfrida Mwinula alishinda kwa kura 34 akifuatiwa na Salome Makamba aliyepata kura 30.

 Bulaya
Kama isingekuwa ni kura za maoni za viti maalumu zilizomfuta machozi, Bulaya alikuwa tayari ametupwa nje baada ya kuanguka katika Jimbo la Bunda Mjini.

Bulaya aliyekuwa miongoni mwa makada saba wa chama hicho waliokuwa wanawania kuliwakilisha jimbo hilo, alipata kura 37 kati ya 182 zilizopigwa akiwa nyuma ya Pius Masururi aliyeibuka mshindi kwa kura 65 na  Magembe Makoye aliyepata kura 40.

Baadaye katika mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), uliofanyika baadaye usiku, Bulaya alipata kura 71 kati ya 110 zilizopigwa na kuwabwaga Godliver Masamaki aliyepata kura 31, Joyce Sokombi (4), Minza Shani (3), Dk Jane Nyamsenda (1) na Alice Wandya aliyeambulia patupu.

Awali, Bulaya alikwaa kisiki baada ya jina lake kuwa miongoni mwa waliokatwa na kamati ya utendaji inayosimamia majimbo hayo wakidaiwa ni wageni katika chama; wapenda fujo na matabaka, akiwa pamoja na Chacha Nyamhanga, Sulemani Daudi lakini walirudishwa kundini baada ya kikao cha viongozi na watiania.

Katika Jimbo la Bunda Vijijini, Sulemani Daudi aliibuka mshindi kwa kura 84 kati ya 127 zilizopigwana kuwashinda John Masenza aliyepata kura 14, Dk Lucas Webiro (11), Frank Mongateko (8), Edgar Chibura (5) na Mathias Bandio aliyepata kura moja.

CUF Wakanusha Kujitoa UKAWA.......Wasema UKAWA Haina mgombea Urais Mpaka Sasa. Wawashangaa CHADEMA Kutaka kumtangaza Dr. Slaa


Chama cha wananchi CUF kimekanusha madai ya kujiondoa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA na kusisitiza kuwa chama hicho hakitajiondoa, na kwamba mgombea wa urais kupitia UKAWA bado hajapatikana.
 
Chama cha Wananchi (CUF), kimesema hakikushiriki kikao cha juzi cha UKAWA kutokana na sababu za kikatiba za ndani za chama hicho kwa sababu wao kama chama bado wanajadiliana ili kuafikiana kwa maslahi mapana ya taifa kama vyama vingine vinavyofanya na sio kweli kwamba wamejitoa katika umoja huo.
 
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara Mhe. Magdalena Sakaya amesema kwa sasa wamekuwa na vikao vinavyojadili kwa upana juu ya namna watakavyogawana madaraka endapo wakishinda uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
 
Akizungumzia nafasi ya mgombea urais anayependekezwa na chama hicho ,Mhe. Sakaya amesema Mwenyekiti wa chama CUF Prof.Ibrahim Lipumba aliposema wamtangaze mgombea urais wa UKAWA Julai 14 mwaka huu alikiuka vikao vya maamuzi vya chama hicho ambavyo vilikuwa bado havijakaa kutoa maamuzi.
 
Aidha, Magdalena Sakaya amesema kuwa UKAWA bado haijapata mgombea urais na kuongeza kuwa chama hicho hakitambui taarifa iliyotolewa na baadhi ya viongozi wa UKAWA kuhusu kupatikana kwa mgombea ambaye anasubiri utambulisho rasmi.
 
Sakaya amesema kwa mujibu wa taratibu za UKAWA, wagombea wote wanapaswa kwanza kupitishwa na vyama vyao, halafu wakutane pamoja kama UKAWA kuamua ni yupi agombee, jambo ambalo halijafanyika hadi sasa.
 
"Katika mkutano wa juzi sisi CUF hatukuwepo, sasa wanasema wamempata mgombea urais, watampataje bila chama kimoja kuwepo? ukweli ni kwamba bado mgombea wa UKAWA hajapatikana, lakini atapatikana baada ya taratibu tulizojiwekea kufuatwa" Amesema Sakaya.

Wakenya kumpokea Obama wakiwa uchi ?



Kundi la Wakenya, limejiapiza kumkaribisha rais wa Marekani, Barack Obama, nchini kwao wakiwa hawajavaa nguo ili kuonesha kuwa hawajakubaliana na kitendo cha kuruhusu mapenzi ya jinsia moja.
 
Obama anatarajiwa kutembelea Kenya kwa mara ya kwanza tangu kuwa rais na kutegemea kuwa na mkutano na wafanyabiashara kuanzia Julai 24-26 mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa barua iliyosambazwa na kundi hilo la wakenya, imedai kuwa watafanya maandamano ya amani jijini Nairobi, Julai 22 na 23 mwaka huu kuanzia Uhuru kona.
 
Wamedai kuwa maandamano hayo yatafanywa na wanawake pia wanaume takriban 5,000 wakiwa watupu bila nguo yoyote kupinga Umoja wa nchi za Amerika kupitisha sheria ya mashoga kutambuliwa kisheria.
 
Wamesema lengo kuu la maandamano wakiwa uchi ni kumuonesha na kuelewesha rais Obama, utofauti uliopo kati ya wanawake na wanaume.
 
Wiki iliyopita, Wakenya hao walienda katika mitaa kuandamana wakimuonya rais Obama, kutothubutu kuzungumzia suala la haki za mashoga kwenye ziara yake ya kutembelea nchi hiyo.
 
Mbunge Charles Njagagua, pia aliwataka wabunge kumfukuza Obama, nje ya Bunge mara moja akigusia haki za mashoga.
 
Naye Makamu wa rais nchini Kenya, William Ruto, hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wananchi wake kuwa wamesikia kuwa Marekani wameruhusu uhusiano wa mashoga na mambo mengine yasiyo na maadili na kuwataka viongozi wa dini kutetea nchi yao na kusimamia imani ya nchi yao.

Matokeo kidato cha sita 2015 yatangazwa....Bofya Hapa Kuyaona


Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2015 yametangazwa leo. Kuyaona matokeo hayo angalia hapo  chini….
 

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog